Tume ya Haki za Binadamu: Ukimya wa dola katika utekaji unashangaa na kutia aibu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,126
Ukimya wa dola katika utekaji unashangaa na kutia aibu – Tume ya Haki za Binadamu yaeleza
Apr 11, 2017 by Raia Mwema in Habari

MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga, amesema kujirudia kwa matukio ya kutekwa watu bila ya serikali kuwakamata wale wanaotekeleza matendo hayo, na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, ni jambo la kushangaza na la aibu kwa taifa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa tume hiyo, ni muhimu sasa kwa vyombo vya dola kuchukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wa matukio hayo ya utekaji.

Ushauri huo wa Nyanduga umezingatia ukweli kwamba katika siku za karibuni kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii, kuhusu matukio ya kupotea au kutekwa kwa wananchi katika mazingira yenye utatanishi, suala ambalo limeibua mijadala katika jamii.

Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na tukio la Aprili 5, 2017 msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa, maarufu kama Roma Mkatoliki na wenzake watatu walitekwa wakati wakiwa katika studio za Tongwe Records, eneo la Masaki Dar es Salaam, baada ya kuvamiwa na kundi la watu wasiojulikana na siku tano baadaye, yaani Aprili 10, 2017 msanii huyo alieleza mbele ya vyombo vya habari jinsi walivyotekwa na kuteswa.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Nyanduga anaeleza; “Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vitendo hivyo, kwani vinaashiria kuwepo kwa makundi yanayoendesha matendo ya utekaji watu kinyume cha sheria. Matukio ya hivi karibuni ya kuvamia kampuni za tasnia ya habari na mawasiliano au kuwateka watu, yanaashiria kutoweka kwa uvumilivu wa uwepo wa maoni tofauti katika jamii kuhusu mambo mbalimbali.”

Taarifa hiyo pia inakumbusha matukio ya namna hiyo yaliyowahi kutokea nchini ambayo kwa kadiri yanavyoendelea ni lazma hatua zichukuliwe. Matukio hayo ya kipindi cha nyuma ni pamoja na kutekwa kwa mwandishi wa habari wa Mwananchi Communication Ltd. (MCL) na Deutsche Welle (DW), Salma Saidi, Machi 19, 2016. Salma alidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, akitokea Zanzibar, na ilidaiwa aliteswa na kuachiwa baada ya siku kadhaa.

Tukio jingine ni lile linalomhusisha Mkuu wa Idara ya Utafiti na Sera wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Bernard Focus Saanane, maarufu kama Ben Saanane, aliyetoweka nyumbani kwake eneo la Tabata jijini Dar es Salaam Novemba 18, 2016 na mpaka sasa hajulikani alipo.

“Wakati Salma Saidi na Ibrahim Mussa na wenzake watatu walionekana baada ya muda mfupi, Ben Saanane bado hajulikani alipo, yapata miezi mitano sasa,” anaeleza Nyanduga kupitia taarifa yake hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo, Aprili 11, 2017.

Anaongeza; “Uchambuzi wa Tume unaonyesha kuwa waliotekwa wamefanyiwa hivyo kutokana na tasnia yao, au kutumia haki yao ya msingi ya uhuru wa maoni na kujieleza, haki ambazo zimeainishwa na kulindwa katika Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (1966), na Ibara ya 9 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (1986).”

Anasema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba hiyo, na matamko mbalimbali ya kimataifa yanayosisitiza haki hizo.

“Haki ya kujieleza inaweza kuhojiwa iwapo tu itatumika kinyume na hadhi ya mtu mwingine, au maslahi ya taifa, kiusalama, kiafya au kimaudhui, na itahojiwa kwa taratibu za kisheria zinazokubalika katika jamii inayoheshimu demokrasia, kwa kuzingatia Katiba ya nchi na mikataba ya Kimataifa,” anasema

Kutokana na hali hiyo, ameshauri mambo matano ambayo ni pamoja na kwanza, vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi, vifanye uchunguzi wa kina kuhusiana na matukio hayo, na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kuhakikisha kwamba waliohusika na kupotea kwa Bernard Saanane, na utekaji wa Salma Saidi, Ibrahim Mussa na wenzake wanapatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pili, alisema tume inapenda kuvitaka vyombo vya dola vya ulinzi na usalama, kuwahakikishia wananchi kwamba, watu wanaohusika na matukio haya siyo watu walioko miongoni mwa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama.

Tatu, aliweka bayana kwamba ili kuhakikisha hilo ni vema Jeshi la Polisi likatangaza mapema hatua lilizochukua juu ya mtu aliyeonekana na silaha akimtishia Nape Nnauye na kwamba kutosikika kwa hatua zilizochukuliwa kuhusu mtu huyo kunazidi kuacha hisia katika jamii kwamba analindwa asichukuliwe hatua za kisheria.

Nne, kupitia tume, anawaasa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa Bernard Saanane, na zitakazofanikisha kuwapata watekaji wa Salma Saidi, Ibrahim Mussa na wenzake.

Tano, anawakumbusha wananchi wote na vyombo vyote vya serikali, umuhimu wa kufuata taratibu za kisheria iwapo kuna malalamiko yoyote kuhusu matumizi mabaya ya uhuru wa maoni na haki ya kujieleza, na siyo kuendekeza utekaji na utesaji wa watu, kwani kufanya hivyo ni kujichukulia sheria mkononi na ni ukiukwaji wa sheria, ni matendo yanayotishia amani, na ni kinyume cha haki za binadamu na utawala bora nchini.
 
Kinacho shangaza majambazi wakifanya hujuma, haifiki wiki watatangaza wame wakamata. Lakini watekaji hutosikia hata kukamatwa, hii inaonesha serikali(usalama wa taifa) ndio wahusika wakuu.



Ndukiiiii
 
It is very unfortunate kwamba Pombe kadanganyika na ushauri wa Kagame na kuiga style ya utawala wa kidikteta wa Kagame. Kagame na Mseveni wanalazimika kutawala kimafia kwa sababu wao ni life presidents. Magufuli hata kama ana ndoto za kuwa rais wa maisha kwa Tanzania hilo asahau, huko tulishatoka na kamwe watanzania pamoja ni woga na ulofa wao hawawezi kurudi huko. Asahau kabisaa!
 
*KAULI ZA WABUNGE WA CCM BUNGENI JANA 11/04/2017*

Hivi Waziri wa Habari alikwenda kufanya nini katika Press ya Roma, mkiambiwa mlimteka mtakataa? Bora kusema ukweli kuliko kukaa kimya, najua mtasema kwa kuwa nilikosa uwaziri No! - *Juma Nkamia (CCM)*

Mimi nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM (machozi) - *Hussein Bashe (CCM)*...

Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu.-- *Ridhiwani Kikwete (CCM)*

Mimi ni miongoni mwa wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar licha ya kuimisi sana *-Hillary Aeshi (CCM)*

*Tafakari, Chukua hatua*
 
*KAULI ZA WABUNGE WA CCM BUNGENI JANA 11/04/2017*

Hivi Waziri wa Habari alikwenda kufanya nini katika Press ya Roma, mkiambiwa mlimteka mtakataa? Bora kusema ukweli kuliko kukaa kimya, najua mtasema kwa kuwa nilikosa uwaziri No! - *Juma Nkamia (CCM)*

Mimi nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM (machozi) - *Hussein Bashe (CCM)*...

Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu.-- *Ridhiwani Kikwete (CCM)*

Mimi ni miongoni mwa wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar licha ya kuimisi sana *-Hillary Aeshi (CCM)*

*Tafakari, Chukua hatua*
Huwa simshabikii saana Juma Nkamia kwa sababu kwa kawaida namjua huwa hana point. Ila kauli yake ya jana niliipenda na imekua "eye opener" kawa wengi ambao ni wavivu wa kufikiri. Roma ameitisha "press conference" ili afunguke kile ambacha watanzania wengi walikuwa wanahamu ya kujua. All of a sadden and for no reason mkutano ukawa unaongozwa na serikali. Yaani hata uwe fala utaelewa hii picha!
 
Ni kitu cha kushangaza sana Mkuu. Serikali haikusema chochote kuhusiana na huyo asiyejitambua Mwakyembe kuhudhuria mkutano ule. Watanzania wengi tuliokuwa tunafuatilia sakata hili tulijua ni mkutano wa Roma tu na wenzie. Kuwepo kwake pale kunathibitisha kushiriki kwa Serikali katika kutekwa na kuteswa Roma na wenzake. I hope hawajapewa sumu na iko siku labda yaliyojiri yatawekwa hadharani halafu wamejaribu kumnunua kwa kumpa $5,000 wahuni hawa.

Huwa simshabikii saana Juma Nkamia kwa sababu kwa kawaida namjua huwa hana point. Ila kauli yake ya jana niliipenda na imekua "eye opener" kawa wengi ambao ni wavivu wa kufikiri. Roma ameitisha "press conference" ili afunguke kile ambacha watanzania wengi walikuwa wanahamu ya kujua. All of a sadden and for no reason mkutano ukawa unaongozwa na serikali. Yaani hata uwe fala utaelewa hii picha!
 
Ni kitu cha kushangaza sana Mkuu. Serikali haikusema chochote kuhusiana na Mwakyembe kuhudhuria mkutano ule. Watanzania wengi tuliokuwa tunafuatilia sakata hili tulijua ni mkutano wa Roma tu na wenzie. Kuwepo kwake pale kunathibitisha kushiriki kwa Serikali katika kutekwa na kuteswa Roma na wenzake. I hope hawajapewa sumu na iko siku labda yaliyojiri yatawekwa hadharani halafu wamejaribu kumnunua kwa kumpa $5,000 wahuni hawa.
So sad! Hawa wanaweza kuwa wameshawadunga eti! Mafia in its making!
 
Back
Top Bottom