Tatizo la Tanzania ni uwajibikaji hata uunde nini kitafel.Jiulize hivi mamlaka zilizopo zimesaidia nini? Elimu na wenyewe wanataka mamlaka naona kila wizara sasa iunde mamlaka.
kwanza kabisa mimi naunga mkono ikiwa shughuli zote za serikali zitaundiwa mamlaka.
nikianza na mamlaka hii ya maendeleo tanzania. maendeleo yanakuja kwa kupanga.
serikali inaibuka na mikakati mingi tu ambayo inakwama kutokana na wanaopanga mipango hiyo hawaangalii mambo mengi katika jamii yetu kwa mapana.
mfano wakati inajengwa barabara ya kila wizara ya maji kupitia dawasa walikuwa wameweka bomba la maji kuelekea temeke, bomba la maji limeisha halijaanza kutumika wizara ya ujenzi ikataka kupanua barabara na kutoka katika pesa ya kujenga barabara hiyo wakalipa gharama za kuhamisha bomba kulisogeza pembeni.
serikali inafanya maboresho ya barabara nyingi za dar ili kuondoa msongamano na katika kufanya hivyo inabidi kuharibu barabara nyingine ambazo zilikuwa na uwezo wa kukaa miaka kumi ijayo kitendo ambacho ni kupoteza fedha.
kutokana na kutokuwepo kwa masta plan ya maendeleo ya taifa kila shughuli ya maendeleo tunayotaka kuifanya inakuwa ni ghali sana kutokana na miundo mbinu iliyopo haiingii katika mipango hiyo.
lakini kama tungekuwa na masta plan ya maendeleo ya taifa kila mradi unaotengenezwa ungekuwa kwanza unaingia katika masta plan hiyo hivyo mradi unaofuata sio kufuta uliotangulia na kuanza upya bali ni kuendeleza.
mfano mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi tulivutana juu ya kuvunja jengo la tanesco pale ubungo, barabara zote zilizokuwepo zimekwanguliwa ili kuweka mpya. hivi kama tungekuwa na masta plan tangu mwanzo inaonyesha kwanza eneo la barabara au usafirishaji kama tunampango wa kutumia treni katika barabara hiyo ni lipi na hivyo tangu masta plan imetolewa hairuhusiwi kufanya mwendelezo wowote katika majengo yaliyoko katika eneo hili. pili tunaangalia katika miaka 30 ijayo mfumo wa barabara utakuwaje ili kama ni kujenga sehemu fulani kwa sasa tunajenga sehemu moja na baada ya miaka kadhaa tunajenga sehemu ya pili kuongezea na sio kuharibu kilichokuwepo na kuanza upya. maji yanawekwa sehemu yake, umeme unawekwa sehemu yake.
kwa sasa nani apange haya? kila wizara inaangalia mambo yake. na ndio maana kunakuja umuhimu wa kuanzisha mamlaka hii kuziunganisha kazi zote zinazofanywa na wizara zote na hii ni kazi ya waziri mkuu hivyo mamlaka hii inatakiwa kuwa chini ya waziri mkuu.
mpango wa kwanza katika maendeleo ya mji ni kuapnga mji, nani aseme hili? waulize dawasa wanavyahangaika kutoa huduma za maji dar kutokana na mji kutokupangwa, waulize mawasiliano walivyoshindwa kuweka anwani za makazi kutokana na dar kujaa makazi holela, waulize wanaohusika na kurasimisha biashara walivyoshindwa kurasimisha biashara kutokana na biashara kukaa holela bila mpangilio, waulize tanesco wanavyosumbuliwa na makazi holela. ki msingi kila wizara utakayoigusa makazi holela yanawakwamisha.
wote wanakwama kwa tatizo hili lakini kutokana na kutokuwepo chombo kinachoangalia matatizo ya taifa kwa pamoja na kikapanga kuwa mfano ili kuiboresha dar ndani ya miaka 15 ijayo tutaanza na kupanga makazi na kutafuta mpango ambao utapanga makazi yetu kwa gharama ndogo si kufanya dili za kutengeza fedha kupitia miradi mikubwa. bali kuangalia jinsi serikali inaweza kuwawezesha wataalamu wa upimaji kwa kuwapa vifaa, wizara inatoa masta plan wao wanawapimia wananchi kwa kuwatoza ghara ndogo, kila kiwanja kinakuwa na barabara na kila uongozi wa mtaa unasimaia shughuli hii na kuweka utaratibu wa kwenda mpaka ngazi ya taifa kwa gharama ndogo sana. wizara itapata kodi za majengo baadae na wanaweza kuwa na miradi mikubwa ya kuweka sehemu za viwanda na huduma nyingine.
mpango unaelekeza baada ya kumaliza au wakati tukiendelea na mpango huu tunakuwa na mpango wa kuboresha usafiri wa umma tunaweka mikakati, tunaweka ubora wa makazi unaoruhusiwa maeneo fulani fulani, tunaweka mpango wa huduma za jamii.
hapa ni pale tunapozungumzia jiji au mji.
lakini ipo mipango ya kitaifa ambayo mkishafanya hizo skeletoni ni kazi ya mamlaka husika na wizara kujaza nyama ili kukamilisha na wakati huo mamlaka hii inapita kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa mipango ili kufanya maboresho.
lakini bila mipango kila mmoja anafanya anavyojua na akija mwingine anafuta kabisa ya mwenzake anafanya ya kwake hatuwezi kuendelea.
hivyo kuendesha shughuli za taifa kwa kutumia zaidi mamlaka na kupunguza ukubwa wa serikali ni jambo la msini sana na lina tija.
mfano huduma za jamii zote zinaweza kuundiwa kila hiduma mamlaka yake alafu zote zinawekwa katika wizara moja inayoitwa wizara ya huduma za jamii.
shughuli za maendeleo zote zinaweza kuwekwa katika wizara moja kila moja ilikundiwa mamlaka yake. huduma hizi zikiwa katika wizara moja kunakuwepo urahisi wa kuweka kipaumbele, wataalamu kushirikiana na kuona jamii inahitaji huduma gani kwa haraka na malengo ya sekta husika kusimamiwa na mamlaka inafanya mipango endelevu katika sekta na sio kupanga kwa kuangalia mda wa waziri kuwa kwenye uongozi. na mpango huu unaweza kuwaweka viongozi wa kisiasa katika sera zaidi na utendaji ukabaki kwa mamlaka.