Tulitambua ujinga wetu ni upi, badala ya kuushinda tukautumia kufaidika dhidi ya waliowajinga zaidi yetu

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,309
4,017
"Hivi lakini sisi watu weusi tuna shida gani kwenye akili zetu"

Hii ni moja ya kauli nyingi ambazo vijana wa kiafrika wanapenda kuisema pale wanapokuwa wakishangaa mambo ambayo yanafanywa na waafrika wenzetu.

Ujinga umekuwa approved kwetu, watu wajinga ndio wanaopata nafasi, ujinga ndio unaokuwa una trend, ujinga ujinga ndio umekuwa uwazi na ukweli.

Huko nchini China amabako ndio TikTok inapotokea, ukicheck kwenye reels zinazotrend huko TIKTOK ni videos za ubunifu na inventions lakini huku kwetu videos zinazo trend ni za matako na watu wakiwa wanafanya utumbo utumbo.

Mimi namiini Nyerere alijitahidi ku-eliminate ujinga ujinga hapa nchini, lakini aliowapa mwanga wasaidie kuendelea kukomboa jamii yetu na ujinga walijifanya kufanya hivyo huku wakitumia ujinga wa watu ili wao kufaidika kifedha, sifa na mamlaka.

Tumekuwa watumwa wa ujinga katika dini, tumekuwa watumwa wa ujinga katika kupigania haki zetu, tumekuwa watumwa wa ujinga katika ushirikina, and the list goes on.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom