Tukumbuke zamani wale maplayers.

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
5,077
Reaction score
2,250

1972 Hawa si wachezaji wa Ngumi bali ni wachezaji wa Taifa Stars wakikaguliwa na Rais wa Sudan wakati huo.
 
Mkuu hii ilikuwa 1972 sudan wakachezea kichapo cha 3-0 ilikuwa Timu inatisha sana acha sahizi mashalobalo kibao.

Inawezekana Mkuu.......
Nilisema mwaka 75 kwa sababu kipindi hicho ndio nilikuwa nacheza mpira wa mchangani . Na timu yangu ya watoto tulikuwa tume-adopt majina ya hao wazee hapo juu kotokana na position uliyokuwa unacheza. Rafiki yangu Karigo yeye ndio alikuwa goal-keeper kwa hiyo tulikuwa tunamwita 'Hassan Mlapakolo"
 
Hii ilitokana Na kufanana Kwa Jezi Za Timu uwanjani, ni kweli timu nyingi zilikuwa zikimiliki jezi loji moja tu, that's why inarushwa Shilingi timu moja inavua top yake, but si kweli Kwamba seventh Timu ya Taifa haikuwa Na Jezi..

Naweka sawa tu ..
 
Anaye mtmbulisha Rais Nimeir ni Nahodha wetu Abdulhaman Jumaa!

Kutoka kushoto ni beki Abdallah Mohamed"CHUMA",anayefutia ni beki Said Zimbwe;na anayefutia ni mshmabuliaji Abdallh Kibaden Mputa;huyo anayeonekana kichwa tu kama nipo sahihi ni mshambuliaji Juma Masementi!

Hao walikuwa wana ujua mpira mno na miili mikubwa ukikutana nao utadhani wacheza mieleka;siku hizi wachezaji wetu hawana kabisa miili!
 

Umejitahidi sana kuelezea hii kitu chukua LIKE zako 12.
 
Said Zimbwe? mbona kama miaka ya 80 (mpk early 90's) mimeshawahi kumuona akicheza. are u sure? Said Omar Zimbwe, right? alikuwa beki , ana kichwa "kirefu" hivi. tena beki wa pembeni km Garry Neville
 
Wa kwanza kutoka kushoto ni Abdallah Chuma alikuwa ni Centre Half (No 5) wa timu ya taifa kwa miaka 10, alikuwa akitokea timu ya Bandari Mtwara, anafuatia Zimbwe kutoka moja ya timu za Tanga sina uhakika kati ya Costal Union na African Sports, anafuatia Kitwana Manara Centre Forward wa timu ya Yanga na Taifa, anayetambulisha wenzake ni Abdulrahman Juma alikuwa anacheza namba 6 Yanga na timu ya taifa. Anaeonekana kichwa tu ni Abdallah Kibaden alikuwa anacheza namba 10 Simba na timu ya taifa
 
Said Zimbwe? mbona kama miaka ya 80 (mpk early 90's) mimeshawahi kumuona akicheza. are u sure? Said Omar Zimbwe, right? alikuwa beki , ana kichwa "kirefu" hivi. tena beki wa pembeni km Garry Neville

Huyo unayemzungumzia wewe ni majina tu!Huyu wa miaka ya 90 alicheza African Sport na akina Ally Mwaliza na akina Bakari Tutu!

Kama nipo sahihi Zimbwe huyu sasa ni marehemu na kafa miezi 3 iliyopita(nipo tayari kusahihishwa kwa hilo)
 

I salute you!
Mkuu Hussein Njovu!
Abdallha Kibaden sio huyu wa 3 hapa akimfutia Zimbwe?Na yule mwenye kichwa kile sio Jumanne Masementi?

Hawa nilikuwa nahaidiwa kwenda kuwaona lkn kwa masharti lzm nifanye vyema shuleni,motivation ya kuona soka hili la hali la juu toka kwa Mzee wangu(RIP)lilinifanya nisome kwa bidii mno shuleni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…