Tumekubali kufanywa watumwa tena kama wazee wetu?

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Bila shaka kiwango changu cha hasira kimepitiliza leo.
Hivi sheria zipo Tanzania?
Kwanini tunaishi kwa kunyanyaswa na kubaguliwa ndani ya nchi yetu? Hivi wana jamii forum nyie ma- great thinker mmeshindwa hata kutatua changamoto ndogo ndogo zinazoweza kuzaa matatizo na shida kwa Taifa? Hivi sheria za nchi yetu zinaruhusu kampuni binafsi kujipangia muda wa kuingia kazini na kutoka? Tena muda unaonyonya nguvu za wananguvu kazi wa taifa letu!!! Unaambiwa kuingia kazini saa 1:00 asubuhi, kutoka saa 11:00 jioni. Sidhani kama hii ni sahihi kabisa, muda wakutoka hauzingatiwi kabisa wakati ikiwa muda wa kuingia ni limited. Ubaguzi umezidi, naskitika kusema kuwa ninyi wazee wetu ndio mmekuwa mstari wa mbele kukubali kubaguliwa kirahisi na hawa RAIA wa kigeni. Yaani unabaguliwa ukiwa kwako? kwakweli hii ni kwa Tanzania tu.
Ombi langu nikuona viongozi husika tembeleeni maeneo ya kazi ili mfahamu ni nini matatizo ya watu wenu wanayokumbana nayo huko, kisha yatatuliwe kwa usawa na haki, maana msije mkaanza kutatua tatizo kubwa lijalo kwa kufunguliwa na misiba mikubwa ya taifa. Haki zifuatwe ili kuepusha majanga makubwa kwa RAIA na Mali zao ( cc MOHAMMED BUILDERS
2bda786aff707386cf0996c14864e56c.jpg
LTD) Mvunja sheria za nchi.
 
Kama serikali haiwathamini wananchi wake huyo mgeni ndiye atakuthamini???Tukiendelea na CCM tujiandae kuwa wakimbizi wa ndani
 
Peleka malalamiko yako chama cha wafanyakazi mahali pa kazi.
 
Bila shaka kiwango changu cha hasira kimepitiliza leo.
Hivi sheria zipo Tanzania?
Kwanini tunaishi kwa kunyanyaswa na kubaguliwa ndani ya nchi yetu? Hivi wana jamii forum nyie ma- great thinker mmeshindwa hata kutatua changamoto ndogo ndogo zinazoweza kuzaa matatizo na shida kwa Taifa? Hivi sheria za nchi yetu zinaruhusu kampuni binafsi kujipangia muda wa kuingia kazini na kutoka? Tena muda unaonyonya nguvu za wananguvu kazi wa taifa letu!!! Unaambiwa kuingia kazini saa 1:00 asubuhi, kutoka saa 11:00 jioni. Sidhani kama hii ni sahihi kabisa, muda wakutoka hauzingatiwi kabisa wakati ikiwa muda wa kuingia ni limited. Ubaguzi umezidi, naskitika kusema kuwa ninyi wazee wetu ndio mmekuwa mstari wa mbele kukubali kubaguliwa kirahisi na hawa RAIA wa kigeni. Yaani unabaguliwa ukiwa kwako? kwakweli hii ni kwa Tanzania tu.
Ombi langu nikuona viongozi husika tembeleeni maeneo ya kazi ili mfahamu ni nini matatizo ya watu wenu wanayokumbana nayo huko, kisha yatatuliwe kwa usawa na haki, maana msije mkaanza kutatua tatizo kubwa lijalo kwa kufunguliwa na misiba mikubwa ya taifa. Haki zifuatwe ili kuepusha majanga makubwa kwa RAIA na Mali zao ( cc MOHAMMED BUILDERS
2bda786aff707386cf0996c14864e56c.jpg
LTD) Mvunja sheria za nchi.

Fanya kazi acha uvivu wewe, wenzako Ujapani, Korea na kwengineko mpaka wanaombwa na Serikali wachukuwe likizo wewe unalia kufanya kazi masaa 10 tu? Unafikiri uchumi unajijenga?
 
Japo Sera ni " hapa kazi tu" lakini vigezo vizingatiwe mkuu. Huko uchina na Japan wanafanya kazi kwa kuzingatia vigezo vyote na ndio maana watu hawatamani kuacha kufanya kazi.
 
Wameanza mambo ya vigezo baada ya kuendelea, wewe nchi masikini halafu unaulizia vigezo? Sasa hvivi ni kushukuru kwanza hata hiyo kazi ipo, piga kazi acha kulalama!
 
Viongozi wa Tanzania ni wezi.. Historia inajirudia. Mababu zetu waliwauza wenzetu kwa wazungu kama watumwa, na leo hii wanawauzeni bongo kwa wazungu. Mmeshakuwa watumwa tena.... Viongozi wapumbavu na wasio na weledi wa utawala bora. Mkapa ilitakiwa akamatwe. Mkapa ndiye kiongozi aliyeleta wizi wa juu bongo aka Grand Theft... Kabla ya mkapa rushwa nyingi zilikuwa miniscous. Bongo mmekwisha... Viongozi tunaowachagua wanatuuza tena kwa wazungu kama watumwa... Poleni.
 
Fanya kazi kwa bidii na pia pigania haki zako nyingine. usikubali kunyanyaswa na wageni ndani ya taifa lako
 
Back
Top Bottom