Kati ya mambo ambayo yamestua wengi kipindi cha karibuni ni kushuka kwa shilingi ya Tanzania kilinganisha na dola ya USA hadi kufikia £=2000 na kitu. Huku tukiwa tunamtafuta mchawi ni nani aliyeturoga, kuna vitu vya msingi ambavyo vimeachwa holela tu, vinachangia kwa kiasi kikubwa kuididimiza hela yetu chini zaidi na zaidi.
1. Ingia kwenye basi lolote la mkoani halafu jaribu kuuliza abiria wengine tiket wamekata kwa kiasi gani utashangaa. Kila mtu na bei yake lakini safari ni ile ile na basi ni lile lile. Kwa hapa bongo ukiondoa safar za morogoro, mikoa mingine yote haina fixed fare au nauli.
2. Nenda kariakoo, fanya utafiti mdogo tu ingia maduka matatu tofauti na ilizia bei ya kiatu au suruali ya aina ile ile. Bei utakazokuta utashangaa mwenyewe kila duka na bei yake kwa kitu kile kile. Hii maana yake nn? Kila mtu ana uamuzi wa kufanya kile anachotaka bila ya kuulizwa kwahiyo mzunguko wa hela unakuwa mdogo maana hela inabaki kwa wachache.
3. Cement za bongo mfuko mmoja ni 13500/= mpaka 14000/=, wakati kuna cement za pakistan pamoja na usafiri kutoka huko na kodi za bandari bado mfuko ni 10000/= mpaka 12000/=.
Viwanda vya ndani vinawakamua watanzania hata ukija kwenye bei ya sukari hailingani na uwepo wa viwanda vinne vya sukar nchini.
4. Bei ya nyumba za kupanga nalo ni tatizo, mwenye nyumba akiamka tu vibaya utasikia kuanzia Januari kodi inapanda hutaki unahama na ukihama leo kesho mwenzako ameingia wenye nyumba wamekuwa miungu watu. Mpangaji akajitetee wapi, hakuna vyombo vinavyoregulate kodi za nyumba, hakuna mtu anaesimamia. Je hizi nyumba zinalipa kodi maana ile ni biashara kama biashara nyingine, no one care.
5. Tofauti ya mishahara kati ya kima cha chini na cha juu. Tofauti ya mishahara kati ya wizara za serikali na mashirika ya umma hapa ndo unaweza kulia kabisa kama huna moyo wa jiwe.
Ukiangalia mshahara wa karani anaenza kazi kwenye halmashauri na yule anaenza kazi labda kwenye mfuko wa hifadhi wa umma tofauti ni kubwa sana.
Turekebishe ratio za mishahara atleast ifike 1:3 kati ya kima cha chini na kima cha juu.