Wakati pilikapilika zikishika kasi kwa wanaotajwa kuanza kampeni za chini kwa chini kutaka kuwania ubunge jimbo la Moshi mjini hapo mwakani,makada wa Chama hicho wameibuka na kisisitiza kuwa bado wanaimani na mbunge wa sasa,Priscus Jacob Tarimo .
Pamoja na kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa wanaoendesha kampeni chafu za kumchafua,Priscus bado anaonekana kukubalika ndani ya chama na kwa wananchi.
Hii inatokana na kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020 kwa aslimia 85 kwa mujibu wa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa.
Taarifa kutoka ndani ya ccm moshi mjini ni kwamba mkakati wa Chama hicho ni kuhakikisha kinashinda Tena uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa na mgombea anayekubalika ndani ya chama na kwa wananchi .
"Nikuambie brother sisi tupo ndani ya chama,tunajua fitina zinazoendelea za kumchafua Priscus lakini nikuhakikishie Priscus ndio chaguo letu wanaccm hao wengine acha watumie pesa zao hakuna anayewapangia matumizi",amesema kada mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Wanadai kuwa maeneo mengi ambayo Priscus aliahidi kwa kiasi kikubwa ametekeleza ikiwamo suala la afya ambako alichangia kwa kiasi kikubwa kukamilika kwa jengo la mama na mtoto katika Hospital ya Rufaa ya mkoa,Mawenzi
"Fuatilia miradi mingi ya maendeleo ndani ya jimbo letu imetekelezwa chini ya ufuatliaji wake ikiwamo ya barabara,shule za sekondari za Kata kwa kushirikiana na waheshimiwa madiwani na mstahiki meya wetu ,Zuberi Kidumo*,anasema kada huyo .
Kada huyo anasema kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Lucy Lameck iliyopo kata ya Majengo na kuanza kuchukua wanafunzi ,ni matunda ya kazi ya mbunge huyo.
Unataka kujua zaidi ya yaliyofanywa na mbunge Priscus Tarimo ?
Kaa mkao wa kula tunakuletea makala iliyosheheni data za kutosha