Maziwa yepi mkuu, haya yaliyochakachuliwa ambayo lita mbili inachanganywa na lita tatu za maji?Dah... basi kuleni matunda na maziwa kwa wingi sana...
🙄🙄🙄🙄Nimekuja nimeona bi mkubwa anafagia uwanja nimejibanza hapa kwenye mkorosho,.akitoka tuu......utafurahia shoo sugar babu
Ndio kukosa maarifa kwenyewe huku mzee mwenzangu,.watu wanawafurahisha watu ambao hawana muda nao..badala ya ku-focus kwenye pendo lao na kulistawisha..huko ni kujilisha upepo tuu..Kweli kabisa mkuu, kuna watu wanateketea kwa ndani lakini ukiwaangalia kwa nje unaweza ukawaonea wivu ukidhani wananufaika hasa huko ku-show off kwao huko.
Mleta uzi emu tugonge selfiee kwanza...[emoji91][emoji91]Habarini JF,
Swala la kudumu katika mahusiano limekuwa tatizo Sana kwa dunia ya Leo na wengi wamekata tamaa na kufanya maamuzi ambayo sio ya kujenga Bali yanaharibu taswira yake katika jamii inayomzunguka.
Wengi wanachukulia kawaida lakini ni jambo ambalo linatakiwa lipatiwe ufumbuzi ili kuokoa vizazi vinavyokuja.
Dunia ya Leo watu wenye umri chini ya miaka 18 wanajihusisha na mahusiano ya mapenzi ambapo mpaka anafika age ya under 25 tayari anakuwa ameshapitia changamoto nyingi ambazo wengine huishia kujiua na wengine kukata tamaa kabisa ya maisha.
Dunia ya Leo invavishawishi vingi kila kitu kipo mtandaoni na huwezi kumpangia MTU kutumia simu na kupitia hii hali picha za ngono zinaangaliwa for free kwa asilimia kubwa Sana wadogo kwa wakubwa, mwisho wa siku ushawishi unakuwa mkubwa na watu kujiingiza katika maadili yasiyoendana na Jamii inayomzunguka.
Kuna sakata la kujianika mitandaoni na kuonyesha uchafu unaofanyika Kati ya wapenzi wawili, yaani sijui kwanini watu wanafanya hizi drama halafu baadaye unasikia Mara simu ya mpenzi wangu iliibiwa sijui ,, hivi kwani ni lazima watu mnavyokuwa faragha mjichukuwe video? Unapata faida gani? Sijui tunakwama wapi kwa kweli na aliyetologa nahisi na yy alilogwa.
Swala LA kudanga, Leo upo na huyu kesho upo na huyu na hapa sio kwa wakike tu hadi wanaume pia isee, hivi huwa tunatafuta nini hasa inashindikana nini kuwa katika mahusiono yakudumu? Yah wakati mwingine tunamsingizia shetani sawa inatokea umechepuka labda kwa tamaa ya kitu Fulani lakini kwanini usitulie sehemu moja kwanini kila siku tamaa ikutawale ifike mahali tujizuie na hizi tamaa maana mwisho wa siku thamani ya mwili wako ndo unaporomoka na itafiki kipindi hutakuwa na thamani tena.
Kikawaida kwenye mahusiano kuna milima na mabonde hili halikwepeki, mfano hata mm nimeshakuwa katika mahusiano mpaka sasa nipo na MTU niliyeanza naye mahusiano kutoka 2013 mpaka sasa ninaye na Kama kugombana tumegombana, tukasusiana zaidi ya hata mwaka lakini mwisho wa siku watu mnakaa chino mnamaliza tofauti zenu mnaendelea na maisha.
Mapenzi yasiku hizi yametawaliwa na PESA, bila pesa ujue unatakiwa ujipange lakini hebu tujiulize mababu na mabibi zetu enzi hizo waliwezaje kudumu katika mahusiano maana pesa zilikuwepo lakini kwa system iliyopo sasa zamani haikuwepo. PESA ni Shetani tena ni Pepo chafu Sana linatakiwa likemewe kwa hali ya juu.
Watu wamejengea kuwa mahusiano ni kufanya mapenzi na kushikana shikana tu, lakini swala LA kufanya mapenzi sehemu tu ya burudani ambayo inafanywa kwa dakika chache na linapita, lakini kuna mambo ya kuhusishana ya kimaendeleo ambayo yanaweza kujenga maisha ya sasa na ya baadaye kwa kizazi na kizazi.
Ukiamua kumpenda MTU mpende maana hujui kesho yake itakuaje Leo anaweza akawa anapesa kesho asiwe nazo, au Leo anaweza asiwenazo kesho akawa nazo kwa hiyo maisha tunayopitia kuna kupanda na kushuka,
Kumshirikisha Muumba wako pia ni jambo jema kwani yeye ndiye aijuaye kesho yetu na yy ndiye awezaye kutupatia wenza watakao weza kukidhi mioyo yetu na kuleta faraja katika familia...asante kwa kusoma na ruksa kunikosoa pale nilipokosea
Daah...na ww umeanza vizur Ila umemalizia vibaya...haujaanza vibaya saana, ila umemaliza vibaya
some time iache teknologia ifanye kazi yake
hivi mleta mada we unaweza ukapanga maisha na wanawake wa kileo au mzuka ndo umekupelekea kuandika bila kufikiri
Sawa nimeipenda hii selfieMleta uzi emu tugonge selfiee kwanza...[emoji91][emoji91]View attachment 912428
Yah...tunapepo lakuiga ambalo halina manufaa kwetu zaidi ya kutuumizaYani tulivyo wapumbavu tunajifanya Tunaiga wazungu wakati wazungu wao wapo serious saana na Relationship zao hawana Mamichepuko cjui kudanga cjui kibamia hizo pumba kwao hamna kabisa sasa sisi cjui tunaiga wazungu gani? Mahusiano ya Kibongo bongo kama wanyama vile unakuta demu ana wanaume si chini ya wanne na msela nae ana mademu si chini ya watano unadhani hapo kuna nn tena?
Yah..ni kweli wadada zetu wanajisahau Sana wakati mwingine muda wao wakuanza maisha unapofika mwingine utasikia nakula raha kwanza, mwingine anakuambia sitaki maziwa yangu yachoke sababu ya kunyonyesha, mwingine anakuambia natafuta pesa kwanza, so inafika kipindi umri umeenda ndo anaanza kuhangaika kutafuta wa kumuoa mwisho wa siku unaingia kwenye ndoa isiyokuwa na mahusiano mazuriFor my opinion naona kwa zama hiz kuoa mwanamke ni mtihani mwengine katika maisha ambao unahitaj kuwekewa mikakati mizur ili kufuzu mitihan hiyo. Maana wanawake wa sasa huwa na akili njema na maonk mazur ya kimaisha baada ya umri stahiki wa kjolewa kumpita yaana akiona kama umri unamkata mkono na kashazalishwa na kakimbiwa bas huwa mpole na kukubali yaishe kitu ambach sio kizur kwake ilipaswa awe tayar pale alipoona amechezewa na wanaume zaid ya 5 na bdo hakuna dalili ya ndoa bac angetulia na luchunguza kwa makink whos perfect katika mahusiano na kuamua maamiz sahihi.
Nawasilisha wazo langu. Wanawake wa kileo wanapemda kupitiliza muda ndio waukimbilie. Asanteni
Yah..well said lakini kuna huyu MTU anaitwa globalization ni mdudu mbaya Sana ambaye anazidi kuharibu kizazi kwa kizazi1. Love is a loaded gun.
2. Mapenzi hayana user instruction guide.
3. Mapenzi ni chombo cha moto, yanahitaji lesseni.
Mwisho, kama tungeweza kutokujihusisha na mahusiano kabla ya ndoa, na tukadumu kuwa waaminifu baada yabkuingia kwenye ndoa, matatizo mengi ya mahusiano yasingekuwepo.
Mkuu umeandika kweli tena kwa hisia..na tena tunaoangamia ni sisi vijana kwa kukosa maarifa..wengi tuna elimu lakini hatuna maarifa,adui kauteka ufahamu,.tumejawa na upumbavu,ujuaji mwingi,kujifanya"don't care",majivuno,uzungu mwingi ilihali tunaishi kwenye "jumba bovu"
Wengi ni "mifupa mikavu" na haitaki kuishi tena imeng'ang'ana na mizaha huku inateketea..kutokujua pia nini unataka nayo ni shida.
Dash...umetema point Sana nahisi kila mmoja wetu amepata kitu hapaMleta mada, leo uminifurahisha sana....hivyo natanguliza shukrani zangu dhati kwako kwa jitiada unazozifanya ili kuikomboa jamii yako.
Pili, napenda kuunga mkono hoja, kiukweli hiki kinachoendelea sio kitu chema hata kidogo katika jamii zetu, na niwe tu mkweli, mimi ni miongoni wa waathirika wa hili sakata....anyway naomba niende moja kwa moja kwenye kuchangia mada.
Kiukweli siku hizi wanawake kwa wanaume, wamekuwa na dhana ya kulichukulia suala la mahusiano ya kimapenzi katika uzito mdogo mno, jambo ambalo sio sahihi hata kidogo. Na ndilo linalotufikisha hapa leo hii tulipo, ukijaribu kufatilia kwa makini kuhusu hili ninaloliongea, bila shaka utabaini kuwepo kwa utofauti mkubwa sana, ulipo kati yetu sisi vijana na wazee wetu, hasa wa miaka ya 50-70. Kutokana na hali hiyo kuibuka, tumejikuta kwenye mazingira ya kuchukulia poa hata hali ya mtu kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi leo na kesho. Na wengine wanaemda mbali zaidi, hata kufikia hatua ya kuamua kuifanya miili yao kuwa bidhaa, kwa lugha nyingine naweza sema WANAJIUZA.
Naomba nianze tu kwa kusema kwamba, hili jambo linaloendelea kuzitafuna jamii zetu, ni matokeo hasi ya mbegu nyingi sana. Mbegu zenyewe ni malezi, utandawazi, hali za kiuchumi, hali za kiafya, suala la elimu na suala zima la mapenzi yenyewe. Lakini mimi leo nitajikita zaidi kwenye hiyo mbegu ya mwisho niliyoitaja hapo juu (mapenzi).
Suala la mapenzi, ni suala moja nyeti sana....na ndio msingi mzima wa suala zima la mahusiano............(nitarudi baadae kidogo)
Yah..ni kweli ulisemalo na hali Kama hii inapotokea ndipo hapo michepuko inaanza na hii sio kwa upande wa wanawake tu hadi wanaume pia huwa sisi ndo chanzo cha michepuko😁😁Niliwah kumpenda msichana mmoja hivi,hakika nilimpenda kwa dhati na sikuwahi kuchiti hata siku moja...nilimuonyesha mipango ya maisha yetu ya baadae yaan nilitulia haswa na kumuona kama mama yangu wa pili baada ya mama mzazi,ila akichokuja kunifanyia sitasahau na sitarudia kuwekeza akili yangu kwa mwanamke tena ...pia nikajifunza kutomuamin mwanamke tena na hadi kesho siwaamin hawa viumbe...saiv ninae mmoja ila michepuko siachi ng'oo maana sitak kufa kwa stress za kuachwa na mwanamke tena ....
Hakuna apendaye kuwa na michepuko ila michepuko ni kama vaccine ya mioyo yetu ili pale tunapoumizwa na tuliowapenda bhc tupate walau sehemu ya kupozea machungu yetu.
NB: Huu n mtazamo wangu baada ya kuumizwa....kila MTU anao wakwake
Thank you... Ila sijamaliza, nitamalizia baadae kidogo. Naamini utajifunza mengi sana nitakapomalizia.Dash...umetema point Sana nahisi kila mmoja wetu amepata kitu hapa
PamojaThank you... Ila sijamaliza, nitamalizia baadae kidogo. Naamini utajifunza mengi sana nitakapomalizia.
WELCOME