Baada ya maadui wote kuisha na bila kupata ufumbuzi wa matatizo yetu sasa hivi tumepata adui mwingine mpya naye ni Kiswahili, sasa hivi Watanzania hawakitaki kiswahili wanasema ndio kinatafanya tuwe maskini!
Tulianzia mbali sana, alikuwa Mwarabu katuuza utumwa na kumaliza nguvu kazi zetu ndio maana tulishindwa kuendelea, akaja Mzungu tukasema Ukoloni ulituibia rasilimali zetu na kutubagua kwa kutunyina haki na fursa ndio maana hatukuendelea, tukaja Ujamaa, ulituangusha sana na kutupumbaza na kutufanya wavivu ndio maana hatukuendelea, na sasa hivi hatimaye tumepata adui mwingine baada ya wote hao waliopita naye ni Kiswahili, sasa tunasema hatujui kiingereza ndio maana tunashindwa kuendelea, hatujui kiingereza ndio maana tunauza Rasilimali zetu, tunasema kiswahili ndio adui yetu, ni mpaka hapo tutakapo mtoa ndio tunaweza kuendelea!
Na baada ya kuharibu na kumaliza kila kitu kilichokuwepo kuanzia reli, barabara, mipango miji, Elimu, sasa tunataka kuhamishia majeshi kwenye adui yetu pekee aliyebaki anayeonekana kutukwamisha naye ni Kiswahili, nafikiri na tunaamini tukishamaliza huyo ndio tunaweza kuendelea, sina uhakika hii vita itatufikisha wapi katika kupambana na huyu adui yetu mpya bna pekee aliyebaki mbele yetu, lakini vyovyote vile itakavyokuwa mwisho wa siku nafikiri Michael Jackson aliona mbali sana ingawaje lazima nikubali kwamba hapo zamani sikuelewa mtu anawezaje kufikia uamuzi kama huo wa kujibadilisha kabisa na kuonekana vingine na uasilia wake na sasa nimemuelewa, Mungu akulaze mahali pema peponi MJ!