Django
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 354
- 147
VIONGOZI na wananchi kwa ujumla wetu tuna kila sababu na wajibu wa kujitadhimini wapi tulikotoka, tulipo na tunapokwenda. Taifa letu la Tanzania ni wazi huenda limejikwaa na hata kuinama kwa kuweka viganja kuelekea chini ili kuweza kujizuia na kishindo cha anguko la uchumi wetu.
Mwelekeo wa nchi umebadilika kwa Watanzania kuamua kutafuna nguo zetu bila kuwa na uwezo wa kununua nyingine, tumeamua kujiweka wazi kwa kujinadi hatuna vurugu, tumejaa upendo, huku tukiogopa kukabiliana na hali halisi inayotukabili.
Si haki kuwalaumu viongozi kwa ngonjera nyingi na nyimbo za mapambio bila kufanya tafakuri jadidi kwa namna jahazi linavyozidi kutota eti tunashangilia kwa kuimba wimbi wa amani na utulivu.
Kwa sasa tuendako ni kubaya kutokana na hali ya umaskini kusababisha kununuliwa na wabaya wasioitakia mema nchi yetu na watu wake hali ya kuwa kundi kubwa la vijana wengi hawana ajira za kuweza kujenga maisha bora.
Hatari kubwa ni kununulika kwa kuchafua amani tunayoilingia, watatokea magaidi kupenya katika mipaka yetu wakitumia fedha zao na kuweza kuwanunua baadhi ya vijana ili wafanye vitendo vya kihuni pasi na kuona uchungu wa damu za Watanzania wenzao ili mradi tu apate fedha.
Kwa namna tulipofikia sasa ni vema kwa mamlaka zinazohusika kuweza kuchukua hatua za makusudi ili kuweza kuboresha uchumi kama njia kuondoa moyo wa ushawishi wa kutumika na mabeberu ambao wana nia ovu kwa nchi yetu na watu wake.
Tujipange kwa kuweka sheria kwa Watanzania ili nao waweze kumiliki rasilimali za nchi, ambapo kila anayetaka kuwekeza lazima aingie ubia na watanzania.
Mtaji wa Watanzania ni rasilimali zilizopo na si kuwanyanganya fursa ya ardhi na kuwapa wageni.
Vitendo vya kuwanyanyasa wazawa ni hatari kwani vitendo hivi ndivyo vinavyowafanya vijana wengi kukimbilia mijini kila kukicha.
Ikiwa Serikali itaweka mazingira mazuri kwa maeneo ya vijijini ni wazi kundio hili la vijana linaweza kuzitumia huko walipo kuliko kuzifuata mijini.
Na ikiwa viongozi watatambua wajibu wao na hata kujiuliza kila mmoja wenu anawajibika vipi kuupiga vita umasikini, na kuacha kujinufaisha kwa unafsi wa mali za walipa kodi wanyonge ni wazi Taifa linaweza kusonga mbele kwa kuwa na uchumi imara.
Taasisi zilizobeba dhamana ya kusafisha nchi hii zifanye kazi bila kuegemea upande wowote, na ziache kuendeshwa mawazo na mikono ya vigogo wa serikali kwa kujitemegea kama njia ya kuweza kunusuru uchumi.
Kila mara watu wamekuwa wakijiuliza inakuaje Tanzania kuna utajiri wa kila aina lakini watu wake ni maskini wa kutupwa huku wengi wao wakiishi chini ya Sh 640 kwa siku.
Hali hiyo huwafanya hata wengine kushindwa hata kumudu mlo mmoja wa siku kutokana na kuyumba kwa uchumi kuanzia ngazi ya familia hadi kwa taifa ambapo waliopewa mamlaka wameshindwa kutoa muelekeo wa kueleta nafuu ya maisha kwa watu wao.
Leo kundi kubwa la viongozi wa kisiasa limejikuta limejiingiza katika biashara za kuchuma mali kupitia madaraka yao, waliobaki nao huiba katika nafasi zao kwa kutumia usemi wa mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake kwani hii ni hatari na tunaipeleka wapi Tanzania yetu?.