Enzi hizo nikiwa shule, moyo ukamndondokea binti fulani matata sana wa kihaya kwa jina Methodia....
Sasa naanzaje kumface? kijasho kikanitoka! Mara wazo likanijia, nikanunue karatasi mbili za barua zenye michoro ya moyo huku mioyo mingine ikiwa imechomwa mishale nimundikie barua.
Kidume nikaanza kuandika riwaya jinsi nilivomzimia Methodia, nakumbuka prepo yote iliisha kwa kushuka mashairi matamu matamu.
Kisha asubuhi yake nikaikunja nikachukua bahasha nikaipulizia pafyumu kidogo ya YOLANDA, kitu kiende na manukato fulani hivi "amazing".
Siku hiyo hata masomo hayakwenda vizuri nikiwaza kumkabidhi mtoto Metty barua jioni yake after dispersion...
Kweli jioni ilifika nikamkabidhi waraka wa Mtume Mimi kwa Methodia. Akapokea kisha tukaachana huku akili yote ikisubiri kesho yake kupata majibu.
Bondo la shule siku ile halikulika, prepo haikusomeka, usiku ukawa mrefu na nikawa mtu wa kwanza kuamka alfajiri yake!
Kilichokwenda kutokea nilikuta barua zangu kabandika ubaoni madenti wanasoma na kucheka ile mbaya............................