Juma chief
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 2,764
- 2,366
Benki ya Dunia yasifu ustahimilivu wa uchumi wa Tanzania
Benki ya Dunia imesema Tanzania inafanya vizuri katika sekta ya uchumi kuliko nchi nyingine jirani kama Kenya na Uganda kwa ukuaji imara wa uchumi wa asilimia 6 hadi 7.
Mtendaji mkuu wa Benki ya Dunia anayeshughulikia mambo ya Tanzania Bi. Bella Bird alisema hayo katika mkutano wa 9 wa shirika hilo kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, akaongeza kuwa Tanzania ni moja ya nchi tatu za kusini mwa Sahara, pamoja na Rwanda na Ethiopia, ambazo zina mwelekeo mzuri wa kiuchumi.
Pia amesema Tanzania imefanikiwa kupunguza kiwango cha umaskini kutoka asilimia 60 hadi 47, na kutokana na ongezeko lake la uchumi, kiwango hicho kinaweza kuendelea kupungua.
Ameihamasisha Tanzania kuendeleza uchumi kwa kutunga sera zenye ufanisi na kupanua uwekezaji ili kuongeza ajira na kupunguza umaskini