Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,934
Tumeambiwa kuwa marehemu Ndugai alizuia pesa ya matibabu kwa Lisu, na kisha kumsimamisha ubunge kwa madai kuwa ni mtoro, huku Dunia nzima ikijua kuwa Lisu yu mgonjwa, tena mgonjwa majeruhi, akipitia hali hatari ya maisha yake. Sababu ya kufanya hivyo, tumeambiwa kuwa Hayati Ndugai alielekezwa kufanya hivyo na Hayati Magufuli. Na kama huo ndiyo ukweli wenyewe, hii inadhihirisha yafuatayo:
1. Tanzania haina mhimili huru wa Bunge
2. Kinachoitwa Bunge, ni kaidara tu ka ikulu ambako kanapokea maelekezo kutoka ikulu ya Rais.
3. Tanzania ina watawala matapeli wanaowadanganya wananchi kuwa kuna mhimili wa Bunge kumbe haupo, na uwepo wa Bunge na wabunge ni ufujaji tu wa pesa kwa sababu hicho kiitwacho Bunge, hakina uwezo wa kutimiza majukumu ya Bunge kama yalivyoainishwa kwenye katiba, yaani kuisimamia Serikali na kiongozi wake, ambaye ni Rais.
MAZINGIRA MABAYA YA SASA YA BUNGE:
Tunaweza kumlaumu Hayati Magufuli kwa hayo yaliyotokea wakati wa marehemu Ndugai, lakini hata leo, kuna lolote lililobadilika bungeni chini ya spika Tulia? Tujiulize yafuatayo:
1. Wakati wananchi wanaoikosoa Serikali wanatekwa na kuuawa, spika Tulia alizuia kabisa jambo hilo lisijadaliwe na Bunge, je, na yeye alielekezwa na ikulu kufanya hivyo? Maana katika hali ya kawaida, hakuna mahali popote Duniani ambapo spika angeweza kuzuia hoja kama hiyo ya wabunge kujadili yanayowasibu wananchi wanaowawakilisha.
2. Katikati ya malalamiko kutoka nchi nzima, kutoka makundi mbalimbali, chini ya Spika Tulia, bunge lake liliidhinisha na kubariki mkataba uliokuwa umekiuka sheria, maslahi ya nchi nchi na mamlaka yake, wa kuwapa wageni bandari yetu kuu ya Dar es Salaam, jambo ambalo usingelitarajia kufanywa na bunge lolote linalowasikiliza na kutetea maslahi ya wananchi na rasilimali za nchi. Je, tuamini kuwa spika Tulia alifanya hayo kutokana na maelekezo toka ikulu, ikulu ambayo ilionekana kuuteea mkataba huo kwa nguvu zote?
3. Spika Tulia aliwahi kutamka kwa uwazi na kwa kujiamini kuwa eti Bunge lipo chini ya Serikali na Rais, hivyo lazima lifanye vile Rais na Serikali wanavyotaka, je, kama huo ndio ukweli kuhusu Bunge la Tanzania, kuna haja gani ya kuwa na Bunge? Kwa nini tusibakie tu na Rais na Setikali yae?
4. Kama maspika wa Bunge wanatumika kama viranja wa Rais bungeni kwa nia ya kutekeleza maelekezo ya Rais, tuendelee kushuhudia furaha na sherehe za wananchi kila spika anapofariki, kwa sababu wananchi wanaona adui gao ameondoka?
5. Kama bunge lipo kwaajili ya kutekeleza maelekezo ya Rais, tuna mashaka yoyote kuhusu mahakama zetu ambazo nazo zinaonekana wazi kutofanya kazi kwa weledi na uhuru wa fikra katika kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kusimamia haki?
6.Kama Bunge lenyewe ndiyo la namna hii, hivi hata uchaguzi huo unaofuata una maana gani kwa wananchi wa Tanzania? Kwa nini tupoteze muda wetu kwenda kuchagua puppets wa Rais ambao jukumu lao kubwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais? Kwa nini tusiutumie muda wetu huu kuhangaika na upatikanaji wa katiba itakayoiwezesha nchi kuwa na Bunge katika maana halisi ya Bunge?