BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,846
wakati zile zilizomaliza kazi walizopewa mapendekezo yao bado hayajafanyiwa kazi
Tume kuundwa kuchunguza Mgololo
Ikunda Erick, Dodoma
Daily News; Thursday,August 14, 2008 @00:03
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu amekubali kuunda Tume kuchunguza utata wa mkataba wa ubinafsishaji wa Kiwanda cha Karatasi cha Mgololo ambacho sasa kinajulikana kama MPM.
Dk. Nagu alikubali kufanya hivyo baada ya Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (Chadema), kutaka hatua hiyo ichukuliwe, wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi juzi ili kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo.
Katika kamati hiyo yaliibuka malumbano baina ya Waziri na mbunge huyo kuhusu utata wa mkataba wa kiwanda hicho, ndipo Mwenyekiti Anne Makinda aliamuru pande zote mbili zishirikiane kufanya uchunguzi na kuleta taarifa bungeni. Shirikianeni kufanya uchunguzi na mtuletee taarifa hapa bungeni, alisema Makinda ambaye ni Naibu Spika.
Awali, Dk. Slaa alisema utata wa mkataba unatokana na ukweli kwamba ingawa mkataba wa ununuzi wa kiwanda hicho unaonyesha Dola za Marekani milioni 26, ni dola milioni moja tu zilizolipwa. Dk. Slaa pia alisisitiza kuwa Kampuni ya Angel Hurst Industries ya Uingereza yenye hisa asilimia 99.88 katika kiwanda hicho haionyeshwi popote na haijulikani Brela.
Alisema wawekezaji wanaojulikana Brela ni Kampuni ya Rai Brothers ya Kenya yenye hisa asilimia 0.006. Akitoa maelezo ya hoja hiyo, Dk. Nagu alisema Kampuni ya Angel Hurt inajulikana Brela na imesajiliwa katika Visiwa vya Virgin kwa usajili namba 395195. Mapema Dk. Slaa alisema uchunguzi walioufanya ulionyesha kampuni hiyo haikusajiliwa katika visiwa hivyo.
Hata hivyo, Waziri Nagu alisema ubinafsishaji wa kiwanda hicho umekuja baada ya miaka 12 kukosa mwekezaji na hali ya kiwanda kuwa mbaya kwa kuwa kilisimamisha uzalishaji huku serikali ikiendelea kutumia fedha nyingi kugharimia matunzo ya mitambo, hivyo ilibidi kiuzwe kama mali. Hatua hiyo ilisababisha kiuzwe kwa dhana ya dola moja ya Kimarekani, lengo likiwa mwekezaji aendelee na uzalishaji, alisema Dk. Nagu.
Alisema kama ungetumika utaratibu tofauti na huo, wawekezaji Rai Brothers wangekuwa na uwezo hata wa kungoa mitambo ya kiwanda na kwenda kuipeleka Kenya. Baada ya kufafanua hayo, Dk. Slaa alisisitiza kuwa mkataba unaonyesha ni dola milioni moja na siyo dola moja, wakati thamani halisi ya kiwanda hicho ni dola za Marekani milioni 500.