Tulia nae

Tulia nae

CLONEY

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
104
Reaction score
29
Ndugu zangu ukifungua MMU topic nyingi zinaonyesha jinsi gani mapenzi yanasumbua sana siku hizi,yani wanaume wanalia huku wanawake nao wanalalamika.

Wapo wengine leo wanadiriki kusema mapenzi sasa basiiii tena kumbuka kuna wengine wengi tu wanaougulia moyoni hawna hata pa kusemea.

Naamini leo hii tukiwekwa uwanjani kuimba kuhusu mahusiano yetu ya mapenzi huo mdundo wake hakuna atakaeweza kucheza maana ni majanga ya kuua mtu.

Pamoja na vilio na malalamiko hayo yote kutoka kila upande haki ya nani wapo wanaofurahia sana mahusiano yao mapenzi kabisaa hata chembe ya presha hawana kwahyo wale walioko kwenye kundi la furaha chondechonde jamani tulia kama unanyolewa ndugu yangu mapenzi yanapeleka mbio hii dunia ndo maana wengine wanaua au kujiua oohooo sio jambo dogo hilo.

Kwa bahati mbaya unakuta mtu kapata mwenza aliyetulia lakini yeye sasa duuh utadhani kalaaniwa na hajui huko nje kuna watu hawali vizur au hawana amani hata chembe kwasababu ya mapenzi,ni bora kama unaona uko na mtu sahihi tafadhali tulia ndugu.
 
Umetufikia na tumekusikia. Ila wanawake wachokozi saaana. wakiona umetulia na wako wanaona wivu wanakutega hadi basi. Wanaume wengine mtego mdogo tu wananasa hata ule ulioko wazi kweupeeeee.
 
Kwa bahati mbaya unakuta mtu kapata mwenza aliyetulia lakini yeye sasa duuh utadhani kalaaniwa na hajui huko nje kuna watu hawali vizur au hawana amani hata chembe kwasababu ya mapenzi,ni bora kama unaona uko na mtu sahihi tafadhali tulia ndugu.

maneno kuntu hayo.
 
Hata me nikimpata wa hivyo nitashikiria kwa juhudi nisianguke

Alma
 
Back
Top Bottom