Tuliowahi okota embe dodo tukutane hapa

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Kuna wakati hadi unashukuru Mungu hata ulie machozi kwa jinsi ulivyo na bahati.

Wengine wamewahi okota fedha, wangine wachumba, wengine kazi.. etc.

Kuna mengine yanatokea kwa uzuri upande wako lakini sio mazuri kwa wengine.

Mfano huna pesa.. unampa mwuza duka buku ununue kitu cha buku ila ajabu anakurudishia elfu 9 akidhani umempa buku 10..

Mimi niliwahi rushiwa laki 5 na wakala wa mpesa hadi leo hawaja ulizia.. na unajua ukitumiwa fedha na wakala haina namba ya simu.. hivyo nipo nasubiri voda wanipigie leo ni mwaka wa 3.


Ebu twambie jambo gani ambalo ulijiona kama mtu mwenye bahati.
FB_IMG_1560915462432.jpeg
 
Ukifurahia ulichokiokota ujue huko aliyepoteza analalamika au hata anamwaga chozi.........niliwahi kuokota sh elfu 42, nikafurahi sana, lakini baada ya mwezi mmoja hivi nilikuja kupoteza sh laki 2 na elfu 80........machungu yake yake sitaki kabisa kuyakumbuka, sasa hivi nikiokota hela basi nitakaa eneo lile hata kwa nusu saa ili nikiona mtu anakuja huku anaangzaangaza chini najua ndio mwenye mzigo
 
Huamini katika miujiza ya mwenyezi Mungu.. Kuiba lazima kuwe na process ya planning .

Hujaiba ila umepewa
Kupewa ni lazima upewe kwa ridhaa ya mtoaji akiwa na akili timamu,huo ni wizi kama wizi mwingine tu,

Kama wewe ungerudishiwa chenji pungufu ungeamini kua ni miujiza ya Mungu amemzawadia mwenye duka au ungemuona muuzaji ni mwizi anataka kukuibia pesa zako?
 
Huo mkungu wa ndizi inaonakana umemfikia mtunza bustani wakati muafaka hata haamini nini kimetokea mbuzi kufia kwa muuza supu.
 
Niliwahi kuokota dodo mida ya jioni kabisa nikiwa nimeshakata tamaa kbs leo nalalaje na njaa baridi yote hii ya june Arusha. Kila alieniona nalo alilitamani nami nikalilinda lisiniponyoke.
Nilikuja kugundua sio dodo baada ya kufika geto maana tangu naanza kuchapa mzigo mpaka namaliza alikuwa anapokea simu kama yupo kitengo cha huduma kwa wateja vodacom, hamu iliisha na sikurudia tena.
 
Mara mbili, kwanza niliiwekea pesa 200,000 kwenye mashine ya selcom, pesa ikaingia kwenye mashine na bado kwenye airtel money ikabaki na nikaitoa.
Pili jiran yangu dukan alikuja kutoa mpesa 100,000 kabla ya kuchukua pesa akaitwa dukan kwake akaenda nikijua atarudia pesa yake ajabu hakurudi na hata siku zingine alipokuja dukan alikuja kwa mishe zingine tu.
 
Back
Top Bottom