Tume ya maadili mlikosea au mna jambo lenu?Mtuombe msamaha Watanzania kwa taarifa yenye makosa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,890
Akiwasilisha majina ya mawaziri ambao hawakujaza form jaji Salome Kaganda alimtaja pia waziri wa mambo ya ndani mheshmiwa Charles Kitwanga kuwa nae hajawasilisha tamko lake.

Wakati ukweli ni kwamba alikuwa amewasilisha ila ofisi yake ilifanya makosa ikiwa jaji wa kusimamia maadili anadiriki kufanya uzembe wa wazi namna hii nadhani anastahili kuadhibiwa.

Kuna siku atakuja leta upotoshaji wenye hasara kubwa sana kwa taifa haiingii akilini mtu mwenye taaluma ya sheria serikali inampa kila kitu alafu ameshindwa kujiridhisha kabla ya kuwatangaza watu hadharani.
 
Tume ya Maadili iwe makini katika utendaji wake hasa kipindi hiki cha Serikali hii mpya kuepuka kudhalilisha Viongozi kwa kutoa matamko bila kufanya uhakiki.

Nasema haya baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa tamko la kuhusu Mawaziri kutokurudisha fomu zao za maadili hazikuwa sahihi kwa baadhi yao hivyo kuleta usumbufu kwao,familia zao na hata jamii inayowazunguka kutokana na kosa la Tume hiyo kuwasilisha taarifa zisizo rasmi kwa Mhe.Waziri Mkuu, mfano nimegundua kuwa mmoja kati ya Mawaziri waliotajwa kutokurudisha fomu zake za Maadili Mhe Kitwanga(Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) alirudisha fomu yake tarehe 04 mwezi Januari mwaka 2016, na siku hiyo hiyo alirudisha fomu yake Ofisi za Bunge kwa mujibu wa Sheria..sasa iweje Bunge wawe nayo na Tume ya Maadili wasiwe nayo?

Na kutokana na Sheria ya Tume ya Maadili Kiongozi anatakiwa awe amejaza na kurudisha fomu yake ndani ya siku 30 baada ya kuteuliwa na ukiangalia Mawaziri waliteuliwa tar 12 mwezi wa 12 mwaka 2015 na hivyo kwa mtu aliyerudisha fomu tar 04 Januari bado amewahi maana siku 30 zinakuwa bado na kwa minajili hii natumaini Kamishna wa Tume ya Maadili Bi.Salome Kaganda inampasa aombe radhi kwa Mawaziri ambao kimakosa taarifa zao zimewasilishwa bila kuhakikiwa kwa Mhe Waziri Mkuu.

Na pia amuombe radhi Waziri Mkuu kwa niaba ya Tume yake ikiwa ni pamoja na kuangalia kwa makini watendaji wake ambao hawako makini katika kuangalia nani karudisha fomu na nani hajakamilisha ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kwa wahusika na pia siku nyingine wasirudie kosa kama hili.
 
Ila amemwaibisha waziri bila sababu, halafu mbona jina lake ni kaganda ni mganda
 
Hii tume imejidhalilisha sana. Mtu anakosea na kuonywa mara tatu. Sasa hata kama walikuwa kweli hawajarudisha je kuna effort gani imetumika kuwakumbushia au ni kujiatafutia sifa za bei rahisi kwa Rais na kwa Waziri Mkuu?

Huyu mama anastahili kuondolewa pale. Hatufai watanzania. Huo ni unafiki. Pia mwajenga nyumba moja kwanini kugombea fito?
 
Akiri uzembe, aombe msamaha kwa waziri mkuu, waziri husika na watanzania aeleze wazi kwamba hali hiyo haitojirudia tena aangalie ustaarabu wa Kujiuzulu HAPA KAZI TU haiaford uzembe muulize Magufuli
 
Kwa hiyo mkuu, huyo Kitwanga kaonewa? Hebu tafuta video ya kwanza wakati mama Kaganda anaongea kuhusu urejeshwaji wa fomu za maadili, halafu angalia posture na gesture ya Kitwanga pindi jaji akilalama, bila kuwataja. Halafu hizo fomu zinarejeshwa bila kusaini? Hebu tuache siasa bwana. Kitwanga karejesha fomu jana. Full stop!!!
 
Hii tume imejidhalilisha sana. Mtu anakosea na kuonywa mara tatu. Sasa hata kama walikuwa kweli hawajarudisha je kuna effort gani imetumika kuwakumbushia au ni kujiatafutia sifa za bei rahisi kwa Rais na kwa Waziri Mkuu?

Huyu mama anastahili kuondolewa pale. Hatufai watanzania. Huo ni unafiki. Pia mwajenga nyumba moja kwanini kugombea fito?

Mkuu hizo fomu ni lazima zijazwe, utatumbuaje majipu watu wakati wewe mwenyewe unashindwa kutimiza majukumu yako. Huhitaji kubembelezwa.
 
Akiri uzembe, aombe msamaha kwa waziri mkuu, waziri husika na watanzania aeleze wazi kwamba hali hiyo haitojirudia tena aangalie ustaarabu wa Kujiuzulu HAPA KAZI TU haiaford uzembe muulize Magufuli

Mnamhukumu jaji bila kujiuliza. Mnadhani fomu zinarudishwa tu bila kusaini dispatch book? Muone jana Mahiga kasaini wapi. Mnaingia kwenye mitego ya wanasiasa kichwa kichwa.
 
Watu wanafki sana,, bado mnataka business as usual tu. Wakati wa kubebana na kuleana umekwisha, see the signs and take in the message.
 
Sio raia wa uganda, ila Kaganda=ametulia, motionless, kawa barafu, ice cream, maji ya barafu, au nguzo ya chumvi kama mke wa Rutu, etc

Yaani umenchekesha, watu jameni mnajua kufikir....
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Ila amemwaibisha waziri bila sababu, halafu mbona jina lake ni kaganda ni mganda

Ni kweli kamwaibisha sana. Je ingekuaje kama Rais angetangaza kuwatimua bila kuwapa muda wa ziada, si ingekuwa balaa? Huyu jaji alipaswa kuwatafuta mawazi kwanza na kuhakikisha kabla ya kupeleka majina. Saizi kila kitu kinafanywa kisifa mno. so bad.
 
Tume ya Maadili iwe makini katika utendaji wake hasa kipindi hiki cha Serikali hii mpya kuepuka kudhalilisha Viongozi kwa kutoa matamko bila kufanya uhakiki.

Nasema haya baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa tamko la kuhusu Mawaziri kutokurudisha fomu zao za maadili hazikuwa sahihi kwa baadhi yao hivyo kuleta usumbufu kwao,familia zao na hata jamii inayowazunguka kutokana na kosa la Tume hiyo kuwasilisha taarifa zisizo rasmi kwa Mhe.Waziri Mkuu, mfano nimegundua kuwa mmoja kati ya Mawaziri waliotajwa kutokurudisha fomu zake za Maadili Mhe Kitwanga(Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) alirudisha fomu yake tarehe 04 mwezi Januari mwaka 2016, na siku hiyo hiyo alirudisha fomu yake Ofisi za Bunge kwa mujibu wa Sheria..sasa iweje Bunge wawe nayo na Tume ya Maadili wasiwe nayo?

Na kutokana na Sheria ya Tume ya Maadili Kiongozi anatakiwa awe amejaza na kurudisha fomu yake ndani ya siku 30 baada ya kuteuliwa na ukiangalia Mawaziri waliteuliwa tar 12 mwezi wa 12 mwaka 2015 na hivyo kwa mtu aliyerudisha fomu tar 04 Januari bado amewahi maana siku 30 zinakuwa bado na kwa minajili hii natumaini Kamishna wa Tume ya Maadili Bi.Salome Kaganda inampasa aombe radhi kwa Mawaziri ambao kimakosa taarifa zao zimewasilishwa bila kuhakikiwa kwa Mhe Waziri Mkuu.

Na pia amuombe radhi Waziri Mkuu kwa niaba ya Tume yake ikiwa ni pamoja na kuangalia kwa makini watendaji wake ambao hawako makini katika kuangalia nani karudisha fomu na nani hajakamilisha ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kwa wahusika na pia siku nyingine wasirudie kosa kama hili.
hiyo form haina maana kwa sasa kwa sababu haijawahi kusaidia kupunguza Ufisadi, Tanzania hakuna maadili kabsa hiyo Tume yenyewe ni JIPU inabidi ifumuliwe usukwe upya kabsa maadili yamekwisha siku nyingi.
 
Hata mimi naunga mkono hoja, Tume imuombe radhi Waziri kwa kumjengea taswira mbaya mbele ya Umma.
Hii iwe ni alarm kwa wote wanaojiita watumbuaji kwamba wakati mwingine wanawaadhibu watu bila kuwa na taarifa zao sahihi na hivyo kuwaonea!

Huyo Jaji awajibike kwa taarifa za Uongo
 
Mimi nauliza kwamba ni kweli Jaji alikuwa sincere au ana mambo yake mwenyewe yamejificha nyuma ya hili ? Iweje mimi mpita njia niafuatilie na kujua kwamba bwana Kitwanga alisha weka kila kitu mezani yet yeye asijue na anazo mechanism zote ?
 
Back
Top Bottom