Ndugu zangu naomba niwaweke sawa kuhusu uchaguzi wa meya jiji la Arusha. Ni kweli taratibu zote zilifuatwa katika uchaguzi ule. Uchaguzi ulifanyika baada ya kuahirishwa kutokana na sintofahamu ya mjumbe mmoja ambaye ni mbunge wa viti maalumu kupitia Tanga na ni katibu wa CCM mkoa wa Arusha ambaye ni Mary Chitanda. Kutokana na hilo, ufafanuzi ulipatikana kuwa mjumbe yule ni halali kupiga kura. Utata ule ukawa umekwisha. Ulipowadia wakati wa kupiga kura CDM waliotoka nje kwenda kujadili katika hotel Equator iliyopo mkabala na halmashauri ya Arusha maana ilionekana wale diwani mmoja wa TLP tayari alishanunuliwa na CCM, wakiwa katika kikao hicho wenzao CCM waliendelea na uchaguzi wakisema CDM wamesusia uchaguzi ule na hapo ndipo walipopigwa bao la kisigino na CCM kwani walikwisha saini kwenye orodha ya waliohudhuria kikao kile.
Baada ya hilo, CDM iligundua CCM wamewazidi ujanja na ndipo walipojenga hoja unazozisikia hadi leo. Kiukweli CDM wakubali kuwa umeja wamepoteza kwa kuzidiwa fitna kidogo na CCM. CCM ilikuwa na wajumbe 16, na mmoja wa TLP 17. CDM 14 na 1 wa TPL 15, CDM wana mapandikizi yao mawili ndani ya CCM hivyo ingewaongezea kura hadi 17. Hivyo ukiangalia kura ambayo ingeamua nani awe meya ni za wale wanafiki wawili wa CCM na mmoja wa TLP basi na si vinginevyo.
Mwisho, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ilikaa na kujadili na nilifanikiwa kuiona nakala ya kikao hicho mara baada ya kumalizika ilikuwa inajieleza kabisa na CDM hawana mlango wa kutokea katika hilo.
Ikiwa kweli CDM wanadhamira ya kutengua matokeo basi wangeenda mahakamani kisha wangeandamana kushinikiza kesi isikilizwe haraka hapo ningeona kuna logic. Viongozi wote wa CDM wanalijua hili kwa mapana na marefu na ndiyo maana hawataki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa meya kwa kuwa kila kitu kipo wazi tena kwa ushahidi.
Mwisho, naungana na wale wote wanaosema kuwa matokeo ya umeya yatabadilishwa na mahakama pekee kwa kuwa suala hilo ni kisheria. CDM fungueni kesi kupinga matokeo na acheni blah blah za majukwani.
Nyumba haichomwi kwa maji ya moto.
Nakaribisha hoja tofauti na ukweli huu, ukihitaji zaidi niPM nikujuze ABC. Habari hii nimeiandika bila kuegemea upande wowote ule.