Tume yatangaza tarehe ya uchaguzi Zanzibar

abdulrahim

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
408
286
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limefanywa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.
Bw Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
"Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," amesema Bw Jecha.
"Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu."
Source: Tume yatangaza tarehe ya uchaguzi Zanzibar - BBC Swahili
 
"hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," said by Jecha Salim Jecha..
Mnaoijua Katiba si vibaya mkatupa elimu na sisi.
 
wanarudia uchaguzi upi wakati mshindi anajulikana? mshindi atangazwe yaishe, otherwise nikupoteza rasilimali zetu tu.
 
ninachojiuliza ni kwamba..
lengo la uchaguzi huo ni kumpata kiongozi ambae ni chaguo la wengi,chaguo la watu au chaguo la nani ?
nimeamini demokrasia tanzania ni kile kinachowanufaisha wanaCCM hata kama ni mauwaji.
 
Haya sasa kipenga kimepulizwa, uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu, tume iwe huru, taratibu za uchaguzi zifuatwe, mshindi atangazwe bila kuchakachua matokeo
 
Mkuu nia ya kuitisha uchaguzi mwingine huko zanzibar ni kuwapa ushindi ccm na si vinginevyo namaanisha ccm itatumia kila mbinu iwezavyo ili ishinde hata kwa kumwaga damu na kwa kurudia kwa uchaguzi hata kama cuf ikishinda kama ikishiriki haiwezi tangazwa mshindi ccm inaweza kujitangaza mshindi kwa nguvu kwa hiyo ni kazi bure kutumia rasilimali za watu wa zanzibar kwa kufanya kitu ambacho hakina democrasia yoyote afadhali wangejitangaza ili kazi iendelee ili tujue moja,,,,,,!!!!
 
Wamtangaze Tuu huyo Shenii wao..Waepushe kumwaga Damu za watuu..
Jecha ni hopeless
 
wanarudia uchaguzi upi wakati mshindi anajulikana? mshindi atangazwe yaishe, otherwise nikupoteza rasilimali zetu tu.
Usiwe bwege na lofa wewe. Mshindi gani anajulikana wakati Tume haijatangaza? Unapaswa kukamatwa na kushtakiwa kwa
Mkuu nia ya kuitisha uchaguzi mwingine huko zanzibar ni kuwapa ushindi ccm na si vinginevyo namaanisha ccm itatumia kila mbinu iwezavyo ili ishinde hata kwa kumwaga damu na kwa kurudia kwa uchaguzi hata kama cuf ikishinda kama ikishiriki haiwezi tangazwa mshindi ccm inaweza kujitangaza mshindi kwa nguvu kwa hiyo ni kazi bure kutumia rasilimali za watu wa zanzibar kwa kufanya kitu ambacho hakina democrasia yoyote afadhali wangejitangaza ili kazi iendelee ili tujue moja,,,,,,!!!!
Tunataka mshindi apatikane kwa haki siyo mtu kujitangazia ushindi!!!!!!
 
Usiwe bwege na lofa wewe. Mshindi gani anajulikana wakati Tume haijatangaza? Unapaswa kukamatwa na kushtakiwa kwa

Tunataka mshindi apatikane kwa haki siyo mtu kujitangazia ushindi!!!!!!
niondolee usenge wako hapa! mmezoea vya kunyonga. mshindi atangazwe na maamzi ya wananchi yaheshimiwe!
 
Back
Top Bottom