Tuliombee taifa hali ni tete

Deogratius Kisandu

Verified Member
Dec 2, 2012
1,335
2,000
barikiwa na ombi hili;

DUA au SALA au MAOMBI YA KUOMBEA WATANZANIA NA TANZANIA YETU.

Mungu mwenyezi uliyeumba Dunia ndani yake kuna nchi yetu Tanzania na sisi wananchi tunaishi katika nchi hiyo Tanzania. Umetukabidhi tumiliki kila kitu hapa Duniani kwa maendeleo ya maisha yetu ikiwemo kukutumikia wewe Mungu wetu. Nasi tumepokea vyote kwa jina la Yesu Kristo mwokozi wetu ambaye kupigwa kwake Watanzania na Tanzania yetu tumepona.

Baba Mungu nchi yetu bado inasafari ndefu ya kuwa yenye fikira mpya katika Ukombozi wa Pili wa Taifa Letu katika kulinda Amani, Upendo, Utu na Usalama wa Taifa letu bila machafuko.

Katika 1Wakorinto 14:33, Baba umesema nasi kupitia mitume kuwa "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani..." nasi Watanzania tunasimama katika Neno hili tukikuahidi kuilinda Amani ya nchi yetu Tanzania. Kwa jina la Yesu kila Mtanzania mwenzetu mwenye pepo la machafuko tutamdhibiti kwa Jina la Yesu.

Hivyo Mungu linda familia zetu, Wazee wetu, wazazi wetu, watoto wetu, Rais wetu na Viongozi wote wa kila idara. Amani yetu ndio hadhina yetu ya kesho yenye Taifa lenye Uchaji wa Mungu. Tunasema aksante Mungu kwa uweza wako, sijui tukulipe nini sisi Watanzania kwa Amani tuliyonayo, kaa nasi tena bado tunasafari ndefu ya kujenga Taifa lenye kuamini Amani na Upendo. Katika Jina la Yesu tumeomba na kushukuru. Amina

Mwl.Deogratius Nalimi Kisandu 2014
Mtumishi mdogo sana wa Mungu na Houseboy wa Roho Mtakatifu.
 

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,968
2,000
Na Wote tuseme Amina.


Shetani ashindwe na alegeee.

Ila hapo leo ungeandika Rev badala ya Mwl maana hii ipo kiroho zaidi baba Mchungaji kuliko zile thread zako nyingine halafu unaweka ya Rev.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom