GANG MO
JF-Expert Member
- Dec 6, 2016
- 2,089
- 2,198
Tunahitaji "strong media"kuzuia dharau na kebehi kwenye tasnia hii! Ndani ya mwaka mmoja waandishi wa habari wamekuwa wanakutana na kadhia ya kudharauliwa na baadhi ya viongozi hususani baadhi ya viongozi wa serikali.
Huko Arusha mwandishi wa habari wa ITV alikamatwa na kuwekwa ndani na mkuu wa wilaya kwa madai ya kuandika habari ambayo haikumpendezesha yeye,alimuweka ndani mwandishi,mamlaka zikakaa kimya,waandishi wakajibu na kukemea kirahisi rahisi tu.
Huko mkoani Pwani,mwandishi wa gazeti la mwananchi alipigishwa magoti na mkuu wa wilaya mbele ya hadhara,eti aombe radhi kwa kuandika habari ambayo haikumpendezesha mkuu wa wilaya,waandishi na vyombo vya habari vilikaa kimya,hatukupaza sauti.
Mkoani Kagera,wakati wa tukio la Tetemeko la Ardhi,mwandishi wa habari wa kituo cha ITV alikamatwa na mkuu wa Wilaya kwa madai ya kuripoti habari za baadhi ya wananchi huko Karagwe kukabiriwa na tatizo la uhaba wa chakula,hakuna chochote kilichofanyika!
Hivi karibuni tukasikia taarifa za mkuu mmoja wa Wilaya huko Arusha akisema hataki kuona waandishi wa habari wakiripoti habari za vikao vya madiwani ,akaenda mbali sana kwa kusema mwandishi atakayeenda kwenye vikao vya madiwani atakutana na virungu vya polisi.
Waandishi wamekuwa wanapigwa,wanan yanyaswa na kuoneakana kuwa watu wa hovyo hovyo,wananyimwa taarifa hata pale zinapokuwa na uharaka,kwenye chaguzi kumekuwa na matukio ya waandishi wa habari kufukuzwa kwenye misafara ya wagombea ubunge!.matukio haya yamekuwa yanaonekana masuala ya kawaida tu kwa waandishi wa habari!.
Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amevamia kituo cha TV cha Clouds na kulazimisha habari aliyokuwa amerekodi irushwe kwenye kipindi,mbaya zaidi akiwa na askari wenye silaha za moto,na kutaka habari yake iruke!.
Matukio haya dhidi ya waandishi na vyombo vya habari nchini Tanzania yanaonesha ni namna gani waandishi na vyombo vya habari tulivyo dhaifu,kila mtu anaweza kuviingilia vyombo vya habari na kufanya anavyotaka yeye! Vyombo vya habari vipunguze unyonge,waandishi walianza kufukuzwa field na viongozi,sasa wanaingiliwa mpaka studio na kuelekezwa nini cha kufanya!.
Unyonge huu sasa basi,inatosha sasa,tasnia ya habari iondoke kwenye unyonge.Waandishi wa habari tuungane kuondosha huu unyonge!.