Tume ya haki ya jinai

Tume ya haki ya jinai

Msee Paka

Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
41
Reaction score
38
Ila kuna tatizo kidogo la uelewa kwa hawa watoa mada japo ndio kuna utitiri wa vyomba vyevye sura ya kijeshi lakini vimepitishwa kisheria.

Kitendo la kudharau vyombo hv ni kudharau sheria za nchi pia

Ila pia hichi chombo wanachokitetea ndio huwa wanakilalamikia kila kukicha kuwa wanabbikizia watu kesi, wanaua watu kwenye mahabusu, wanachukua rushwa, wanafanya kazi kwa maelekezo na zaid wanasema hawana weledi wakazi hata PGO yao hawaifahamu lakini leo naona wanawatetea zaid.

Ifikie hatua sasa waheshimu vyombo hv vya kijeshi hata kama vipo kama utitiri

Ikumhukwe jeshi kuu ni moja tu JWTZ na huwezi kulisikia likilalamikiwa sababu halijihusishi moja kwa moja na raia lakini majeshi mengine yaliobaki yanajihusisha moja kwa moja na raia ndo maana lawama zitakuepo tu.

Ikumbukwe kwamba raia hata uwafanyie nini hawawezi kuridhika lazima tu watoe dosari juu ya jambo fulani hiyo ni kawaida kabisa.

Wanachotakiwa kushauri ni vyombo hv sasa wanaoviita utitiri wavitolee mapendekezo namna gani vijiboreshe ili viweze kuwahudumia vzuri na zaid kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu.

Huwezi sema kazi za Uhamiaji, Zimamoto, Magereza, Tanapa nk zirudi kwa polisi utakua unajidanyanya, dunia nzima wana vyombo hivi ukitoa ambavyo kila chombo kina kazi yake.

Uhamiji ni chombo nyeti sana katika usalama wa wanaoingia na kutoka, wanaoshughulikia ukaaji wawageni, na kazi nyingi nyingi ambazo zimeainishwa kwa mujibu wa
Sheria hatuwezi kuzidharau hata kidogo.

Hivyo hivyo hatuwezi dharau majukum ita hv vyombo vingine ambavyo majukum hayo yamewekwa kwa mujibu wa sheria.

Hvyo basi ni vizuri tukajenga misingi ya kushauri nini kiboreshwe na sikusema majukumu ya vyombo apewe mtu mwingine.

Ni vizur sasa kila chombo kikaachiwa kifanye majukumu yake kwa mujibu wa sheria a endapo itatokea kuna makosa basi kikosolewe na kama kitakua kinavunja is sheria basi kisemwe.
 
Back
Top Bottom