Tukumbushane adhabu za walimu wetu wa shule ya msingi wa miaka ya 1980 - 2000

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
431
310
Mimi nimesoma Kirumba primary bwana alikuwepo mwalimu mkuu jina lake Mwl. Jirabi huyu baba alikuwa anachapa bwana tena akikuchapa ni lazima ushike masikio.
 
Kupiga magoti na kuita mvua..

Kuinama na kushika masikio..

Kupigwa na Rula kwenye vidole vya mikononi..

Kuinama na kushika vidole vya miguuni na bonge la stick linashuka hapo kiunoni na makalioni...

Kuunganisha mikono yote na kuchapwa, ukijifanya unapooza, ticha anasema anaanza upya..

Kuchapwa stick za mgongoni...

Kukaa mkao wa Push up na walimu kama watano wanakuja na mifimbo yao kukuchapa kila mmoja atakazo..
 
Kuna mwalimu alitupa adhabu ya kulala
Uzuri ilikua jumamosi, yaani akatuwekea na walinzi bwenini wanapita kukagua kama umelala. Mnaamshwa mda wa chakula na kwenda kula kwa mstari na kurudi kulala.. Ilikia adhabu sana kwa wasiopenda kujilaza mchana
 
Nakumbuka nilipokuwa railway boarding primary kule itigi singida palikuwa na Mwl.anaitwa Nkuhi alikuwa mrefu halafu anavaa suruali fupi kipindi hicho ziliitwa Tokyo..alikuwa anafundisha hesabu ukikosa tu unaingiza kichwa ndani ya dawati kisha unapewa fimbo sita za moto...ukitaka kuinuka unainuka na dawati...wee acha bhana lkn alinisaidia sana kihesabu
 
Mi sijasoma, siujui hata mlango wa darasa ukoje ...nimekosa vitu vitamu kwakweli!
 
tapatalk_1487108621681.jpeg
 
Mimi nimesoma Kirumba primary bwana alikuwepo mwalimu mkuu jina lake Mwl. Jirabi huyu baba alikuwa anachapa bwana tena akikuchapa ni lazima ushike masikio.
Pale shule zilipokuwa shule kweli na Mwalimu alipokuwa Mzazi wa pili wa mwanafunzi. Sio leo amekuwa lover.
Pale tulipokwa tunafundishwa Sayansi Kimu na Sayansi Kilimo.
Mitihani ya kumaliza elimu ya msingi ikifanywa siku ya Jumatano. Kila msongo wa shule akiwaza kufauli kwenda special schools.
Du those time
 
Kila nikikumbuka zile adhabu yn najiskia kuchoka, they punish me for nothing sa iv nguvu zangu ndo zinaninyooshea maisha na sio hiyo elimu yao, mpk sa iv sijaona imenisaidia wapi. Najuta kuenda shule
 
Nakumbuka nilipokuwa railway boarding primary kule itigi singida palikuwa na Mwl.anaitwa Nkuhi alikuwa mrefu halafu anavaa suruali fupi kipindi hicho ziliitwa Tokyo..alikuwa anafundisha hesabu ukikosa tu unaingiza kichwa ndani ya dawati kisha unapewa fimbo sita za moto...ukitaka kuinuka unainuka na dawati...wee acha bhana lkn alinisaidia sana kihesabu
Pole mkuu I feel your pains, mtu akinifanyia hivi kwa mtt wangu lazma nimtoe mshipa maji
 
Back
Top Bottom