Tumalize Utata: Messi Vs Ronaldo ulimkubali yupi zaidi?


Lakini kumbuka hata huyo Pele anayesemwa ni bora sana, hajawahi kucheza ulaya
 

Naunga mkono hoja
 
Kwa akili yako wewe Messi ligi gani itamshinda hapa duniani?.....hebu taja,hapa kipaji cha kuzaliwa kinahusika zaidi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kumradhi ila Wewe ni shabiki maandazi..

Kweli messi ni bora zaidi ya cr7 kwangu mimi, lakini, cr sio wa kumkosea adabu kiasi hicho. Bonge moja la player wa kukumbukwa daima kama moja ya wachezaji bora wa wakati woote
 
Itakuja chukua miaka mingi sana, kumpata mchezaji anaeweza kupachika mabao kama CR7 inaweza chukua hata miaka 100.Hajabebwa na mfumo wa timu,either timu itengeneze chance nyingi au chache yeye atafunga

Huyu CR7 kitu alichofanikiwa ,nikuficha kipaji chake kwenye Hardworking, Lakini ukimtazama kwa umakini sio tu hardworking ila anakipaji kikubwa sana tena sio kawaida cha kucheza mpira.

Mimi ni timu CR7 ila Messi ni complete player, Messi anafanya kila kitu uwanjani, Kwenye soka messi hajaacha kitu, messi amefanya vituko vyote amemaliza, hakuna jipya.
 
Top 3 ya wachezaji walionivutia toka nimeanza kufatilia soka na kuanza kuangalia games actively 2005 ni....1. Lionel Messi....2. CR7.....3. Andres Iniesta.

mimi ni shabiki pure wa United toka enzi za cr7 ila Messi alinifanya nikaipenda Barcelona....Ronaldo ni mchezaji bora sana sana na ambae sisi wapenda soka tumebahatika kumshuhudia..anastahili heshima yake ila kwa upande wangu, Messi ni JINI.
 
Reactions: PNC
Miller ni mchezaji mkubwa?
Sasa thomas muller unamfananisha na nani, michael sarpong? Jitu lina uefa champions league 2, ana world cup, bado mikombe kibao.. Na sio kapata kwa mgongo wa watu ana mchango mkubwa katika makombe hayo.. Kuwa na heshima kidogo mzee. Ana mpaka golden boot ya fifa worldcup 2010, 2014 akabeba silver ball.. Bado tu si kitu!?
 
nilianza kumpenda Ronaldinho muda wake ulipoisha nikawa shabiki wa CR7 mnyama mpaka leo ukizingatia aliwahi kupita kwenye chama langu la UNITED .nimebishana mara nyingi sana kuhusu Ronaldo na Messi hali iliyopelekea nikamchukia Messi na timu yake tena hii chuki ya Barcelona ndo sidhani kama itakuja kunitoka maana naweza kuwabetia na bado nikafurahia kusikia wamefungwa.kuna kipindi niliweka clips nyingi za magoli na skills za wachezaji wa Ulaya kwenye computer yangu,nilivyokuwa natizama mojamoja hasa zile za magoli nilijikuta navutiwa zaidi kurudia clip za Messi .kwa akili timamu niseme tu japo niliichukia lakini Barca ile ya Pep ndo ilikuwa timu inayoogopesha zaidi kucheza dhidi yao,Messi ndo alikuwa mchezaji hatari zaidi kumkabili sitasahau fainali ya Wembley....Iniesta ndo kiungo hodari zaidi kupata kumshuhudia.pamoja na ushabiki wangu kwa United lakini Messi na Iniesta wanaingia kwenye kikosi changu bora cha wachezaji niliowashuhudia kwa macho yangu japo timu lao silipendi mpk cku naingia kaburini.Ronaldo ni bora lkn Messi ni genius.
 
Messi ni Left Footer
Vs
Ronaldo ni Both Footer, na anafunga mpaka na vichwa.

Messi kawika Barcelona
Vs
Ronaldo kawika Lisbon, Man U, Real Madrid and now Juve.

Nje ya Barca hata Sarpong anamzidi Messi.
mpira haupimwi hivyo ukizungumzia hvyo kuna Ibrahimovic kacheza klabu nyingi kuliko yeyote.
Messi ana kipaji na ashahamia PSG ndan ya dakika 30 ame dominate mchezo mpk watu wakashangaa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…