Tunaipeleka wapi elimu yetu ya Tanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaipeleka wapi elimu yetu ya Tanzania??

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Lyamungo, Oct 6, 2012.

 1. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na tabia ya wanasiasa walioko kwenye nafasi zao kama mawaziri kufanya mabadiliko yasioyokuwa na kichwa wala miguu kwenye tasnia muhimu kama elimu bila kuwashirikisha wadau au kujali madhara yake, mfano wa mabadiliko hayo ni:-
  1. Kubadili mihula ya A- Level kama homa za vipindi
  2. Kuondoa michezo mashuleni
  3. Kufuta masomo ya Kilimo, ufundi, sanaa, biashara
  4. Kuunganisha somo la kemia na fizikia
  5. Kuondoa hadhi ya mtihani wa kidato cha pili
  6. Kupeleka walimu wakasome mwezi mmoja wakafundishe
  7. Kubadili mitaala kila mara
  8. Kuidhinisha vitabu visokuwa na kiwango vitumike shuleni
  n.k
  Mshangao wangu ni kuwa wanavyofanya maamuzi ya namna hiyo ambayo hayahitaji sana utafiti wa kina kuyajua yalivyokuwa ya kihuni wadau na wananchi wanakaa kimya kama haliwahusu
  Najiuliza
  1. Huwa wanatumwa na nani na kwa manufaa ya nani?
  2. Wanaoathirika na maamuzi hayo wanafidiwaje?
  3.Tutakaa kimya hadi lini?
   
 2. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Unashtuka leo,wanawalemaza watoto wetu,wa kwao waku Harvard University wanaandaliwa kuja kututawala!Chezea Magamba wweeeeeeeeeee!
   
 3. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Lyamungo, nimekusoma kwa makini,
  Hapo kwenye fidia ndio zaidi panahusika maana vitu kama Ziwa Nyasa leo ukiambiwa haliko Tanzania inakubidi kupitia machapisho yote ili kubadili haya na ni gharama pia. Kizazi cha wasikivu na wanaoona mbali kinakuja kwa mapinduzi na jukwa lao lakusemea ndipo pakupeleka mambo kama haya kwani wananchi wakiungana katika hili nani apingae?
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwani we hujui kuwa Elimu tunaipeleka kuzimu??
   
 5. Jstrong

  Jstrong Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Dah haswa la vitabu visivyo na ubora,haswa vya Oxford.
  Kufuta mitihan kidato cha pili ni upumbavu mkubwa sn kwa maslahi ya kisiasa,na madhara yake ni ya muda mrefu sana
  Hivi wadau pia kuna tofauti yoyote iliyopo kati ya syllabuses za 2005 na 2010 za sec mi sijaona ila nahis kuna ulaji ktk kuchapisha but hamna kipya kabisa wamecopy 2.
   
 6. a

  adolay JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,577
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  Mkuu Lyamungo

  Hatuna viongozi tunawachumia tumbo kiasi kwamba yeyote anapoamua wengine nao hupitisha kwa upumbavu ndiyooo bila kutafakali wala kutathimini athali za mabadiliko ya mara kwa mara kwa Vizazi vya watanzania na Taifa kwa ujumala.

  Suala la elimu limegeuka kitendawili tangu baba wa Taifa aondoke madarakani, hatujapata tena kichwa cha uhakika katika kuwekeza. Enzi za mwalimu ilikuwa jambo la kawaida kabisa watoto wa mawaziliri na wakuu wengine wa serikali kusoma shule moja na watoto wa walalahoi kutoka vijijini. Elimu ya matabaka haikuwepo.


  Enzi za mwalimu japo shule zilikuwa chache heshima ya elimu ya mtanzania ilikuwa juu, ubora wa elimu na uadilifu wa serikali kwa watanzania kuhusu elimu ulikuwa juu sana, walimu walithaminiwa na vifaa vya kufundishia vilipatikana.


  Enzi za mwalimu hapakuwa na elimu ya matabaka kama tunavyoshuhudia hivi sasa, shule za kata moja kwa moja zinaandaa mazingira ya watoto wa wakulima kutawaliwa na aKina malecela, Riziwani na ndugu zake, makamba, mwinyi nk.

  Usitegemee kabisa kuwa na elimu bora unapokuwana Raisi kilaza kama kikwete anaye tukana walimu waziwazi, mishahara mibovu, kuiongeza hataki na kwa kejeli akitumia mahakama kuwakandamiza. (Wakenya wanafahamu kwamba kuchezea elimu ni upumbavu wamejadili na kufikia muafaka na walium)

  Tanzania itabakia kuwa taifa la mbumbumbu kwa muda mrefu kwasababu damu za watawala walewale wenye fikra mgando zinaendelea kututawala unless aina ya watawala wengine wenye uchungu na Taifa tanzania wakaingia madarakani. (kama ilivyo katika michezo na laana yetu ya kichwa cha mwendawazimu)

  Unapoona wanasiasa bungeni wakisifu kwa idadi ya wingi shule na wanafunzi bila kujali ubora wa elimu itolewayo na ubora wa wahitimu hakika Taifa limepotea njia na kuirudia njia sahihi itahitaji kichwa kingine chenye maono ya kweli katika kumkomboa mtanzania.
   
 7. Nguchiro

  Nguchiro JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 365
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Anayebisha abishe ila hakuna wizara niliyotokea kuichukia kama wizara ya elimu kila kukicha ni vioja, kipindi hicho paper darasa la 4, darasa la 7, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita sasa hivi hakuna kitu, kuna siku napita mtaani nakutana na wadogo waliofeli mtihani wa kidato cha pili eti wadogo wanadai average ya 30% paper ya kidato cha pili ni kubwa sana hawawezi kupata hasa kwa wale wa shule za serikali inasikitisha kusikia,pia mtihani wa darasa la 7 kuwa wa kuchagua ni weakness kubwa zile zama za swali,kazi,jibu zimeishia wapi hasa kwenye hesabu?mtoto anafaulu mtihani wa darasa la 7 wa kuchagua kafika sekondari hawezi hata kuandika jina lake yaani ni vioja nasikia kua uvumi kwamba mfumo wa maswali ya kuchagua wanataka utumike sekondari na vyuo vikuu ona balaa litakalotokea hapo, maamuzi ya mfumo mbovu wa elimu yanayopitishwa na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza ni ya kipuuuzi na si ya kuyafumbia macho hata kidogo, wanaoamua watoto wao hawasomi hapa so maamuzi yao hayana madhara yoyote kwao bali kwa walalahoi walio wengi,inasikitisha kuona na kusikia:shule za kata nyingi ni utani,madarasa hayatoshi,mabweni hakuna hela zinatoka watu wanakula, walimu hawana nyumba, maabara hakuna, vyoo hakuna vya kutosha, maktaba hakuna, vitabu hakuna, walimu hawatoshi, jamii hazijitoi kwa maendeleo yao binafsi,unapata wapi ujasiri wa kuita kitu kama hicho shule? unaweza ukatukana bure ukapata Ban bure
   
 8. Haroun jotham

  Haroun jotham Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza wenyewa kwa wenyewa hawaelewan! Kama wazir wa elimu na Necta cos mpaka tm ii six hawajui watafanya mtian wao lin? Wazir alitngaza mwez wa 2 na shule hazjapata walaka znasema mtian wa 5! Upuuz mtup,, 2naumia 2lio chn
   
 9. Nguchiro

  Nguchiro JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 365
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ni matatizo matupu kujadili elimu ya bongo yaani sioni hata penye nafuu pa kupasifia,sisi tumetokea hukohuko ila hali ya sasa imezidi kuwa mbaya kila kukicha tabu tupu dah na usanii ndo 500%,God forbid :poa
   
Loading...