Tuliompigia kura ya Urais Magufuli, kura za ubunge na udiwani UKAWA

IFRS

JF-Expert Member
Dec 19, 2014
2,904
5,168
Katika uchaguzi wa mwaka 2015 ni moja ya chaguzi ambao hautakaa kusahulika kutokana na ushindani mkubwa kati ya Chama tawala CCM na muungano wa vyama vya upinzani UKAWA. Chama cha mapinduzi kilimsimamisha mgombea wa urais mh. John Pombe Magufuli na ukawa wakamsimamisha mh. Edward Lowassa.

Kiukweli mimi ni mmoja wapo niliyemchagua John Magufuli kwa kura ya Urais lakini nilichagua UKAWA kwenye kura ya ubunge na udiwani.

Sababu kubwa sana ya kutomchagua mgombea wa UKAWA kwenye kura ya Urais ni kutokuwa na imani na Mh Lowassa na kukatishwa tamaa na wabunge wa CCM kwenye bunge lililopita ambao badala ya kutetea maslahi ya wananchi wao walikuwa wanatetea maslahi ya Chama.

Je, mwanaJF mwenzangu ulifanya uamuzi wa kuchagua CCM kwenye urais na UKAWA kwenye ubunge na udiwani kwa sababu gani?
 
Kabla ya michango ya wengine huku ikizingatiwa kwamba kura ni siri. Je, unajutia maamuzi yako au bado unaona ulifanya maamuzi sahihi? Tuanzie hapo kwanza
Sijutii kumchagua mbunge wa cuf temeke badala ya mtemvu wa ccm. At least huyu anafanya kazi za mbunge na yupo karibu na matatizo ya wananchi.
Kuhusu urais ndio kabisa namuelewa sana JPM na nadhani nitamchagua tena uchaguzi ujao
 
Basi kama ni hivyo ni vyema ukatulia kwako ukisubir uchaguz ujao
 
Magu wengi wetu tulimchagua kwa sababu tulimwamini kuwa ni mpenda maendeleo na mwenye utu kutokana na utendaji wake kwenye wizara ya ujenzi. Wabunge na madiwani wengi tuliwachagua wa UKAWA. Kwa sasa sitaki hata kumsikia huyu Magu. Namsubiri kwa hamu 2020. Lazima nimtumbue kwenye sanduku la kura. Kutumbuana kwa zamu.
 
Mimi bashite namuunga mkono Magu na nitamchagua japo najua ni garasa na hatari kwa ustawi wa taifa
 
nlimchagua JPM. KWAKUA ANAJITOA MUANGA KILA SIKU KATIKA KUITETEA NA KUIPIGANIA TANZANIA DHIDI YA WAPIGA DILI NA MAFSADI SINCE ALIPOKUWA WAZIRI. NA SIJUTI KWA UAMUZI HUO NA NTAMCHAGUA TENA MWAKA 2025. KWANI 2020 ASHASHINDA
 
Point
 
Kwa mwendo kasi huu wa kupiga rambirambi za wahanga, najutia sana kumpa kura yangu ya uraisi huyu mheshimiwa. Sitorudia upuuzi niliofanya tena, hata wakichakachua lakini nitakuwa na amani ya moyo kutokuwa mmoja wao.
 
Back
Top Bottom