KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,150
Nyimbo za Madilu nazopenda (sana):
- Pie Mboyo
- Biya
- Apula
- Autoroute
- Fanta Cebene
Pumzika Giant Madilu.
lazamwa ni ukimwi kweli? Unajua hata Francoo alipokufa inasemekana ni huo huo ukimwi, yana ukweli haya?Madilu hakuna cha kuanguka wala nini. Ilikuwa ukimwi tu ndo uliomuua. Omar bongo na mkewe huo huo. Walikuwa womanisers saana hawa jamaa. Full stop
Umesahau pesa positionumesahau yajean..
Kwenye huo wimbo mimi Napenda jinsi Solo gitaa lilivyovutwa nyuzi.Wimbo wake wa Ya Jean ndo wimbo mkali zaidi.
Ya Jean!Nyimbo za Madilu nazopenda (sana):
- Pie Mboyo
- Biya
- Apula
- Autoroute
- Fanta Cebene
Pumzika Giant Madilu.
Kwenye huo wimbo mimi Napenda jinsi Solo gitaa lilivyovutwa nyuzi.
Nyimbo iliyomtoa Madilu kwenye uimbaji ni "Non" 1983 Utunzi wa Franco wakiimba duet na Madilu. Hii ndiyo nyimbo ya kwanza toka kuingia OK Jazz 1980 alisikika na kuimba solo. Hizo nyingine zilifuata nyingi zikiwa utunzi wa Franco kama Mamou.Akiwa na mzee Franco na TP OK JAZZ nyimbo ambayo ilimtoa madilu ilikua ni "Mamou" ambayo ilikuja kuwa nyimbo bora kwa mwaka 1984
Kiongozi wa TP OK Jazz baada ya kufariki Franco alikuwa Le Poete Simaro Lutumba mpaka kuvunjika kwa bendi 1993 na baada ya hapo walianzisha Bana OK 1994 na Madilu ndio akaenda solo hadi umauti ulipomfika. Kwa utaratibu alijenga bendi yake "Multi-System" ambayoilikuja kufanya vizuri bahati mbaya ndio umauti ukamfika 2007.lakini baadae TP OK JAZZ Ikarudi upya chini ya Madilu
Le Grand Maitre Franco hakuwa na undugu wowote na Madilu Sytem.Hata hivyo nina swali, inasemekana kua Franco Lwambo Lwanzo Makyadi mpiga solo namba moja duniani alikua na uhusiano wa damu na Madiluu, kwamba eti Madiluu na Francoo walikua ni mtu na mjomba-ake, kuna ukweli kuhusu hili?
Sidhani kama kuna mtu anaweza kuwa mrithi wa Franco. Kuna ambao wameendeleza mziki wa Franco wakiwamo Madilu na Youlou (hawa wamesema hadharani na kuonyesha kimuziki kuwa ni watoto wa Franco kimuziki). Kuna bendi za Bana OK (Kinshasa), Bana OK International, na wengine. Kumbuka Franco alikuwa kiongozi, mpiga solo, muimbaji, talent hunter aliyeongoza bendi kubwa zilizowahi kutokea Congo. Hivyo viatu vyake ni vigumu kuvaliwa na mtu mwingine. Mtu ambaye alimkaribia Franco ndani na nje ya OK jazz ni kiongozi wa OK Jazz na Bana OK-Simaro Lutumba -familia ya Franco ilipo msimamisha huyu kuwa kiongozi wa OK Jazz wanamuziki karibu wote waliacha OK Jazz na wengi wakaanzisha Bana OK na baadae Bana OK International (Odemba International). Kwa wapenzi wa Madilu watakumbuka kitu kama Ofela, Dati petrol mtunzi wake alikuwa Mzee Lutumba (miaka 79 sasa na bado yuko active kiasi). Huwezi pia kumsahau Commander Josky Kiambukuta huyu ni sauti ya OK Jazz na mtunzi mahiri sana (1973-1993) nae bado anatoa moja moja.Madilu alikuwa ni noma baada ya kifo cha Franco wataalamu wa muziki wa Congo walisema yeye ndo alikuwa mrithi wake.