Tumekuwa watumwa na karakana ya shetani

Mwamba Usemao Kweli

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
744
186
Kiukweli watanzania tubadilike. Tunatia aibu jamii yetu kwa kujenga utamaduni wa kulalamikia kila jambo linalofanywa na serikali na viongozi wetu.

Napata shida sana kufahamu ni kipi hasa watanzania wanahitaji.

Serikali awamu ya nne imelalamikiwa sana kuwa dhaifu, fisadi, rais mzururaji, haikusanyi kodi na mengi mengineyo.

Serikali awamu ya tano imeamua kupambana na mambo haya ila sasa inalalamikiwa haifuati katiba wala sheria, serikali ya kidikteta, rais haendi nje ya nchi anakosesha fedha taifa.

Swali mnataka nchi iendeshweje?

JK ameenda sana nje yeye na wasaidizi wake kwa miaka 10 je tulipata fedha kiasi gani zilizoondoa umaskini?

• "Mtumwa hutumia uzushi na ujinga kutamka na kutenda kuliko hekima, busara na maarifa".

• "Mtumwa hugeuka kuwa mvivu wa kufikiri na kutenda na huishia kuwa karakana ya shetani kwa kuharibu yaliyo mema"

Tuepuka uharibifu.
 
Back
Top Bottom