Tume haingiliwi, hatuna madalali

Tume haingiliwi, hatuna madalali

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
424
Reaction score
1,281
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio vurugu za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Chande amekanusha uvumi wa kuwa Tume hiyo imeongezewa muda ili ripoti yao ichakachuliwe.

Jaji Chande ametaja sababu za kuomba nyongeza ya muda wa siku 21 kuwa ni Ukubwa, Uzito, Kina cha kazi na ushahidi uliochelewa kuwafikia na ripoti hiyo kutakiwa kuandikwa kwa lugha mbili ya Kiswahili na Kingereza.

Aidha, Jaji Chande amesema kuwa awali walipanga kufanya Uchunguzi katika mikoa sita lakini wamelazimika kufikia mikoa 12 na kukusanya taarifa mfano Kwanini Arusha kuwe na ghasia kubwa alafu Kilimanjaro zisiwepo, au Zanzibar kuwe shwari lakini Dar es salaam kuwe na ghasia wakati maeneo hayo yapo karibu.

Mwisho Jaji Chande amesema wanataka ripoti ikitoka iwasemee Waathirika na wajione wametendewa haki, na Tume hiyo imependekeza Maridhiano ili kurejesha mshikamano na umoja.
 
Anazuga tu huyo, hana ubavu wa kutoingiliwa na kutoa taarifa za uchunguzi kwa kina Abdul na mamake ili aelekezwe cha kuandika.
 
Back
Top Bottom