Franco Zetta
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 1,661
- 843
Katika kipindi cha kwanza cha Uongozi wa awamu ya nne Mheshimiwa Rais Mstaafu J.K Kikwete alikuja na wazo zuri sana na akalitamka hadharani juu ya kuwepo siku maalum ambayo kila Mtanzania kwa Imani yake aweze kumshukuru Mungu kwa ajili ya Tanzania.
Binafsi niliamini pengine wazo hili Mheshimiwa atakuwa alilipata katika moja wapo ya ziara zake Marekani na akakutana na siku ambayo Wamarekani wanaiheshimu sana siku ya THANKS GIVING. Si jambo baya pamoja na Serikali kutokuwa na Dini ikawapa fursa raia kufanya vile kama zilivyo siku nyingine za ibada japo hili ni mara moja tu ndani ya Mwaka,lakini kwa bahati mbaya sana kiongozi wetu hakulikumbuka tena jema lile labda kwa kutingwa na majukumu ila kwa kupitia line yake binafsi nilimtumia ujumbe na ukamfikia akanijibu kuwa analikumbuka na kushukuru kwa kumtia moyo.
Baada ya ukimya nilimkumbusha tena mwanzoni mwa kipindi chake cha pili ila safari hiyo sikupata jibu. Nadhani sio vibaya kuiga jambo zuri na huo ni wivu mzuri, tukijua nchi yetu ilichezewa sana kwa makafara na matambiko ya mizimu na hata Mwalimu Nyerere alipata kukiri mambo haya kufanyika. Mambo haya bado yana nguvu ndani ya nchi na hata kwa vifo vya ndugu zetu walemavu wa ngozi wakati wa chaguzi inathibitisha hayo pamoja na mengine yanayomchukiza Mungu, na wala tusishangae neema yote tuliyonayo isitunufaishe kama nchi na kama Watanzania.
Ni Rai yangu kuwa Siku moja tu katika mwaka iwepo kwa ajili ya kumlilia Mungu na kuvunja LAANA zilizopo juu ya nchi na kuishia kumshukuru Mungu kila Mtanzania kwa imani yake,jambo hili nimelikumbuka hasa baada ya kusikia TAZARA inarejeshwa kwa Wachina waliotufadhili. Hiyo sio kawaida ni LAANA na ninapata shaka hata kwa hiyo sera ya viwanda kama itakuwa na Manufaa.
Naomba fikra pana zitumike kulifikiria jambo hili kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.Tanzania inaliwa na LAANA VINGINEVYO MUNGU AME TUPENDELEA SANA NA KUTUPA NEEMA KUBWA,TUOMBE TOBA NA KUMSHUKURU MUNGU KAMA TAIFA ni siku moja tu katika mwaka.