Ni heri matendo mabaya ya mzungu kuliko ujinga wa mtu mweusi

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,263
2,000
Yanayo endelea Marekani ni Mambo ya kutisha Hasa kwetu watu weus ilianzia China now ni Marekani

Wote Kama mmeshuhudia Ile video nadhan mtakua mlijua mzungu ni mtu wa namna Gabi

Mtu analia hawezi kupumua Mpaka anakufa mzungu Hana habar Tena ndio kwanza kaweka pozi. Pia Sio kwamba hili tukio ndio la kwanza kwa Black American Mana wanakufa wengi Sana Tena vifo vya kifedhul na kidhalim

Kwanini nimesema ni Bora matendo mabaya ya mzungu kuliko ujinga wa mtu mweusi kwa sababu Nina uhakika katika kuratibu izo harakat za maandamano au kudai haki ya marehem Kuna watu weus wamewasalit wenzao kwa kutoa taarifa na kuripot mipango. Pia ilo linadhihirisha watu weus tuna matatizo makubwa Sana na hili linafanya nimuamin kanyewest sababu alisema tusiwalaum wazungu kwa utumwa sababu tulipenda wenyewe ili Jambo ni kweli kabisa

Kwa sababu kipind Cha utumwa asilimia 90% ya watumwa waliuzwa na ma cheaf wao na kumi ndio walio kua wana kamatwa msituni. Na ilikua ukiuzwa alafu ukatoroka kurudi Kijiji Basi utakamatwa na adhabu yako ilikua kufa.

Pia mfano umetoroka baada ya kua umeuzwa na kuamua kuto kurudi kwenye Kijiji chako na kwenda Kijiji kingine Basi ulikua hupokekew Kama mtu mweusi mwenzao Ila na wao walio kupokea kwenye icho Kijiji walikua wana kuchukulia Kama mtumwa na bidhaa Yao Basi ilikua unafungiwa ndani kusubir wazungu ndio Mana wazungu wawil walikua na uwezo wa kuwaongoza kwenye msafara waafrica hata Mia Tena walio Shiba bila matatizo yoyote kwenye Safar ndefu

Pia hata katika dunia yetu ya leo bado tunafanya Yale Yale muafrica anatoka AFRICA anaenda ulaya kwa mzungu kutusema vibaya waafrica tulio Baki nyumbani AFRICA na kuomba ufadhili ili aweze kufanya vurugu na kufanikisha anayo yataka

Tena kwa kumbembeleza mzungu alafu wazungu wakitufanyia ukauzu tunaanza kulia wakat sisi ndio tumemuita waafrica ifikie hatua tujue tukiendelea kua wajinga Basi tujue tutaish maisha yetu yote tukiitwa Nyan tutaish maisha ya kunyongwa Mpaka tushindwe kupumua.

Kama umeona Ile video pamoja na mzungu kuombwa japo atoe hata got ili jamaa apate kuvuta pumzi ya bure hata kwa dakika moja Ila mzungu kamnyima na kaakikisha mpaka anakuta Sasa jiulize wewe unae enda ulaya kunfata mzungu akusaidie upate unacho taka wewe Kama wewe umeahid kulipa fadhila kitu gan? Au kutuuza wote?
Mana mzungu Sio rafik hawezi kupa kitu for nothing

Waafrica tusipo amka dunia itakua mtihani kwetu
Pia SEREKAL zote za AFRICA zipinge zile kaul za vijana Bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa binadam AFRICA pia wale wa bongo Bahati mbaya waziwiliwe Tena ziwekwe Sheria Kali juu Yao?

Au mnaogopa wazungu watawaambia haki za binadam?
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,246
2,000
Nataka kuzama meli niende ng'ambo, kutafuta maisha, kwani naona maisha ya hapa mimi yamenishinda.
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
9,982
2,000
Wazungu wanakera sana, mi nashangaa serikali zetu zinapopokea misaada yao
 

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,341
2,000
Wazungu ni wetu walituletea ustaarabu.

Walituletea Biblia (Neno la Mungu) tukamjua Mungu wa kweli na wa pekee, Mungu wa Israeli, YEHOVA YWHW.

Ikiwa pamoja na kutufanyia hayo yote hadi leo waafrika wanaabudu mapangoni, ingekuweje kama wasingekuja huku gizani.

"dark continent"
 

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
5,652
2,000
Wazungu ni wetu walituletea ustaarabu.

Walituletea Biblia (Neno la Mungu) tukamjua Mungu wa kweli na wa pekee, Mungu wa Israeli, YEHOVA YWHW.

Ikiwa pamoja na kutufanyia hayo yote hadi leo waafrika wanaabudu mapangoni, ingekuweje kama wasingekuja huku gizani.

"dark continent"
Ustaarabu gani aliotuletea MZUNGU? au KUCHAMBIA TOILET PAPERS?, na Dada zetu kuvaa Nusu uchi?
 

DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,704
2,000
Watu weusi tunabaguliwa na kuteswa kila sehemu, kuanzia Arabia Hadi China Hadi Ulaya
Ila angalau ulaya utaenda kuwakuta watu weusi wengi wakitafuta maisha na kupewa uraia kabisa. Ni mara chache kuwakuta watu weusi wanaoishi na kuweka makazi kule china na uarabuni.

Hata weusi wakifanyiwa ukatili china au uarabuni hatua hazichukuliwi kama ulaya na Marekani. Nakwambia watu weusi tuna makosoro mengi hatujitambui kabisa ndio maana wanatunyanyasa
 

Esmarion

Member
Apr 18, 2020
21
45
Wazungu ni wetu walituletea ustaarabu.

Walituletea Biblia (Neno la Mungu) tukamjua Mungu wa kweli na wa pekee, Mungu wa Israeli, YEHOVA YWHW.

Ikiwa pamoja na kutufanyia hayo yote hadi leo waafrika wanaabudu mapangoni, ingekuweje kama wasingekuja huku gizani.

"dark continent"
Ustaarabu ni nini?
Na ustaarabu wetu ulikuaje kabla ya wazungu?

The true revolution comes from inside yourself....!
 

DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,704
2,000
Acha kuwatuhumu kabla Mzungu hajaja watu walikuepo wanavaa nguo. Kuvaa Nusu uchi tunaenda kule tulikotoka kama zamani kabla Mzungu hajatutawala.
Ustaarabu gani aliotuletea MZUNGU? au KUCHAMBIA TOILET PAPERS?, na Dada zetu kuvaa Nusu uchi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom