MkuyuMkubwa
Member
- Sep 27, 2009
- 50
- 0
kuchagua CHADEMA akigombea urais nani? au hata CHADEMA ikiweka jiwe tuchague tu?...hata hivyo mimi naomba turejee uchaguzi wa 2005 na haya yaliyotokea ndani ya utawala wa JK....tujiulize, kwakuwa ni kweli JK kachemsha, na tunaamini tulikosea, je tungemchagua nani kati ya washindani wake wale? akina Lipumba, Mbowe, Mvungi, nk?
Nimepita sokoni, nikakuta watu wanajibishana.....mmoja anasema "yani huyu kikwete ndio bomu kweli, hebu angalia, maisha yanazidi kuwa magumu, uongozi umemshinda...kuongoza nchi kazi....ningejua wala nisingemchagua" ingawa ni maneno ya magengeni, lakini nijikuta napata swali gumu...kwamba pamoja na udhaifu mkubwa wa JK, hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?...Lipumba, Mbowe, Mrema, Mvungi, nani angekuwa nafuu? hebu tujadili kwa kupima vigezo walivyonavyo.....wasiwasi wangu ni kwamba watanzania wanapenda upinzani kuimarisha utawala, lakini viongozi wengi wa upinzani wanapwaya mno kuaminika kwa dhamana ya kuongoza dola kama viongozi mbadala....nimeona kuna wanaosema labda ndani ya CCM kwakuwa alikuwapo Salim....lakini mimi naomba kujua katika wale walioshindanishwa na JK nani ambae tungemwamini dhidi ya JK kutokea upinzani/...au ndo tuseme upinzani ujipe nafasi zaidi kujizatiti bungeni? urais baadae kabisa?
Ni vigumu kujua kama mtu anafaa uongozi au laa kabla hajapewa hiyo nafasi. Hiyo ni kwasababu kampeni za kisiasi ni kama matangazo.......bidhaa huonekana bora mpaka unapo inunua. Mfano mzuri ni huyo JK mwenyewe. So ni vigumu sana kujua nani angefaa.
Mazee hatuwezi kwanza kuwafanyia majaribio wanasiasa wote wanaoomba kuongoza nchi kisha ndipo tujue nani anafaa na nani hatufai.Kama utaratibu ungekuwa huo basi tungekesha vizazi na vizazi kuwajua viongozi wanaofaa na wasiofaa.