EINSTEIN112, Mimi yangu ndefu Sana lakini kufupisha ni kuwa nilipewa suspension o level nikiwa form four ya wiki mbili kisa nasoma tuition nje na shuleni na ilikua shule ya day.
Suspension ya pili nilipewa nikiwa advance kisa nilikuwa mmoja wa waanzisha mgomo,
Na hii nilikula ya wiki 6, na nilipewa barua ya kwenda kuisaini kwa afisa elimu wa mkoa nirudi nayo shule siku suspension ikiisha
Sasa kimbembe kilikua kuisainisha hiyo barua, maana nilimkuta afisa elimu ambae alikuwa ni mkuu wa shule katika hiyo shule niliyokuwa ninasoma mwaka mmoja uliopita kabla ya Mimi kuingia hapo form 5.
Nilipoingia ofisini kwake, hii ofisi iko katikati ya jiji , akaniambia nishuke chini nikatafute fimbo (ofisi iko ghorofani) maana hawezi kukubali shule aliyokua akiiongoza iwe na wanafunzi wasio na nidhamu kama mimi hivo alitaka aniadhibu pia,
Kweli nikashuka chini nikaenda mpaka kwa mlinzi nikamueelezea situation akanikubalia kukata tawi la mti mmoja uliokua nje ya geti pale, nikarudi ndani, sasa wakati napishana na watu wakati napanda ngazi nilikuwa najifanya nachechemea ili waone ule ni mkongojo
Nikafika mpaka juu ofisini kwake, akaniangaliaa halafu akaniambia nilikua nakupima tu nione kama Una nidhamu, akachukua barua akaisaini, basi ndio ikawa pona pona yangu, nikarudi zangu chini kwa style Ile Ile ya kuchechemea, nakumbuka Ile fimbo nilipanda nayo gari mpaka nyumbani kama ukumbusho.
Sent using
Jamii Forums mobile app