Nakusudia laana kwa maana ya LAANA hasa. Nini kimebaki ili tuzinduke na tuwe tayari kuleta mabadiliko ya fikra. Nchi imezongwa kwa miongo kama sita hivi toka kupata uhuru hadi leo.Viongozi wanatumia nguvu zaidi ili kupata mtandao wa kulindana na kulinda vyama visisambaratike lakini hawana habari na maslahi ya nchi. Ni mtandao ule ule ukishashika IKULU ghafla jitihada zinayeyuka. kwa nini hao wanaoitwa WAZEE wasikutane kumjadili RAIS na kuweka Msimamo wa kumtaka alinde maslahi ya nchi pale mambo na maamuzi yanapokuwa hovyo? wanakuwa wapi mijizee hii ? hawa wanatofauti gani na WANGA? wanaochamba mchana kweupe? MASKINI KIZAZI CHA TANZANIA, maskini wavuja jasho na mayatima, maskini walalahoi, maskini warandaji na mizigo iliyowapita kimo mnaotafuta mlo wa siku kwa udi na uvumba, MASKINI WATOTO WA TANZANIA. Aaah? Yaani mijitu inajisahau inacheza kumbwaya yenye MIDUNDO ILE ILE? Sad. Inauma sana.
Kwa Niaba ya watoto na walalahoi wa tanzania.
Cc
Mwenezi wa CC ya CCM,
Mzee Kinana,
Kambi zote za wanamatumaini na wakosa nia
UKAWA.
Kwa Niaba ya watoto na walalahoi wa tanzania.
Cc
Mwenezi wa CC ya CCM,
Mzee Kinana,
Kambi zote za wanamatumaini na wakosa nia
UKAWA.