Tunahitaji tume huru "NEC"

Wakuu,uchaguzi umeisha kilichobaki ni kuanza vugu vugu la kupata katiba mpya kabisa na tume huru kabisa.Wataalamu wa sheria watushauri ni wapi pa kuanzia.Tusitegemee serikali kuvileta hivi wakati wananufaika navyo.Please mwenye njia rahisi na sahihi ili tufikie lengo.Katiba mpya na tume huru ni lazima kwa hii miaka 5,tujitahidi kwa hili.Tuache malumbano tuanze vugu vugu la mabadiliko.Hii ni kwa watanzania wote wenye vyama na wasio na vyama.Toa mawazo yako kitaalamu pia wapi pa kuanzia.Mimi nafikkiri wabunge wote wa upinzania ,vyama vya kiraiya,NGOs,wananchi,taasisi ya haki za binadamu watuanzishie hili.Anayepinga itabidi apelekwe Hospitali ya Mirembe akapime akili yake kama iko vizuri
 
Mkombozi nipo pamoja na wewe asilimia mia nane (800%) Ila tatizo serikali tuliyonayo inafaidika na mfumo wa katiba iliyopo, ambayo inampa rais madaraka makubwa sana. Rais anamteua Mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Mwenyekiti wa Tume, IGP, nk.

Hivyo kwa kuwa mazingira kama haya yamekuwa mateso kwa wengi, dawa yake ni kupeleka Hoja rasmi Bungeni, vyama vya upinzani lisimamie suala hili ikibidi hata mbunge awe tayari kufukuzwa bungeni, kutumia vyombo vya habari kuishinikiza serikali kukubali mabadiliko ya katiba, pamoja na NGO's bila kusahau nchi wahisani.

Tukipata katiba mpya itatupa uhuru wa kujadili mikataba ya madini ambayo ni rasilimali kubwa ya nchi hii, lakini mpaka sasa ni wawekezaji ndiyo wanaofaidi asilimia 97, huku nchi ikibaki na asilimia 3.
 
Ndugu wana JF

Kama kuna mtu ameumia na dhuluma waliyoifanya CCM na NEC yao dhidi ya matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka huu 2010, basi mimi nimeumia zaidi. Ni dhahili kwamba CHADEMA kupitia mgombea wake wa urais Dr. Slaa mtanzania na mzalendo halisi walishinda ila kumefanyika mafinyufinyu na ma+=x<"%$/... hadi nafasi hiyo ikaenda kwa fisadi asiye na mapenzi mema na nchi yetu. Inauma sana, ni heli usijue jambo lolote.

Ok, ngoja nifupishe mada. Kinachotakiwa kwa sasa ni kupatikana kwa tume huru ambayo watendaji wake hawatakuwa waajiriwa wa serikali ya chama kilicho madarakani au chama fulani peke yake. Kwa mtazamo wangu tume hiyo - NEC inapaswa iundwe na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi. Hapo ndipo itakuwa huru na mwanya wa kuchakachua matokeo ya mtu hautakuwepo kwani vyama vyote vitahusika kupitia wawakilishi wao kupokea na kuhakiki matokea kisha kuyatangaza kwa uwazi. Naomba maoni yenu kuhusu jinsi muundo wa tume hiyo unavyotakiwa kuwa ili iwe huru. Bila hivyo CCM itaendelea kutawala mpaka umma uchoke na kuikataa serikali yake. Sasa hiyo siyo leo hii.

Kuna makala/article ninaiandaa kuhusu mtazamo, maoni na mapendekezo ya muundo wa tume hivo mpya. Katiba tumeitengeneza wenyewe na tunaweza kuitengua wenyewe. Let's work out for it!
 
nafasi ya mwenyekiti wa tume ipatikane kwa kufanya application, sifa za applicant zijulikane, awe na security of tenure kama ilivyo kwa majaji! Nafasi nyinginezo zipatikane kwa vyama kuwa na uwakilishi kwenye tume!
 
Asante sana Buchanan.. wengine vipi au hamjui kuwa tatizo lipo kwa NEC na mfumo/mchakato mzima wa kuandaa, kupiga, kuhesabu na kutangaza matokeo ya kura?
 
Ikiwezekana kama hakuna tume huru vyama vya upinzani vigomee uchaguzi wa 2015 bse it shall be useless bse CCM wataendelea kuongoza milele
 
Ndugu zangu,
Kama tulivyojionea uchaguzi wetu mkuu ambao upo ukingoni na chaguzi nyingine za vyama vingi zilizopita. Kuna hitilafu nyingi sana zilizojitokeza katika mchakato mzima wa uchaguzi. Hitilafu hizo ni za kimfumo zaidi kwani matatizo mengi yanayojitokeza yamesababishwa na Tume kushindwa kuwa huru lakini pia kupindishwa kwa makusudi kwa kanuni na taratibu ili kukibeba chama tawala.

Matatizo kama kukosekana kwa wafanyakazi wakutosha wa kudumu wa Tume, au wakurugenzi wa halmashauri kuwa wakurugenzi wa uchaguzi, au majina ya wapiga kura wenye kustahili kupiga kukosekana na matatizo makubwa zaidi kama kucheleweshwa kutangazwa matokeo na hata kuchakachuliwa na kutangazwa kwa washindi wasiostahili yanaondoa uhalali wa zoezi zima na kulifanya kuwa kama mchezo wa kuigiza!

Malalamiko ni mengi mno yenye kuonesha kutokutendewa haki. Tumezoea kuwa ni viongozi wa upinzani wamekuwa wakilalamikia ukiukwaji huu lakini sasa hata wananchi wameonesha kukosa kabisa imani na zoezi hilo. Kuna idadi kubwa ya wananchi (zaidi ya 55%) ambao walistahili lakini hawakupiga kura na wengi wao wamesikika hata kabla ya uchaguzi kutokana na uzoefu wa chaguzi zilizopita walisikika wakisema hawatajisumbua kwenda kupiga kura kwani "hata iweje CCM wataiba kura tu". Hata baada ya uchaguzi wananchi waliokuwa na ujasiri walikesha vituoni kulinda kura zao na hata kufanya fujo walipoona haki yao inaanza kudhulumiwa.

Ni dhahiri hali isipobadilika na tukiendelea na mfumo huu wa hovyo, vurugu zitakuwa ni kubwa zaidi na hata kufikia hatua kama ya wenzetu Kenya.

Rai yangu, tuchukue hatua ili tusifike huko kubaya. Tudai tume mpya na huru ya uchaguzi na mfumo mpya utaotoa fursa na haki sawa kwa vyama vyote. Najua dawa ni kudai katiba mpya lakini hilo kwa wananchi wa kawaida wengi hawaoni kama ni tatizo, hasa kwa kuwa ni la kisheria zaidi, lakini hili la uchaguzi hata wamachinga wanaliona na kulilalamikia.Mfumo huru wa uchaguzi utakuza demokrasia itakayozaa katiba mpya!

Kwa kuwa CCM wananufaika mno na mfumo wa sasa, hawatakubali kuubadilisha kiurahisi. Ndio maana nasema TUDAI! Tusiwaachie wanaharakati na wabunge wa upinzani tu, tudai mfumo mpya wa uchaguzi kwenye social media & web, kwenye serikali za wanafunzi vyuoni na sekondari, mitaani, misikitini, makanisani na hatimaye bungeni.

Wasanii wetu wa ukweli waimbe nyimbo,kuigiza,kuchora ujumbe huu, tutengeneze hata picha maalum yenye ujumbe huo, tuvae kwenye tshirts, kila kona iwe ni kudai MFUMO MPYA NA HURU WA UCHAGUZI.
 
Asante sana ndugu yangu kwa kuliona hilo. Ninasikitika kuwa wana JF karibu wote humu ama hawajui tatizo linalotukwamisha na litakaloendelea kutukwamisha wanaharakati za mabadiliko au ni wana CCM wasiotaka tume nyingine. Nasema hivyo kwa sababu wamekuwa mbele sana kuchangia hoja za kipuuzi na kutupilia mbali topic zinazozungumzia kudai tume huru.

Mi siwaelewi...!!!!!!!!!
 
Unasema kweli, kuna haja ya kudai mabadiliko ya katiba na tume huru ya uchaguzi vinginevyo tutaendelea kuhesabu maumivu!
 
Naona tuanze na tume huru mabadiliko ya katiba yatajiset tuu bse ukiwaangusha CCM definately katiba mpya inafuata.
Naona Slaa itabidi ampe JK masharti ya tume huru na mabadiliko ya katiba kama sharti la kukaa kimya ie kutoongelea madudu ya 2010 election hasa katika ngazi ya uraisi
 
Ngoja niende jukwaa la kikubwa kwanza nitarudi hapa baadaye:smile-big:
 
If you love Tanzania, you won't support CCM. End of discussion.
 
Kufuatia idadi ndogo kupita kiasi ya waliojitokeza kupiga kura, na matokeo ya uchaguzi yaliyogubikwa na dalili za uchakachuaji mkubwa wa kura, wadau wameanza kudai tume huru ya uchaguzi. Hili sio jambo la CHADEMA peke yake wala la wapinzani kwa ujumla wao pekee, ni jambo zito lenye maslahi ya taifa, lipaswalo kuungwa mkono na kupewa msukumo unaostahili na kila Mtanzania mzalendo.

Hali inavyoonekana sasa hivi nchi ipo mahali pa hatari. Nasema ni mahali hatari kwa sababu katiba yetu na mifumo ya utawala imekaa kwa jinsi ambavyo nchi inaweza kuendelea kunyonywa na kikundi kidogo cha wajanja wanaoitumia siasa kwa maslahi yao kwa kutumia katiba hiyo na mifumo yake. Hali ilivyo sasa nafasi yoyote ya uongozi inaweza kununuliwa na wajanja, na mtu asiweze kuhoji wala kupinga mahakamani. Inaweza kabisa kusemwa kuwa katika hali hii, upinzani kuingia ikulu ni ndoto.

Katiba inazuia kuhoji mtu akishatangazwa kuwa raisi. Hii ina maana kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi anayo kura ya turufu ya kumchagua raisi. Haijalishi wananchi wanachagua nani, kama tume ikiamua kubadili matokeo na kumtangaza mwingine basi watanzania hawana budi kukaa kimya. Hii ndiyo demokrasia ya Tz! Lakini pia swala la tume kuteuliwa na raisi ni jambo lingine lisiloingia kichwani. Tangu lini refa wa timu ya mpira akatokana na timu mojawapo? Angalia wabunge wanaoteuliwa na raisi! Hivi hawa wanakwenda bungeni kumwakilisha raisi au wananchi? Inakuwaje wabunge wanaotakiwa kuidhibiti serikali watokane tena na kiongozi mkuu wa serikali? Si ajabu uwajibikaji Tz umekuwa kama hadithi.

Angalia mfumo wa bunge letu! Wabunge wa chama watokanao na wananchi, wakishafika bungeni, badala ya kuweka mbele maslahi ya nchi na kuwawakilisha wananchi wanaweka mbele zaidi matakwa ya viongozi wa chama! Ni vyema tukumbuke kuwa hata hizo kanuni za bunge anazotutisha nazo spika kama hazina maslahi na wananchi hazitufai. Kama bunge limeweka kanuni za kuziba vinywa wawakilishi wetu, tuna haki ya kuhoji uhalali wa kanuni hizo. Yote haya yatawezekana kama tukiungana kudai mabadiliko ya katiba, na tume huru ya uchaguzi, tume isiyotokana na raisi. Watz, tuamke, tuungane, tuikomboa nchi kwenye ukoloni mpya wa ndani. Aliyemfukuza mkoloni amegeuka kuwa mkoloni mwenyewe.
 
Mpaka lini tutaendelea kudanganywa kama watoto wadogo??? Eti tume ya uchaguzi inateuliwa na rais alafu tunaiita tume huru???? huu si usaniii???? tutadanganywa mpaka lini??? Nadhani kuna haja ya watanzania wote,,,si CCM, CHADEMA,,,CUF,,NCCR,,,TLP na vilivyobaki kuangalia hili kwa makini. Ushabiki wa kisiasa utatupeleka wapi kama tutabaki kuburuzwa kama vipofu waliovaa mawani ya mbao!! Hebu watanzania tuamke!! na nyie wabunge tunawaomba mlishupalie hili kwani hakuna haki wala uhuru wowote tunaoupata tukiendelea na mfumo huu wa tume ya taifa ya uchaguzi kuteuliwa na raisi
 

Ofcourse hata wanachama wa CCM wenyewe wanaliona hili kwasababu wanaofaidika na huu mfumo mbaya wa uchaguzi ni viongozi wa juu wachache na mafisadi. Inabidi sote kwa pamoja bila kujali itikadi zetu tusimame imara kudai katiba mpya itakayopelekea tume huru ya uchaguzi kwa manufaa ya wote na vizazi vijavyo!! Hii ni vita kubwa kati ya wale wanaoipenda na kuitakia mema nchi na mafisadi wachache wanaobebwa na CCM kama Rostam Aziz, Edward Lowassa, Jakaya Kikwete, Makamba and others!!
 



Tutaendelea kudanganywa mpaka siku tutakapojua tunadanganywa. Na wadanganyaji watakapojua tumejua wanatudanganya ndiyo wataacha kutudanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…