Tumecheka na nyani RUSHWA, sasa tunakula mabua!!!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanganyika, halafu Tanzania huru, rushwa inatolewa nje nje.
Tumeichekea na kuomba na kusali itokomee yenyewe bila kuchukua hatua madhubuti, tukifikiri Mola huko juu atasikia kilio hiki.
Leo rushwa imeingia Bungeni, tena kwa mbwembwe.
Safari hii maafisa waandamizi wa Serikali WAMEDIRIKI kuwapa rushwa wawakilishi wa wananchi ili wasiwatetee na kuupigia kelele uozo ndani ya dola.
Hili limetushtua sana, tena sana.
Imenichukua karibu masaa 12 hili litulie akilini na kuelewa maana yake halisi.
Si vizuri kuchimba mtu lakini lilotokea si la kawaida kabisa.
David Jairo ni Afisa mwandamizi mwenye mizizi iliyokomaa ndani ya Ikulu.Amekuwa na kulelewa enzi za Kambarage.
Leo kuyaona haya kwa tunaomfahamu, hili linatushangaza sana.
Lakini tata jilaumu wenyewe kwa vile rushwa leo imekuwa mchezo wa kuigiza, sasa hodi limefika sebuleni.
 
Leo rushwa imeingia Bungeni, tena kwa mbwembwe.
Safari hii maafisa waandamizi wa Serikali WAMEDIRIKI kuwapa rushwa wawakilishi wa wananchi ili wasiwatetee na kuupigia kelele uozo ndani ya dola.
Hili limetushtua sana, tena sana.
wana ndugu ulitegemea nini wkati sasa rushwa ni fair game!
Hakuna mla rushwa alyefukuzwa kazi wala kuwajibishwa so far.
Hata hao wala rushwa maarufu wa RADA, RICHMOND,KAGODA wote wana peta.
Tusitegemee jipya hapa, hata mimi ningekuwa Jairo ningetoa michuzi tu mambo yangu yaende fasta!!
 
Kwani hamjiulizi kwa nini watu wanakimbilia ubunge na siasa hawaijui.
Kama hamjui jibu,jibu ndo hilo
 
Na sasa haya yakitokea hajaibuka tu ghafla , si ajabu hii rushwa imekuwapo muda mrefu.
Wawakilishi wetu msikubali kulishwa sumu ya rushwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom