Bwana bwana.
Acha mchezo na hofu, ishu ilivyochanganya nilipata kitripu cha Mombo basi nikaenda nikakaa wiki moja.
Ile kurudi hali si hali, kubanwa kifua , baridi n.k....... Acha ninywe malimao , tangawizi na kitunguu saumu .... Sikuwahi kujua kuwa malimao ukiyasaga na maganda na mbegu zake yanapita kooni.....yalipita.
Nilikuwa na gogo nne za grevilia nilipanga kumpa mtu apasue, nikachana mwenyewe ndani ya wiki...... Mchakamchaka, kichura push-up s........ Mtu ukifikiria kufa unaogopa sana.
Lakini hata hivyo vijana naona wanashukuru kuwa huu mchanganyiko wa malimao, tangawizi na vitunguu saumu umerudisha kwa kiasi chake heshima ya ndoa as kitandani performance imepanda kidogo.