MP CHACHANDU
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 875
- 616
Nichukue fursa hii kuandika Uzi huu kwa huzuni kubwa sana. Mimi ni miongoni mwa vijana 348 tulioajiriwa na mahakama ya Tanzania mwezi June 2016 na kupewa mitakaba ya kazi na kupangiwa kituo cha kazi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha.
Nilipewa na pesa ya kujikimu pamoja na hivyo nilipanga nyumba kwa ajili ya kuishi mimi baada ya kuanza zoezi la uhakiki wa watumishi hewa tulirudishwa nyumbani kwa muda, tulipowauliza maafisa utumishi wetu walitujibu kuwa tutarudi kazini baada ya miezi miwili tu.
Leo hii huu mwezi wa nane tupo nyumbani hatujui hatima yetu serikali IPO kimya kwanini wasituambie ukweli ?
Cha kuhuzunisha zaidi ni juzi mhe. Rais Magufuli aliposema idara ya mahakama ina watumishi wa kutosha hivyo hakuna haja ya kuajiri tena mbali wafikri kupunguza.
Je, Sisi tupo kwenye kundi gani tulioajiriwa na kusainishwa mikataba ya kazi na kupangiwa vituo vya kazi?
Hii ni haki kumsainisha mkataba mtu halafu unamwachisha kazi bila sababu ?
Au tumekoswa mtu wa kututetea sisi tulioajiriwa na tume ya utumishi wa mahakama?