jonnasy
JF-Expert Member
- Dec 27, 2013
- 299
- 235
Chondechonde mheshimiwa rais usianze kuleta maigizo kwenye swala la njaa maana naona kwa kauli ulizoanza kutoa hazitofautiani na sukari ulishindwa kujua ufanye nini ukaanza kuleta hoja dhaifu eti kuna watu kumi tu ndio wanotuchezea kwenye sukari mpaka mwisho hatukuwajua hao kumi ni akina nani mwisho wa siku mpaka leo hakuna asiyejua sukari ilivyotutesa lakini tumesahau yaliyopita tutafakari kwa umakini swala la chakula hasahasa mahindi kwa maana unaweza kuishi bila sukari lakini sio chakula
Njaa ipo na kama mvua itaendelea kwa hali hii hatuhitaji tangazo lako kujua kama kuna njaa utangaze usitangaze shauri yako maana afichaye ugonjwa kifo humuumbua lakini pia dalili ya mvua ni mawingu na usipoziba ufa utajenga ukuta nilitegemea utawaambia au kuwatia moyo wananchi lakini umetoa kauli ya kishujaa kwamba hakuna njaa na wanaoandika ni wapigadili sikatai lakini swala hili ni la kitaalamu Zaidi sote tumeona hali ya mvua matamko baadhi ya viongozi akiwamo waziri mkuu akikagua maghala ya chakula vilevile mamlaka ya hali ya hewa wamekwishatuambia kua hali ya hewa sio sawasawa
Wewe ni mkristo jifunze kwa farao ijapokuwa alikuwa katili lakini lilipokuja swala la njaa alikabiliana nalo wewe ni kiongozi unaweza tumia mawazo ya wengine kuongoza sio kwamba utaonekana mpumbavu ila utakuwa unajitengenezea mazingira mazuri ya uchaguzi ujao maana nakuona umechoka na hautaki msaada wa mawazo kama farao alivyotumia mawazo ya yusufu
Mheshimiwa rais wewe ni kiongozi acha kulalama kwa wananchi wewe ukilalama wananchi wakalalama nani atamsikiliza mwenzie ni kama vile bata analalama kuku analalama mwisho wa hakuna kusikilizana jifunze kusikiliza na kuchuja teua watu unao waamini shirikiana nao hautaona urais ni mzigo kama unavyodhani wanadamu tumeubwa na vipawa tofauti tusaidiane