tunaelekea kizazi kinachokuja kitakuwaje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tunaelekea kizazi kinachokuja kitakuwaje

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chauro, Dec 14, 2010.

 1. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  wanajamvi kuna jambo limekuwa likisumbua akili yangu muda wote hasa nikitizama watoto tuliozaa huwa nawaza mambo mengi sana.nakumbuka hapo nyuma tulipokuwa tunakua wengi watakuwa mashahidi kila mtu mzima alichukua jukumu la kulea mtoto wa mwenzake bila kuangalia ni wa nani leo hii ambapo muda mwingi hatupo majumbani ukikuta mwanao kachapwa na jirani au kakaripiwa unaanza kukuna mengine mengi naamini mtayaweka humu tusisahau hata kama utawalea kwa maadili gani watoto wako kama watazungukwa na uchafu kila mahali itakupa wakati mgumu sana kwenye malezi tupende watoto wa wenzetu na tuwatazame kwa jicho lile lile tunalowapa watoto wetu naamini tutatengeneza kizazi bora na sisi sio kuwa maangamizi wa malaika hawa wa malai
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Too late broda! Wazazi wa siku hizi hawataki hayo.
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmmhhh yaani ni kweli kabisa uliyosema hapo juu..
  lakini yanini ujitafutie balaa.. kwa kumgusa au kumkemea mtoto wa mtu...
  kwanza huyo mtoto atakutukana na mama akitoka huko ndani ndo yatakuishia shingoni....
  siku hizi ni kila mtu na chake...
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ndo maana Wazee wanatongoza mabinti (watoto) wa Wazee wenzake na kuwamega
  Hakuna aibu hata kidogo:A S-alert1:
   
 5. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  subhana llah,,,,,lakini nahisi yatakuwa yakitendeka hayo kwa ajili binaadam sasa hivi tumetokwa sana na imani wallah!!!!! ya rabb tunusuru sisi na unusuru vizazi vyetu ya allah???
   
 6. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Lakini tusisahau maisha yetu ya sasa muda mwingi tunakuwa mbali na familia tusipokubali watoto wetu waonywe na hawa tunawaachia tunajenga au kubomoa

   
 7. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  tumechelewa wapi kwa hiyo tumekubali kuwa na kizazi kibovu sababu tu hatutaki kukifanyia kazi

   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Ukitaka kesi gusa mtoto wa mtu sasa hivi uone kitakachokupata hata kumwambia wee acha kuchezea mchanga au maji machafu ni issue utavaliwa kibwebwe na mama yake mpaka utashangaa
   
 9. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  jamani Dena ndo hicho nachosikitika unajua hata mimi na watoto unapokuta mzazi mpaka mwalimu wa mtoto hutaki amkemee mwanao tunategemea nini kutoka kwa watoto hawa

   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Tena Chauro huko shuleni mie nilishangaa sana siku moja nilikwenda kulipa ada ya mtoto wangu nikakuta mtoto kachapwa sijui alifanya kosa gani sikuuliza lakini huyo mzazi alivyokuwa anaongea laahhhh nilishindwa hata sijui alikuwaje maana anaonekana mtu na heshima zake lakini maneno aliyokuwa anatoa mie hoi nasikia baadae alimhamisha mwanae shule ile kampeleka St....... badala ya ile nyingine usimguse kabisa mtoto wa mtu kipindi hiki ni kujitafutia matatizo
   
 11. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mi sijui lakini mimi nalitazama kama tatizo kubwa sana kwenye familia zetu maana malezi yamekuwa magumu kuliko tutahangaika sana kutafuta pesa na mali nyingi lakini kama tutakuwa na familia mbovu ni kazi bure na yote kwangu nahesabu kama ni ubatili mtupu upewe mali na amani mali bila amani ni kifo
   
 12. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #12
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Kuwa mpole tu mwanakwetu hiyo ndo dunia ya tekinolojia ilivyo kwa sasa
   
 13. F

  Ferds JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  "AN INDIVIDUAL IS THE BEST JUDGE OF HIS OWN INTEREST"( GEREMY BENTHAM) haya mambo ya kumparamia mtoto wa watu na kumkanya jamani kwa dunia ya leo ambapo maisha na utaratibu wa mtu kuishi yeye na kizazi chake ni mali yake binafsi hauwezekani.
  Enzi za zamani wajibu (responsibility) wa mtu ndio uliokuwa unatawala kuliko haki ya mtu mwingine, na ndio maana jirani kukanya mtoto wa mwenzie alijua kuwa anatimiza wajibu wake kama mzazi na mtoto hakuwa na naki ya kuibishia adhabu hiyo, leo neno haki(right) limepiku wajibu, kumbuka leo hii suala la kumuadhib mtoto ni haki ya mzazi wake, wewe ni kuripoti tu juu ya kosa la mtoto kwa mzazi husika, huna haki japo unalimited responsibility juu ya mtoto wa mwenzio, sasa tunaishi kiubinafsi zaid(individualism) tumeyakubali mawazo ya Bentham na ndiyo yanatukeketa
   
 14. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nafikiri hujanielewa sio lazima kumuadhibu huyu mtoto hata mtu mzima anapotoa report kwako kama mzazi huwa tunarespond vip hata hawa walimu basi tunaokabidhi watoto wetu nao waogope kuwakanya sababu ya utandawazi unaongelea tena kuparamia ivi kweli kumkanya mtoto ni kumparamia sisi ni wazazi wa aina gani ndo maana sishangai pale tunaposhabikia mambo yanayobomoa badala ya kujenga


   
 15. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nimeweka tu watu tujadili kuna mambo tunapuuzia lakini kwakweli yatatumiza sisi wenyewe sijui kwanini tunafumbia macho mambo ya msingi kabisa


   
 16. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #16
  Dec 15, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  chauro bibie nakubaliana nawe watoto wanahitaji maadili kutoka kwa watu mbali mbali lakini mmmhhhh
  we watu wazima wenyewe hawana heshimma kabisa sasa hivi..
  ndo maana nikasema kila mtu na chake wazazi ndo wanaotakiwa kumfundisha mwanao maadili mema..
  sanasana na familly members pamoja na walimu.... Dunia hii imesha badilika Chauro huwezi kumuani kila mtu..

  na kingine labda we unapoishi ni sehemu yenye amani na ambapo watu bado wana maadili na heshima ......
  ningependa kusema kama ungekuwa unaishi ninapoishi huku ndo story nyingine kabisa....
  mtoto anakula darasani halafu akimaliza analala kwenye dawati ....
  mwalimu akimwamsha ni balaa tupu..iliwahi kutokea mbele ya macho yangu...

  Hii dunia ya sasa imeguaka 360 degrees .....

  AD
   
 17. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ni mambo ya kukumbushana na kila mtu atekeleze wajibu wake kama mzazi,maana sikuu ya hesabu kila mtu atawasilisha mahesabu yake.
   
Loading...