Tunahitaji akina Muhongo wengi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, ndivyo tunavyolazimika kuanza kueleza msimamo wetu leo, kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Viongozi hawa wawili, hakuna asiyewafahamu kwa matokeo ya kazi zao, lakini pia hakuna asiyefahamu namna wanavyopigwa vita na wapinga maendeleo. Nani asiyefahamu umahiri wa Profesa Muhongo katika kuongoza sekta ya nishati nchini, katika kutetea Mradi wa Bomba la Gesi?

Leo tunashuhudia zaidi ya nusu ya nishati ya umeme tunayotumia, inatokana na rasilimali hii adimu. Hakuna asiyefahamu umahiri wa Profesa Muhongo katika usambazaji wa nishati ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) na hata hatua binafsi alizochukua za kushinikiza kupunguza bei ya kuunganisha umeme kwa Watanzania.

Hayo ni machache tu kutokana na nafasi, kwani amefanya mengi lakini kama ilivyo kawaida, alisakamwa, akahukumiwa na akachukua hatua ya kujiuzulu, akagombea jimboni na kurejeshwa bungeni, kitendo cha Rais John Magufuli kumrudisha Nishati na Madini tu, wapinga maendeleo wakaibuka walikojificha.

Lakini wapinge au wazungumze vinginevyo, Profesa Muhongo ni mchapakazi ambaye Watanzania wanahitaji wengi wa namna hiyo badala ya kuwa na huyo mmoja wa namna yake. Nani asiyemfahamu Makonda, kijana mdogo aliyekabidhiwa dhamana ya kumwakilisha Rais katika Wilaya ya Kinondoni na wapinga maendeleo wakaanza kumsakama?

Hakuna asiyefahamu kuwa ni Wilaya ya Kinondoni, ndiko ambako mgonjwa akipata ajali au akiumizwa, hatahitaji kwenda Polisi kupata Fomu namba tatu, bali akifika hospitali kuna dawati la Polisi, ambako atapatiwa fomu hiyo na kuingia kwa daktari.

Vijana wa Kinondoni karibu wote wanamfahamu, kwani alijitahidi kwa nguvu zote kushirikiana nao katika kutafuta na kutumia fursa, kwa nia ya kuongeza kipato chao. Ni huyo Makonda, aliyejitoa kusuluhisha mgogoro wa madereva na kuondoa kero kubwa iliyokuwa isambae nchi nzima kupitia mgomo uliokuwa umeandaliwa wa madereva wa daladala na wa mabasi ya mikoani, kama asingeingilia kati.

Ni juzi tu amebuni namna ya kusaidia walimu katika mkoa mzima wa Dar es Salaam, kupata usafiri wa bure wanapokwenda kusaidia vijana wetu kama ilivyo kwa watumishi wa majeshi, tena kwa kushawishi wamiliki wa daladala wakakubali, lakini wapinga maendeleo wakampinga.

Tumeeleza machache ya sifa zao, kwa sababu ya kuwatia moyo, ili waendelee kuchapa kazi, lakini pili kwa nia thabiti kabisa ya kuwavunja moyo wapinga maendeleo. Tunajua neno wapinga maendeleo linaweza kuonekana lina ukakasi, lakini tumelitumia kwa makusudi kwa kuwa baadhi ya wapinga maendeleo, wameingia mpaka katika vyombo vya habari na kupofusha macho ya kihabari katika kuona uchapakazi wa viongozi hawa.

Tunajua kuwa viongozi hawa si malaika, wanaweza kuwa na upungufu wa kibinadamu, lakini tunapaswa kuona matokeo na manufaa ya jitihada zao kwa Watanzania na kutazama Tanzania tunayoitaka, ambayo kwa hakika ili tufike huko tunahitaji akina Profesa Muhongo na Makonda wa kutosha na wapinga maendeleo wachache au wasiwepo kabisa.

Tunasisitiza kuwa tunaungana na Rais Magufuli katika kuwatia moyo viongozi hawa, lakini zaidi tunashawishika kuwakumbusha viongozi wengine kutazama mfano wa hawa na kujaribu kuwa akina Profesa Muhongo na Makonda katika maeneo yao ya uwajibikaji, ili tufikie lengo la kuwa na akina Profesa Muhongo na Makonda wa kutosha kutufikisha katika Tanzania tunayoitaka ya asali na maziwa.
 
Nilidhani ni mtu mmoja unaandika mawazo yako
ambayo kimsingi siyo mabaya,ila nimeshangazwa pale unapotumia wingi
yaani neno 'sisi" je ninyi ni akina nani?
 
Usione sifa kuanzisha uzi mara nyingi kwani zote unazobandika hapa ni upuuzi mtupu
 
Well said.........
 
Back
Top Bottom