Izack Mwanahapa
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 497
- 236
KUMTANGAZA RAIS WA TANZANIA BILA MUSTAKABALI WA KURA ZA WAZANZIBARI NI KUITANGAZA ZANZIBAR HURU
Nianze kwa kurekebisha kauli ya mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi NEC alipokuwa akijaribu kuziokoa kura za Rais wa Jamuhuri ya muungano zilizopigwa na kuhesabiwa huko Zanzibar kwa kusema kwamba "Kuahirishwa kwa uchaguzi wa Zanzibar hakutaathiri mchakato wa uchaguzi Tanzania Bara" la hasha uchaguzi wa Zanzibar haujaahirishwa bali umefutwa na raisi anayetafutwa si Rais wa Tanzania bara bali Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
katika hali kama hii dosari zilizotajwa na Mwenyekiti wa ZEC wakati akitangaza kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar ikiwemo ile ya Wapigakura kuwa wengi kuliko watu waliojiandikisha kwenye daftari inaathiri pia kura zilizopigwa na Wazanzibari kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu waliopiga kura ni watu walewale, kwa idadi ileile katika vituo vilevile na maboksi yaleyele.
Kwenye uchaguzi wa Zanzibar Maboksi yalikuwa matano kwa maana ya mabox ya kumchagua Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, mabox ya kumchagua Rais wa Zanzibar, Mabox ya kuchagua wabunge, mabox ya kuchagua wawakilishi na mabox ya kuchagua masheha katika hali kama hii athari yoyote inayojitokeza kwenye vituo vya kura inahusu kura zote.
The principle of non contradiction says "Nothing can be and not be at the same time in the same sense" hivyo haiwezekani kura zilizopigwa na watu walewale kwenye vituo vile vile zikawa na uhalali upande mmoja wa muungano (Tanzania bara) na zisiwe na uhalali upande mwingine wa muungano (Zanzibar).
Uhalali wa kura za Zanzibar kwa mgombea urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ungetokana na ama kuondoa kauli ya kufuta uchaguzi na matokeo yake kule Zanzibar ama kusubiri matokeo ya kura za Wazanzibari baada ya uchaguzi kurudiwa ndipo mshindi wa urais wa Jamuhuri ya muungano atangazwe.
Suala hili ni la kitaifa na ni zaidi ya ushabiki wa kisiasa Kinachopaswa kuangaliwa hapa si wingi au uchache wa kura za wazanzibari bali tuangalie haki za kila upande wa muungano kwani Tanzania ni zao la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivyo sio busara kuubeza upande wowote kwa kigezo cha wingi au uchache wa watu au idadi ya kura.
Kwa hali ilivyo sasa ni kama vile upande mmoja wa muungano (Zanzibar) haujashiriki kumchagua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hali itakayopelekea mgogoro mkubwa wa kimuungano kwani Rais wa Jamuhuri ya Muungano atakosa uhalali wa kisiasa na kisheria kwa upande wa Zanzibar hali itakayowaongezea hari na kasi ya ushindi wale wanaotaka Zanzibar Huru.
Na: Izack Mwanahapa