Tumenunua TV, hatuna chakula, nyumba haina umeme

Mtazamo wa kuajiriwa siyo mzuri. Serikali itaajiri wangapi weweeeee???! Umegonga shule bado unalialia kuajiriwa na serikali, kweeeli???!
-Hapa umeteleza ndugu,serikali yeyote nailiyo makini duniani inahusika pakubwa kwa kuwa na ukosefu wa ajira au wingi wa ajira katika nchi,
-Serikali inatakiwa itoe ajira yenyewe,pia itoe fursa kwa wawekezaji ili wawekezaji watoe ajira kwa raia,

-halafu usimlazimishe kila mtu atake kujiajiri kama wewe serikali umeshindwa kumpa mtu ajira,
hata kama mtu kasoma kuna taaluma nyingine mtu huwezi kujiajiri,hata USA, EU ,RUSSIA, ISRAEL,JAPAN CHINA etc kuna taaluma mtu lazima AAJILIWE.

-pia usizuie ndoto za raia kutafuta kuajiliwa,mfano mtu amesomea masuala ya anga,nyukilia,au mtu ana ndoto za kutaka kuwa mwanajeshi ,polisi,askari wanyama pori,magereza uhamiaji,utafiti, mambo ya mionzi atajiajiri vipi? usimlazimishe mtu kuanzashala duka la kuuza vyakula badala ya kazi aliyoisomea kwa sababu ya wewe kutotengeneza ajira,kuna ajira nyingine zinapatiakana serikalini tu kama nilivyotoa mifano hapo juu,na kuna mtu anatamani maisha yake yote aje kuajiriwa serikalini,wewe unamlazimisha ajiajiri,uko sawa wewe?

-sio kila mtu anatamani kufanya biashara,ndio maana biashara nyingi za Watanzania zinakufa mapema ,kwa sababu watu hawana wito ni kwa sababu ya kulazimishwa na maamuzi ya mijitu kama wewe,

-wenzetu wameendelea Wazungu,waasia na waaajemi wanawasaidia vijana wao kutimiza ndoto zao,ndio maana wana maendeleo, wewe leo unawahimiza watu wakafanye biashara ya kuuza mahindi nje ya ndoto zao,kutoka mikoa ya kusini wakati kijana alisomea mambo ya mionzi ,uko sawa wewe,
Halafu unakuta wewe ni msomi kabisa tena waziri mshauri wa Mkuu.

-Kila mtu hapa duniani huja na matamanio na kutosha kwenye kitu anachokiweza ,mimi nimesomea sayansi fulani wewe unanilazimisha nifanye biashara.

-Sisi Watanzania kama sio Waafrika sijui nani katuloga.
-NDIO MAANA NCHI HAIENDELEI KWA SABABU YA MAWAZO FINYU KAMA YAKO,YA KUWATOA VIJANA KATIKA NDOTO ZAO.
 
Tumenunua mindege mingi, mingine mikubwa na mingine ya kadiri na mingine midogo.

Manunuzi haya hayana tija kwa taifa letu, yanatutia umasikini zaidi. Watumiaji wa ndege hawazidi 2% hata viwanja vyenyewe hatuna vya kutosha.

Mikoa ya kaskazini hakupitiki, madaraja na barabara zimekatika. Watanzania hatuhitaji ndege, tunahitaji kuboreshewa miundombinu. Tunahitaji lishe bora, elimu safi kama inayotolewa kwenye shule mnakopeleka watoto wenu. Tunahitaji maji safi na salama na pia tunahitaji huduma bora za afya.

Magufuli amezunguka vijiji vingi kuanzia Songwe, Rukwa, Katavi, Lindi, Mtwara etc hamna sehemu hata moja ambapo wananchi walimwambia tunahitaji ndege.

Sasa kama yeye ni Rais wa WANYONGE, si asikilize kilio chetu badala ya kufanya mambo anayoshauriwa na Kagame?

Magufuli tunakuombea mema ndio maana tunakukosoa licha ya kwamba hupendi kukosolewa.

Dreamliner ya kwanza ipo tuuuuu imelala ndani haijapaa kwenda kokote licha ya kwamba mlituhadaa kwamba itaanza kwenda India na China.

Hiyo haiingizi pesa yoyote bado mnaleta dreamliner nyingine. Hizi assets zinaharibika, mbaya zaidi zinaharibika huku haziingizi kitu.

Jana umesema tumepata USD 14mil. Tunaomba CAG report ambayo ameikagua ATCL. Tunajua ATCL ni miongoni mwa asasi ambazo hutaki zikaguliwe kwa kuficha aibu.

Sasa tunaomba uache kutuhadaa kuwa ATCL inajiendesha kwa faida.
Pascal Mayalla, usikasirike, najua wasukuma mmeshikamana ili kuteteana hata kwenye ujinga.
Aliye anza kununua ndege ni Nyerere na shirika aliliunda yeye, hapo kabla Kenyata, Obote na Nyerere walikuwa na shirika la ndege la pamoja (EAA)!
 
Mawazo ya kifisimaji haya, nani kasema kuna amani??
Mkuu inabidi ubadilishe mtazamo wako, kwenye business tunaangalia faida. Kama biashara haina faida mfanyabiashara ataachana nayo, na kama ina faida mfanyabiashara ataongeza mtaji pamoja na kuitanua biashara kwa mapana zaidi.

Na ndio maendeleo yanavyokuja, baada ya muda tutakuwa tumefika mbali sana kutokana na hatua moja baada ya hatua nyingine.

Kama ukiwa huna, na kuamini kwamba huna, basi utaendelea kuwa huna.
-Tushukuru Mungu tumenunua Tv
-Umeme UPO wa kutosha kuwasha Tv tofauti na awamu zilizopita (hata mgao wa umeme imekuwa historia"
just open your mind umeme upo mkuu
-Chakula KIPO mkuu, hatujasikia njaa muda mrefu, tumshukuru Mungu kwa kutulinda na janga la njaa
-Nyumba IPO Mungu ametubariki, nyumba ina amani na utulivu unapatikana nyumbani
 
Mimi huwa namshangaa sana mtu anayeamini kuwa anaupeo finyu sana mpaka kuamini jiwe anaweza kumwongoza
Propaganda za maccm zingesaidiwa na strong propaganda za upinzani kwa mtindo wa kukosoa ili kuziboresha....

tatizo propaganda za upinzani zinakuja kwa mtindo wa taarabu, uzushi na majungu.
 
Ukiwa na mawazo kama haya ipo siku utasema tusifanye uchaguzi mkuu vile uchaguzi una gharama na watu hawaoni shida CCM kuongoza milele...
 
Umenena vyema mkuu
-Hapa umeteleza ndugu,serikali yeyote nailiyo makini duniani inahusika pakubwa kwa kuwa na ukosefu wa ajira au wingi wa ajira katika nchi,
-Serikali inatakiwa itoe ajira yenyewe,pia itoe fursa kwa wawekezaji ili wawekezaji watoe ajira kwa raia,

-halafu usimlazimishe kila mtu atake kujiajiri kama wewe serikali umeshindwa kumpa mtu ajira,
hata kama mtu kasoma kuna taaluma nyingine mtu huwezi kujiajiri,hata USA, EU ,RUSSIA, ISRAEL,JAPAN CHINA etc kuna taaluma mtu lazima AAJILIWE.

-pia usizuie ndoto za raia kutafuta kuajiliwa,mfano mtu amesomea masuala ya anga,nyukilia,au mtu ana ndoto za kutaka kuwa mwanajeshi ,polisi,askari wanyama pori,magereza uhamiaji,utafiti, mambo ya mionzi atajiajiri vipi? usimlazimishe mtu kuanzashala duka la kuuza vyakula badala ya kazi aliyoisomea kwa sababu ya wewe kutotengeneza ajira,kuna ajira nyingine zinapatiakana serikalini tu kama nilivyotoa mifano hapo juu,na kuna mtu anatamani maisha yake yote aje kuajiriwa serikalini,wewe unamlazimisha ajiajiri,uko sawa wewe?

-sio kila mtu anatamani kufanya biashara,ndio maana biashara nyingi za Watanzania zinakufa mapema ,kwa sababu watu hawana wito ni kwa sababu ya kulazimishwa na maamuzi ya mijitu kama wewe,

-wenzetu wameendelea Wazungu,waasia na waaajemi wanawasaidia vijana wao kutimiza ndoto zao,ndio maana wana maendeleo, wewe leo unawahimiza watu wakafanye biashara ya kuuza mahindi nje ya ndoto zao,kutoka mikoa ya kusini wakati kijana alisomea mambo ya mionzi ,uko sawa wewe,
Halafu unakuta wewe ni msomi kabisa tena waziri mshauri wa Mkuu.

-Kila mtu hapa duniani huja na matamanio na kutosha kwenye kitu anachokiweza ,mimi nimesomea sayansi fulani wewe unanilazimisha nifanye biashara.

-Sisi Watanzania kama sio Waafrika sijui nani katuloga.
-NDIO MAANA NCHI HAIENDELEI KWA SABABU YA MAWAZO FINYU KAMA YAKO,YA KUWATOA VIJANA KATIKA NDOTO ZAO.
 
Tumenunua mindege mingi, mingine mikubwa na mingine ya kadiri na mingine midogo.

Manunuzi haya hayana tija kwa taifa letu, yanatutia umasikini zaidi. Watumiaji wa ndege hawazidi 2% hata viwanja vyenyewe hatuna vya kutosha.

Mikoa ya kaskazini hakupitiki, madaraja na barabara zimekatika. Watanzania hatuhitaji ndege, tunahitaji kuboreshewa miundombinu. Tunahitaji lishe bora, elimu safi kama inayotolewa kwenye shule mnakopeleka watoto wenu. Tunahitaji maji safi na salama na pia tunahitaji huduma bora za afya.

Magufuli amezunguka vijiji vingi kuanzia Songwe, Rukwa, Katavi, Lindi, Mtwara etc hamna sehemu hata moja ambapo wananchi walimwambia tunahitaji ndege.

Sasa kama yeye ni Rais wa WANYONGE, si asikilize kilio chetu badala ya kufanya mambo anayoshauriwa na Kagame?

Magufuli tunakuombea mema ndio maana tunakukosoa licha ya kwamba hupendi kukosolewa.

Dreamliner ya kwanza ipo tuuuuu imelala ndani haijapaa kwenda kokote licha ya kwamba mlituhadaa kwamba itaanza kwenda India na China.

Hiyo haiingizi pesa yoyote bado mnaleta dreamliner nyingine. Hizi assets zinaharibika, mbaya zaidi zinaharibika huku haziingizi kitu.

Jana umesema tumepata USD 14mil. Tunaomba CAG report ambayo ameikagua ATCL. Tunajua ATCL ni miongoni mwa asasi ambazo hutaki zikaguliwe kwa kuficha aibu.

Sasa tunaomba uache kutuhadaa kuwa ATCL inajiendesha kwa faida.
Pascal Mayalla, usikasirike, najua wasukuma mmeshikamana ili kuteteana hata kwenye ujinga.
Mwenyekiti wa saccos yetu ana vx lakini saccos haina office zake zenyewe
 
wabongo kwa kutafuta cha kusema hawakosagi,
uchumi wa nchi unashikiliwa na 1%, acheni hao wakamuliwe ili nasie tupate japo kidogo.
au unadhani serikali inavoajiri matrafiki weengi hawana akili? wanajuwa wapi pa kiminya ili zitoke.
acha wanunue midege wawaminye vzr mabwanyenye ili hospital zijengwe kwa wingi
 
Jana umesema tumepata USD 14mil. Tunaomba CAG report ambayo ameikagua ATCL. Tunajua ATCL ni miongoni mwa asasi ambazo hutaki zikaguliwe kwa kuficha aibu.

Sasa tunaomba uache kutuhadaa kuwa ATCL inajiendesha kwa faida.
Pascal Mayalla, usikasirike, najua wasukuma mmeshikamana ili kuteteana hata kwenye ujinga.
Hii sentensi ya mwisho nimecheka utadhani nimeambiwa ndege moja nitapewa mimi 'yote yote'.

Hebu punguza maneno babu, twende tukachape kazi tulipe kodi na zingine zije tutembee kifua mbele. (kwa sasa vifua viko nyuma)
 
Mkuu inabidi ubadilishe mtazamo wako, kwenye business tunaangalia faida. Kama biashara haina faida mfanyabiashara ataachana nayo, na kama ina faida mfanyabiashara ataongeza mtaji pamoja na kuitanua biashara kwa mapana zaidi.

Na ndio maendeleo yanavyokuja, baada ya muda tutakuwa tumefika mbali sana kutokana na hatua moja baada ya hatua nyingine.

Kama ukiwa huna, na kuamini kwamba huna, basi utaendelea kuwa huna.
-Tushukuru Mungu tumenunua Tv
-Umeme UPO wa kutosha kuwasha Tv tofauti na awamu zilizopita (hata mgao wa umeme imekuwa historia"
just open your mind umeme upo mkuu
-Chakula KIPO mkuu, hatujasikia njaa muda mrefu, tumshukuru Mungu kwa kutulinda na janga la njaa
-Nyumba IPO Mungu ametubariki, nyumba ina amani na utulivu unapatikana nyumbani
Unajua Bei ya unga Sasa hivi huko kwa wanyonge
 
Propaganda za maccm zingesaidiwa na strong propaganda za upinzani kwa mtindo wa kukosoa ili kuziboresha....

tatizo propaganda za upinzani zinakuja kwa mtindo wa taarabu, uzushi na majungu.
Ila mwenyekiti wenu anaongoza kwa propangada utafikiri mtu wa pwani.
 
Nilipo pata akili timamu ndio nilipoacha kuwasikiliza hawa watu...wanafiki sana ilani ya CDM 2015 inajieleza
 
mngekuwa mna akili tungeona tofauti ya nani is a really fool...

Kwa sasa tunabaki equal na hationi propaganda za mwenyekiti wetu coz zinakuwa better kuliko ujinga wa wanaomkosoa

Ingefaa wanaomkosoa wawe na akili kubwa na umakini....

Wasalimie USA
Ila mwenyekiti wenu anaongoza kwa propangada utafikiri mtu wa pwani.
 
mngekuwa mna akili tungeona tofauti ya nani is a really fool...

Kwa sasa tunabaki equal na hationi propaganda za mwenyekiti wetu coz zinakuwa better kuliko ujinga wa wanaomkosoa

Ingefaa wanaomkosoa wawe na akili kubwa na umakini....

Wasalimie USA
Mzee wa propangada anawaharibu
 
Mtazamo wa kuajiriwa siyo mzuri. Serikali itaajiri wangapi weweeeee???! Umegonga shule bado unalialia kuajiriwa na serikali, kweeeli???!
Tatizo kubwa ni mfumo wetu wa ajira. Unazalisha vilaza wasomi. Utakuta msomi ana digrii na bado anailaumu serikali kutoajiri. Yaani kwa kifupi hajui wajibu wa serikali.

Wajibu wa serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi ili shughuli za uzalishaji zifanyike kirahisi (na ziajiri hao watu). Katika hiyo process serikali inaweza ajiri watu kama "vitendea kazi" ikiwa inahitaji kufanya hivyo!

Wajibu mwingine ni kufanya uzalishaji pale ambapo sekta binafsi haiwezi. Mfano elimu, afya, nk. Hapo ndipo itaajiri walimu, maktari, nk. Ikiwa inadhani wanatosha hailazimiki kufanya hivyo!

Huko shule nadhani kuna wengine huwa wanaenda kusomea ujinga na kulaumu tuu.
 
Back
Top Bottom