Tuna siku tatu hatuna Umeme Kigamboni

Tuna siku tatu hatuna Umeme Kigamboni

mizambwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2008
Posts
4,421
Reaction score
1,792
Katika Jiji la DSM kuna kisiwa maarufu sana ambacho hata Serikali imefikiria kujenga mi mpya. Ni huko Kigamboni.

kwa siku ya tatu leo hakuna Umeme; mji huu mpya unategemea maji kutoka katika visima virefu (Hakuna maji ya kutoka RUVU) ambavyo lazima Pump itumike kuvuta maji.

Hivyo kutokana na ukosefu wa umeme siku ya tatu na haijulikani itaisha lini imekuwa ni kero kwa wakazi wa mji huo mpya.

hakuna Umeme, hakuna maji.....Siku ya tatu Giza, no kuoga, no kufua, vyoo vinanuka na hakuna mawasiliano ya simu kwani zimezima charge.

Jamani TANESCO FANYENI JUHUDI KUWARUDISHIA HUDUMA YA UMEME

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
mmekariri kuwa nuru mjini na giza ni huko bush. mambo yamegeuka shamba sisi umeme upo. zamu yenu kuonja maisha ya mwaka 47.
 
Ni kweli kuna tatizo la umeme kwa maeneo yote ya Kigamboni, Mbagala, Mkuranga na sehemu za Temeke. Kutokana na mvua za juzi usiku, nguzo zaidi ya 15 na nyaya zilikatika.
Hadi saa kumi na moja jioni nguzo zote zilikuwa zimesimikwa na sasa kazi ya kurejesha nyaya inaendelea.
Umeme unatarajia kurudi kwenye saa sita usiku iwapo hakutakuwa na mvua kubwa inanyesha.
Nitawapeni mrejesho kadri ninavyoupata toka kwa uongozi wa Tanesco. Poleni kwa usumbufu.

Asanteni.
Dkt Faustine Ndugulile-Mbunge Kigamboni
 
Angalau tumejua tatizo mheshimiwa,hivi hawa tanesco kwa nini hawatoi taarifa kutujulisha wateja kama kuna tatizo,wabadilike tanesco
 
Ni kweli kuna tatizo la umeme kwa maeneo yote ya Kigamboni, Mbagala, Mkuranga na sehemu za Temeke. Kutokana na mvua za juzi usiku, nguzo zaidi ya 15 na nyaya zilikatika.
Hadi saa kumi na moja jioni nguzo zote zilikuwa zimesimikwa na sasa kazi ya kurejesha nyaya inaendelea.
Umeme unatarajia kurudi kwenye saa sita usiku iwapo hakutakuwa na mvua kubwa inanyesha.
Nitawapeni mrejesho kadri ninavyoupata toka kwa uongozi wa Tanesco. Poleni kwa usumbufu.

Asanteni.
Dkt Faustine Ndugulile-Mbunge Kigamboni
Nguzo zaidi ya kumi na tano ni ngapi??
15.5?
15.75?
Au?
Au hata tanesxo hawana idadi kamili?

Halafu mbona kuna tatizo la mara kwa mara la umeme huko?
Hapa naiongelea kijichi ambayo ipo jimboni kwako nayo inasababishwa na nini?
 
Umeme na maji nchi hii vimeshakua kero isiyotatuliika! Hivi kwanini wasiruhusu wawekezaji? Maana hii ndo nji pekee ya kuongeza ufanisi kama ilivyo sasa kwenye mitandao ya simu.
 
Nguzo zaidi ya kumi na tano ni ngapi??
15.5?
15.75?
Au?
Au hata tanesxo hawana idadi kamili?

Halafu mbona kuna tatizo la mara kwa mara la umeme huko?
Hapa naiongelea kijichi ambayo ipo jimboni kwako nayo inasababishwa na nini?
Kijichi ni sehemu ya Tarafa ya Mbagala. Nayo inahusika na tatizo hili la sasa. Kuhusu umeme kuwa mdogo na kukatika mara kwa mara, baadhi ya maeneo ya Kijichi yana "low voltage", kuna mpango wa kufanya "voltage improvement".
 
Mpango huo utakamilika lini?
Maana najua tatizo la kukatika umeme mara kwa mara umelikuta, au tanesco bado wapo kwenye mchakato?

Kuna haja kubwa ya kuangalia tanesco (na utumishi wa umma) kwa jicho la tatu
 
Hongera mbunge kwa taarifa ya haraka fuatilia umeme urudi mapema iwezekanavyo
 
Leo nimetembelea baazi ya ndugu jamaa na marafiki huko kigamboni. Kwa kweli nyumba nyingi zinanuka kama mabanda ya kuku. Kama hali hii itaendelea mpaka kesho, waume na wake zao watatengana vitanda.
 
Leo nimetembelea baazi ya ndugu jamaa na marafiki huko kigamboni. Kwa kweli nyumba nyingi zinanuka kama mabanda ya kuku. Kama hali hii itaendelea mpaka kesho, waume na wake zao watatengana vitanda.

kwamtoro acha maskhara
Na hapo nguzo takribani 15 ( inawezekana hawana hakika) imechukua karibia 48hrs

Sasa ingekua nguzo 30 wangekaa giza mieZi 6!!!

Achana na tanesco wewe

Nawashauri wakaI wa temeke kuomba hifadhi kwa ndugu angalau waoge kupinguza harufu
 
Last edited by a moderator:
Kijichi ni sehemu ya Tarafa ya Mbagala. Nayo inahusika na tatizo hili la sasa. Kuhusu umeme kuwa mdogo na kukatika mara kwa mara, baadhi ya maeneo ya Kijichi yana "low voltage", kuna mpango wa kufanya "voltage improvement".

Mkuu hii ni kujumuisha na baadhi ya maeneo ya kinondoni ama maana na huku umeme ulikatika hiyo hiyo mida
 
Kijichi ni sehemu ya Tarafa ya Mbagala. Nayo inahusika na tatizo hili la sasa. Kuhusu umeme kuwa mdogo na kukatika mara kwa mara, baadhi ya maeneo ya Kijichi yana "low voltage", kuna mpango wa kufanya "voltage improvement".

aisee kijichi kunatakiwa jitahada za haraka sana ni kero kubwa sana kwa kweli.
 
Tunashukuru Mh.Mbunge kwa,taarifa.me siwezi lala,mpaka,hiyo saa Sita na na ona hali ya hewa badi ni shwari.
 
MH.Mbunge mbona mpaka sasa hamna kitu na usiku wa jana mvua haikunyesha...kulikoni?
 
MH.Mbunge mbona mpaka sasa hamna kitu na usiku wa jana mvua haikunyesha...kulikoni?
Mmbunge inawezekana aliambiwa hivyo,ila hao tanesco gari ya kubebea nguzo pengne mafuta imeisha wanasubili mjipendekeze wawatoboe ndio waje faster,utafikir wao wanatoaga unity za bure.
 
Back
Top Bottom