Tunajisifia magofu waliojenga wazungu na Waarabu

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,331
2,462
Inabidi tabia ya kuonyesha history ya Tanzania kwa kuonyesha magofu waliojenga wazungu ife kabisa kwasababu sio vitu vyetu na hatuwezi kufafanua style na ubunifu uliotumia kwasababu sio sisi tuliojenga

Kama ni history yatupasa kuonyesha sehemu kutoka viongozi wetu wa jadi wa zamani na mahali waliopo kuwa wakiishi kama mkwawa, mirambo na ngome zao ambazo zimeliwa na mchwa na tueleze imekuwaje mchwa wakaweza kula nyumba nzima kilitakiwa kifanyike nini wasiweze kula.

Kuonyesha majengo kunamanisha kwamba tunataka wazungu na waarabu waje tena kututeka kwani tunaonyesha tumemisi mapenzi ya mshumaa tuliokuwa tuwakiwaonyesha ya kukubali kuchukuliwa kama bithaa nyingine na kufanya nao biashara isiyo na mlinganyo sahii.

Magofu yote yahifadhiwe ili wakija waliojenga waone jinsi walinyokuwa watalamu wa kujenga na sifa zote wachukuwe wao kwamba wamekuja wametukuta tunazubaa wakajenga majengo marefu tukashangaa wakatufanya watumwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom