Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,560
Nilikwenda nyumbani kwa RDD (Siku hizi cheo hicho kinaitwa RAS) mmoja miaka ya tisini mwanzoni kumsalimia. Wakati nipo pale nikashikwa na haja, basi nikaonyeshwa msalani. Basi ile kuingia tu nikakutana na ndoo kubwa ya maji ipo kwa pembeni. Nikajiuliza ni ya nini? kumbe mpira wa kupeleka maji kwenye tenki la choo kile umekatika, kwa hivyo ukitaka kuflashi ni lazima ubebe ndoo na kumwaga maji kwenye tenki lile. Choo cha kisasa kinaendeshwa kizamani!!
Nikiangalia kwa jinsi siasa za nchi yetu huwa najiuliza haya mambo ya kuwaiga wazungu kwenye kuendesha nchi zetu wakati matendo yetu hayasawiri tabia za mifumo hiyo faida yake iko wapi? Ni katika Afrika ambapo kwenye uchaguzi watu wanakatwa mapanga na baada ya uchaguzi hakuna mtu anayejali kama kuna watu wamepoteza maisha kutokana na siasa. Kwa sababu Afrika siasa ni kazi kama zilivyo kazi zinginewe na wakati wa uchagauzi ni wakati wakupigani ajira. Atakaye kufa afe na atakayepona apone mradi malengo ya kushinda yafikiwe.
Ni bara hili pekee ambapo ukiwa na madaraka kuyapoteza ni dhambi. watu wakifa, wakiwa vilema au wakiwa ni wakimbizi wa ndani na nje ya nchi hilo si tatizo. Ni katika Afrika ambapo kuna kuwa na hela za kuendeshea anasa za viongozi wakati wananchi wanakufa kwa njaa.
Afrika ni sehemu pekee haijulikani mipaka ya kiuongozi, Kiongozi "Mkuu" ndiye anakuwa dira ya maisha ya kila siku ya taifa husika, hakuna mgawanyo wa kimadaraka bali mgawanyo huo uko kinadharia tu. Nchi ni Kiongozi Mkuu na Kiongozi Mkuu ndiye nchi.
Kama hatutaki kutumia ipasavyo mifumo tuliyoiga toka kwa wazungu,kwa nini tusimie mifumo yetu ya zamani ambapo Uchifu na Usultani ulitamalaki barani Afrika? Tuwe na Baraza la wazee la kumshauri Kiongozi Mkuu, basi!!