pakamwam
JF-Expert Member
- May 28, 2013
- 516
- 656
Ninaanza mjadala huu
Kwa kuiangazia marekani. Sababu inayoifanya marekani iwe nchi thabiti kijeshi ni kwamba, hawa jamaa wamepigana vita nyingi. Katika hizo vita waligundua mbinu na vifaa mbali mbali vya kivita. Pia hata internet ninayotumia kuwasiliana na nyie ni jeshi la marekani liligundua kama njia ya kurahisisha mawasiliano vitani. Leo hii kiteknolojia ya vita hakuna taifa linalonfikia marekani. Wakati wengine wanahangaika na nuclear fission(atomic bomb) na nuclear fussion(hydrogen bomb) yeye amepata mother of all bombs ambayo sio nyuklia. Wakati wengine wanahangaika kutengeza makombola ambayo yeye alitumia enzi hizo, yeye anahangaika na teknolojia ya kuzuia makombora hayo. Wanatumia elimu yao kutatua changamoto zao. Wasomi wao wako busy kusaidia jamii yao.
Mjadala wangu unajikita kwenye elimu na matumizi ya elimu yetu.
Tunasoma kweli lakini nini maaana ya elimu yetu. Ninavyojua elimu ina maana pale inapotusaidia kutatua changamoto zetu na za jamii. Hizi ni magonjwa, ujinga, umasikini na nishati endelevu na mengine mengi
Ipo mifano dhahili ya watu waliotuma elimu yao kwa manufaa ya jamii na wenyewe pia. Lakini asilimia kubwa ya watu wengi tumekuwa ni somasoma tupate degree nyingi tukatishie watu. Nndio maana maprofesa wengine baadala ya kuwafunza vijana na kuibua vipaji vyao wanabaki kuwatisha na kuwakatisha tamaa eti huwezi kuwa kama mimi( who are you, God au)
Kama napata elimu hata maisha yangu siyamudu hiyo elimu ina maana gani. Elimu inatakiwa kubadilisha maisha yangu, familia yangu, jamii yangu, taifa na dunia. Elimu haitakiwa kuwa silaha ya kuibia na kunyanyasia wananchi
Nimeona baadhi ya wasomi walivyotumia elimu ya kuwaibia wanyonge, masikini na hata jamii yao. Najiuliza kuwa kama kweli tuna wasomi au majizi. Elimu kuu ni ile inayotatua matatizo ya jamii husika. Ndio maana watu wetu wako rahisi kuamini waongo na matapeli na hata imani fulani,.kumbuka kikombe cha babu, sisi tunaotakiwa kusema tumelala.usingizi mzito au hatujabuni njia mahususi za kusaidia jamii zetu kwa.mazingira tuliyonayo
Wapo vijana wakisoma wanakuwa malaika na kuanza kukataa hata kazi zingine. Kupata degree nyingi au uprofesa usioleta majibu kwenye matatizo au changamoto za kijamii na mbaya zaidi kushiñdwa kumudu maisha binafsi ni kujitàabisha na kujichelewa. Kumbuka wote tutakufa, ingawa wanaosaidia jamii wataishi mioyoni mwa jamii kama dorkasi na lissu.
Tusome na elimu yetu ilete manufaa kwa jamii. Kumbuka kusoma hakukufanyi uwe binadamu kuliko wengine, tumia elimu yako kutatua changamoto za jamii. Elimu isigeuke silaha ya kuadhibia jamii yetu.
Tulete majibu kwa jamii baadala ya kujaa rushwa na ubinafsi na majivuno. Ndio maana timesoma tunazeekea nyumba za kupanga. Mtu mwenye degree tatu kaachishwa kazi analalamika ataishije, kumbuka mkuu wa mkoa fulani, nashukuru rais hakumrudisha maana hawezi kuleta majibu huyo katika matatizo ya jamii yetu
Tujifunze kwa akina newton, faraday, albert eistein, tundu antipas lissu, julius kambarage nyerere na watanzania wengine wazalendo kama edward moringe sokoine.
Msomi anatengeneza vyeti feki hadi vya madaktari na wanasayansi maabara afya. Huyu mtu si anaua jamii nzima.