Tumbo kuunguruma kuna sababishwa na nini ?

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
724
551
Wana jf tumbo langu linaunguruma sana yaani waweza dhania nimemeza vyura kwani hukimbizana na kugonga kuta za tumbo.Sauti mpaka ninajishtukia kwani watu wanazisikia.Hivi tatizo ni nini?
 
Wana jf tumbo langu linaunguruma sana yaani waweza dhania nimemeza vyura kwani hukimbizana na kugonga kuta za tumbo.Sauti mpaka ninajishtukia kwani watu wanazisikia.Hivi tatizo ni nini?
Kuna gesi tumboni na hii inasababishwa na kula vitu ambavyo havijasagika vizuri unaoipa tumbo kazi ya ziada ya kusaga chakula
 
Kuna gesi tumboni na hii inasababishwa na kula vitu ambavyo havijasagika vizuri unaoipa tumbo kazi ya ziada ya kusaga chakula
Huenda unachosema ni kweli kwani nikila machungwa baada ya mlo miungurumo tumboni hupungua,ingawa sina ushahidi wa kisayansi wa hilo.
 
Epuka vyakula vya protein, wanga na fat.
Naomba unisaidie mbadala wake maana kwenye protini ninatumia sana samaki,nyama na dagaa kauzu na hapo kwenye wanga ninaumia sana dona na mchele.
 
Wana jf tumbo langu linaunguruma sana yaani waweza dhania nimemeza vyura kwani hukimbizana na kugonga kuta za tumbo.Sauti mpaka ninajishtukia kwani watu wanazisikia.Hivi tatizo ni nini?

Acha kula maharagwe Kula mboga za majani kwa wingi
 
Acha kula maharagwe Kula mboga za majani kwa wingi
Mboga za majani aina zipi?Maana nilikuwa napendelea mchicha,majani ya maboga,majani ya maharage lakini vyote hivyo sasa hivi ni kuunguruma kwa kwenda mbele!!
 
Ninapata vizuri ila likianza tu kuunguruma elewa hata choo ya kwanza itakuja ngumu sana mithili ya jiwe na kuitoa nitapiga kelele
usiku huu usile chochote kesho amka na vidonge vya michango/minyoo kisha uje na feedback baada ya dozi kuisha.

maana najua hapo hta kijampo kitakua hakikatiki coz tumbo kuunguruma huambatana na gesi kujaa ambapo ili itoke lazima ujambe.
 
Back
Top Bottom