Tume ya Uchaguzi yawashukia waangalizi wa kimataifa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kuhusu ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, iliyowasilishwa na Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU).

NEC imesisitiza kwamba ripoti hiyo imebainisha mapungufu ambayo hayapo kwenye sheria na taratibu, zinazoiongoza tume hiyo.

Miongoni mwa mapungufu waliyoyatoa waangalizi hao ni Suala la Uchaguzi wa Zanzibar, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na haki ya wagombea binafsi kugombea nafasi katika uchaguzi wowote wa Tanzania Bara na Zanzibar, mgawanyo wa majimbo na uwazi wa kuhesabu kura.

Akitoa ufafanuzi huo, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, waliwapa nafasi hiyo waangalizi wa ndani na nje kuangalia uchaguzi wa Tanzania Bara , kama unaenda kulingana na Katiba, sheria na taratibu za uchaguzi huo.

Alisema kuwa katika ripoti hiyo, waangalizi hao wamezungumzia uchaguzi wa Zanzibar, ambao NEC hawahusiki nao na kwamba wamefanya makosa, kwa kuwa wao walikuwa waangalizi wa uchaguzi wa Tanzania Bara na sio Zanzibar.

‘’Waangalizi wowote wa uchaguzi wanapoomba kibali kuangalia uchaguzi, wanatakiwa kufuata taratibu kwa kutambua kwamba kuna NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Sisi tulitoa kibali kwa waangalizi hawa kuangalia uchaguzi wetu na sio wa Zanzibar,’’ alisema.

Aliongeza kuwa, ‘’hawakupaswa kuingiza katika ripoti yao masuala ya uchaguzi wa Zanzibar ulivyokuwa, badala yake wangeeleza kama NEC hatukufuata sheria na taratibu kwenye uchaguzi huu wa Tanzania Bara.”

Alisema pia kuwa waangalizi walitakiwa kuangalia uchaguzi huo na sio kupendekeza kwamba uchaguzi ulitakiwa kuwa vipi. Kuhusu suala la mgombea binafsi, alisema Katiba iliyopo sasa haijaruhusu, hivyo wasingeweza kuweka wagombea hao, kwani Katiba ingewabana.

Kailima alisema kuwa endapo Katiba Inayopendekezwa ingepitishwa, waangalizi hao wangeweza kuhoji kwa nini hakukuwepo na mgombea binafsi, kwani ndiyo inaeleza kuhusu mambo hayo.

Akizungumzia mgawanyo wa majimbo, Kailima alisema kuwa kila halmashauri ya mji na wilaya ni jimbo na kwamba hawapaswi kulinganisha kati ya Halmashauri ya Temeke yenye watu 419,612 na jimbo la Madaba lenye watu 27,502, kuwa mgawanyo wake haukufuata uwiano.

Alisema kuwa mgawanyo wa majimbo, huzingatia mambo mengi, ikiwemo jiografia ya eneo lenyewe. Alieleza pia kuwa NEC haijawanyima haki Wazanzibari kwa kutoongeza idadi ya majimbo, kwa kuwa Bunge ambalo lilitakiwa kujadili, lilikuwa limekamilisha kazi yake.

Alisema kwamba ZEC yenyewe ilichelewa kutangaza mabadiliko hayo ya majimbo kutoka 50 hadi 54.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania matokeo ya uchaguzi wa Madiwani na Wabunge yalikuwa yanabandikwa kwenye vituo vya kupigia kura pamoja na matokeo ya awali ya Rais.

Alisisitiza kuwa matokeo yote, yalikuwa yanasainiwa na wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa na kutangazwa kwa wananchi.

Aidha, alisema kuwa hawakuweza kutangaza wabunge wa viti maalumu kabla ya uchaguzi, kwani kisheria wanachagua wagombea hao baada ya kujua idadi ya kura ya asilimia tano zilizopata chama, hivyo wasingeweza kutangaza kabla ya uchaguzi.

Hata hivyo, alisema kuwa Tume hiyo imepokea mapendekezo yao na itayafanyia kazi ikiwemo kuwa na watumishi kwa ngazi zote. Kailima alisema kuwa hali hiyo, itawasaidia kujua namna ya kuwaadhibu watumishi ambao watakiuka utaratibu wa NEC.

‘’Pia tutaongeza muda wa daftari la kupiga kura kuhakikisha kwamba kwa mwaka linakuwepo mara mbili ili wapiga kura wote waangalie. Lakini suala la Sheria ya Makosa ya Mtandao wanatakiwa kulipeleka kwa wahusika na mengine kwa serikali kwani sisi kama NEC hatuhusiki nayo,’’ alisema.

Chanzo: Habari leo
 
Tume ya uchaguzi ya zanzibar yaani ZEC, inaongozwa na Jecha, ok mkuu tumekusikia
 
Tofauti ya NEC na ZEC ikoje? Nadhani kuna haja ya kutumia neno TEC badala ya NEC ili kuondoa mkanganyiko huo. Maana walidhani NEC inajumuisha kote
 
Wadhungu pumzi imeishia wamebakia kutapatapa, hii ndo Tz bwana ile ile kama ya Nyerere. Wakajifunze upya la sivyo nao tutawatumbua mapema tu
 
Hawa wazungu huwa wanakurupuka tu.
1. Wanadhani nchi yetu inapaswa kuendeshwa kwa mjibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi zao.
2. Wanadhani Zanzibar ni nchi yaani Tanzania kwao ni nchi mbili, kwa maana ya two sovereign states.
3. Hawana habari kuwa Zanzibar ni state mojawapo tu kwenye URT (United Republic of Tanzania) kama kwa mfano Ohio kwenye USA. Tofauti ya URT na USA ni kuwa sisi zile states zingine ukiacha Zanziba ni kuwa ziko inactivated. Hili ndili huwa linawachanganya hawa watu, kwani states zetu zingine kama Tanganyika huwa hazionekani.
4. Hivyo uchaguzi wa Zanzibar ni sawa na uchaguzi wa serikali ya Ohio kule USA na haukuwahusu kabisa.

Hakika hawa nao ni vilaza au wanajifanya vilaza ili wapate sababu ya kutunyima pesa zao ambazo chimbuko lake zilitoka na zinaendelea kutoka kwetu.
 
Tanzania bara ndio nchi gani? Na zanzibar ni nchi ya wapi? Na NEC ni tume ya uchaguzi ya nchi gani hivi nec ina wanasheria kweli?
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kuhusu ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, iliyowasilishwa na Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU).

NEC imesisitiza kwamba ripoti hiyo imebainisha mapungufu ambayo hayapo kwenye sheria na taratibu, zinazoiongoza tume hiyo.

Miongoni mwa mapungufu waliyoyatoa waangalizi hao ni Suala la Uchaguzi wa Zanzibar, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 na haki ya wagombea binafsi kugombea nafasi katika uchaguzi wowote wa Tanzania Bara na Zanzibar, mgawanyo wa majimbo na uwazi wa kuhesabu kura.

Akitoa ufafanuzi huo, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema kuwa kwa mujibu wa sheria, waliwapa nafasi hiyo waangalizi wa ndani na nje kuangalia uchaguzi wa Tanzania Bara , kama unaenda kulingana na Katiba, sheria na taratibu za uchaguzi huo.

Alisema kuwa katika ripoti hiyo, waangalizi hao wamezungumzia uchaguzi wa Zanzibar, ambao NEC hawahusiki nao na kwamba wamefanya makosa, kwa kuwa wao walikuwa waangalizi wa uchaguzi wa Tanzania Bara na sio Zanzibar.

‘’Waangalizi wowote wa uchaguzi wanapoomba kibali kuangalia uchaguzi, wanatakiwa kufuata taratibu kwa kutambua kwamba kuna NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Sisi tulitoa kibali kwa waangalizi hawa kuangalia uchaguzi wetu na sio wa Zanzibar,’’ alisema.

Aliongeza kuwa, ‘’hawakupaswa kuingiza katika ripoti yao masuala ya uchaguzi wa Zanzibar ulivyokuwa, badala yake wangeeleza kama NEC hatukufuata sheria na taratibu kwenye uchaguzi huu wa Tanzania Bara.”

Alisema pia kuwa waangalizi walitakiwa kuangalia uchaguzi huo na sio kupendekeza kwamba uchaguzi ulitakiwa kuwa vipi. Kuhusu suala la mgombea binafsi, alisema Katiba iliyopo sasa haijaruhusu, hivyo wasingeweza kuweka wagombea hao, kwani Katiba ingewabana.

Kailima alisema kuwa endapo Katiba Inayopendekezwa ingepitishwa, waangalizi hao wangeweza kuhoji kwa nini hakukuwepo na mgombea binafsi, kwani ndiyo inaeleza kuhusu mambo hayo.

Akizungumzia mgawanyo wa majimbo, Kailima alisema kuwa kila halmashauri ya mji na wilaya ni jimbo na kwamba hawapaswi kulinganisha kati ya Halmashauri ya Temeke yenye watu 419,612 na jimbo la Madaba lenye watu 27,502, kuwa mgawanyo wake haukufuata uwiano.

Alisema kuwa mgawanyo wa majimbo, huzingatia mambo mengi, ikiwemo jiografia ya eneo lenyewe. Alieleza pia kuwa NEC haijawanyima haki Wazanzibari kwa kutoongeza idadi ya majimbo, kwa kuwa Bunge ambalo lilitakiwa kujadili, lilikuwa limekamilisha kazi yake.

Alisema kwamba ZEC yenyewe ilichelewa kutangaza mabadiliko hayo ya majimbo kutoka 50 hadi 54.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania matokeo ya uchaguzi wa Madiwani na Wabunge yalikuwa yanabandikwa kwenye vituo vya kupigia kura pamoja na matokeo ya awali ya Rais.

Alisisitiza kuwa matokeo yote, yalikuwa yanasainiwa na wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa na kutangazwa kwa wananchi.

Aidha, alisema kuwa hawakuweza kutangaza wabunge wa viti maalumu kabla ya uchaguzi, kwani kisheria wanachagua wagombea hao baada ya kujua idadi ya kura ya asilimia tano zilizopata chama, hivyo wasingeweza kutangaza kabla ya uchaguzi.

Hata hivyo, alisema kuwa Tume hiyo imepokea mapendekezo yao na itayafanyia kazi ikiwemo kuwa na watumishi kwa ngazi zote. Kailima alisema kuwa hali hiyo, itawasaidia kujua namna ya kuwaadhibu watumishi ambao watakiuka utaratibu wa NEC.

‘’Pia tutaongeza muda wa daftari la kupiga kura kuhakikisha kwamba kwa mwaka linakuwepo mara mbili ili wapiga kura wote waangalie. Lakini suala la Sheria ya Makosa ya Mtandao wanatakiwa kulipeleka kwa wahusika na mengine kwa serikali kwani sisi kama NEC hatuhusiki nayo,’’ alisema.

Chanzo: Habari leo
Mmewaita wenyewe kuangalia chaguzi zenu ili waone fedha yao ya misaada inavyotumika, sasa wanatoa ushauri, bada ya kutafuta namna ya kuufanyia kazi, nyie mnapinga kila wanachowashauri.
 
NEC ilisimamia uchaguzi wa Wabunge wa Jamhuri kule Zanzibar! Wachunguzi kutoka EU waliona kilichotokea Zanzibar ambapo vituo vya uchaguzi vilisimamiwa na NEC & TEC!
 
Mmewaita wenyewe kuangalia chaguzi zenu ili waone fedha yao ya misaada inavyotumika, sasa wanatoa ushauri, bada ya kutafuta namna ya kuufanyia kazi, nyie mnapinga kila wanachowashauri.

Kama hawataki ushauri watafute fedha zao.
 
Kujitete kwa NEC ni kuzidi kujianika katika udhaifu na udhalimu walioufanya. Mfano moja ni kura za Rais wa Jamuhuri ya Maungamo wa Tanzania. Swala hili linawahusu pia Zanzibar. Iweje basi waangaliza watazame tu Tanzania Bara?
 
Tume ya CCM ya uchaguzi imeteuliwa na Mwenyekiti wa CCM unadhani watatenda haki hawa katika maamuzi ya uchaguzi? Tunataka tume huru ya uchaguzi na si hii Tume fake ambayo Mwenyekiti wa CCM/Rais anaweza kuingilia maamuzi yake na wakafanya vile atakavyo kwa kuogopa vibarua vyao kuota nyasi.
 
Tanzania bara ndio wapi? Kwahiyo uchaguzi wa muungano ndio uchaguzi wa Tanzania bara?
 
Kailima
NEC ni huru ha ha haa .....
Don't insult our intelligence you clown
 
Hawa wazungu huwa wanakurupuka tu.
1. Wanadhani nchi yetu inapaswa kuendeshwa kwa mjibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi zao.
2. Wanadhani Zanzibar ni nchi yaani Tanzania kwao ni nchi mbili, kwa maana ya two sovereign states.
3. Hawana habari kuwa Zanzibar ni state mojawapo tu kwenye URT (United Republic of Tanzania) kama kwa mfano Ohio kwenye USA. Tofauti ya URT na USA ni kuwa sisi zile states zingine ukiacha Zanziba ni kuwa ziko inactivated. Hili ndili huwa linawachanganya hawa watu, kwani states zetu zingine kama Tanganyika huwa hazionekani.
4. Hivyo uchaguzi wa Zanzibar ni sawa na uchaguzi wa serikali ya Ohio kule USA na haukuwahusu kabisa.

Hakika hawa nao ni vilaza au wanajifanya vilaza ili wapate sababu ya kutunyima pesa zao ambazo chimbuko lake zilitoka na zinaendelea kutoka kwetu.
Hawa waangalizi wanakaribishwa na nani? Je, wanaamua kufunga safari na kuja bila kukaribishwa? Kwanini waje kama hakuna sababu? Pesa unazosema wanatafuta visingizio kutunyima na zilitoka huku je ilikuwaje sisi hatukuwahi kwenda kuwatawala ili nasi tuwanyonye? Sisi tunajidharirisha wenyewe kwa kupanda mitumbwe na kuzama kwenye bahari kila siku ili tuwafuate halafu tunawatukana.
 
Sasa kama waliwaalika kuangalia uchaguzi wa Tanzania kwanini wasiende na Zanzibar? Halafu sitaki kuamini kwamba NEC haikujua kama hawa jamaa wametuma waangalizi hata huko Zanzibar; by the way, kwani wale wabunge wa muungano from Zanzibar walipatikana kwa kura zilizo ratibiwa na NEC au ZEC? Tunajua uchaguzi uliosimamiwa na ZEC ulifutwa.
 
Mmewaita wenyewe kuangalia chaguzi zenu ili waone fedha yao ya misaada inavyotumika, sasa wanatoa ushauri, bada ya kutafuta namna ya kuufanyia kazi, nyie mnapinga kila wanachowashauri.

Pamoja na kuwaita lakini wanapaswa kuheshimu kanuni na taratibu zetu vinginevyo huenda walikuwa na mgombea wao kapigwa chini wanataka kuleta fïgisu figusi.
 
Back
Top Bottom