John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 214
Tukumbuke Nguzo Kuu za Ukristo
Kama tunavyojua, msingi wa Ukristo ni Yesu. Yesu Kristo Bwana ndiye msingi wenyewe.
Yeye huitwa jiwe kuu la pembeni, na mwamba ambao juu yake sisi sote tumewekwa. Pasipo Yesu hakuna ukristo. Yeye ndiye msingi wa imani ya Kristo.
Aidha, kikawaida, msingi ukishakaa chini, huwa nguzo zinafuata juu yake. Kazi ya nguzo ni kulifanya jengo liweze kushikamana na kusimama vema kutoka juu kwenye paa, hadi chini kwenye msingi.
Hivyo, hata kiroho katika ukristo, ukishaweka msingi wa nyumba yako ya kiroho, fahamu pia moja kwa moja kuwa utanyanyua na nguzo zake, ili kuliunda jengo lako la kiroho. Nguzo hizo ziko saba.
Nguzo saba za ukristo ni upendo, maombi, neno, ushirika, utakatifu, uinjilisti, na utoaji.
Hebu tuangazie hizo nguzo saba, moja baada ya nyingine.
UPENDO
Ni wajibu wa kila muumini aliyekombolewa na Kristo, pindi tu alipookoka aanze kukua ki-upendo. Hii ndiyo nguzo mama, kwa sababu Mungu mwenyewe ni Upendo (1Yohana 4:8).
Muumini anapaswa kufahamu kuwa, upendo wa ki-Mungu siyo kama ule wa kibinadamu wa kupenda wanaokupenda, hapana. Huu ni upendo unaozidi, usio na sharti la kujitoa, ambao unapenda hadi maadui, na kuwaombea wanaokuudhi.
Mtu asiyejijenga katika nguzo hii, haijalishi atajitaabisha vipi kwa Kristo, kazi yake itakuwa ni ya hasara siku ile ya mwisho.
Kitabu cha 1Wakorintho 13:1-13, kinasema:
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
MAOMBI
Ili maisha ya mkristo yasimame vema, maombi ni nguzo nyingine inayomkamilisha. Biblia inasema maombi yanapaswa yawe ni jambo la daima (kila siku).
Wakolosai 4:2 "Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani". Maombi ni sawa na maji mwilini, au mafuta kwenye gari, vikikosekana hivi vitu hakuna utendaji kazi wowote utakaoendelea. Vivyo hivyo ukristo wako usipokuwa wa maombi, hautaendelea sana. Utakufa tu siku moja.
Ili tujengeke vizuri, kiwango cha chini Bwana alichotaka tuombe kwa siku ni saa moja (Mathayo 26:40). Bwana Yesu alikuwa mwombaji, mitume walikuwa waombaji, sisi yatupasa tuweje?
NENO
Ukishaokoka, jambo linalofuata ni kuwa karibu na biblia yako. Katika hiyo utapata kuelewa mpango kamili wa Mungu katika maisha yako. Huku ukisaidiwa na walimu na wakufunzi wako kwenye usomaji wako wa biblia, kama Bwana wetu Yesu alivyokuwa mdogo, akifanya bidii kuwasikiliza walimu wake.
Kujifunza na kusoma kunapaswa kuwe ni tendo la kila siku. Neno ni kama chakula na maombi ni maji. Hivi viwili ndivyo vinakukuza kiroho na kukujenga nafsi. Hupaswi kuacha kusoma biblia. Mkristo asiyeifungua biblia yake ni rahisi sana kuchukuliwa na upepo wa ibilisi kwa mafundisho potofu. Hii ni kwa sababu hamjui Mungu.
Hekima, maarifa, imani, ufahamu, na mamlaka vinatoka katika kulijua Neno na mafundisho. Hivyo soma biblia kila siku, pia sikiliza mafundisho kutoka kwa walimu sahihi wa kweli, kwa sababu ni muhimu sana kuvipata.
Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
USHIRIKA
Ushirika ni kukutana pamoja na wenzako kujengana. Ushirika ni umoja wa Roho katikati yetu.
Waebrania 10:25: "wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia".
Kama mtakatifu, hupaswi kujiaminisha utakuwa na utimilifu wote wa ki-Mungu ndani yako kivyako. Utahitaji kukamilishwa na wengine kwa sehemu baadhi, ndiyo hapo suala la ushirika linakuja.
Ndiyo sababu Mungu ameweka karama tofauti tofauti ili tujengane. Katika ushirika mtaombeana, kushiriki meza ya Bwana pamoja, mtafarijiana, mtasaidiana, n.k.
Pia, biblia inasema wawili walalapo watapata joto (Mhubiri 4:9-12):
9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. 10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! 11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? 12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
Muwapo pamoja kuna ulinzi wa kipekee unaongezeka juu yenu. Hivyo kamwe usijaribu ule ukristo wa kivyako-vyako. Ni lazima kuwa washirika wa kanisa. Kama kanisa la kwanza lilivyoweza kusimama kwa kanuni hiyo.
UTAKATIFU
Utakatifu ni utambulisho wa ukristo. Huwezi kuwa mkristo, halafu ukawa mwovu. Huwezi kupokea Roho Mtakatifu, halafu sifa za utakatifu usizionyeshe ndani yako. Hii ni kwa sababu maandiko yanasema, Mungu tunayemtumikia ni Mtakatifu, hivyo na sisi pia hatuna budi kuenenda katika utakatifu.
Bwana Yesu pamoja na watakatifu wa kwanza, walizingatia viwango vyote vya usafi na ukamilifu. Vivyo hivyo na sisi, "kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu" (1Petro 1:16).
UINJILISTI
Ushuhudiaji unaanza pindi tu unapookoka. Kila mkristo ameitwa kuitenda kazi ya Bwana. Na ni lazima afanye hivyo kama sehemu ya maisha yake. Ili safari yake ya wokovu hapa duniani iwe imara, ni lazima azae matunda. Uwakili ni kazi yetu ya daima. Ukristo bila uinjilisti hauwezi kuwa imara. Kanisa la kwanza lilikuwa la kiinjilisti. Kila mmoja alitambua wajibu wake wa kuisambaza injili kila mahali, walipokuwa wakilizingatia lile agizo la Bwana: "Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno" (Matendo 8:4).
UTOAJI
Sifa ya Mungu ni utoaji, ndiyo maana mpaka leo tunanufaika na mengi katika ulimwengu wake. Hata tulipopotea katika dhambi, alijitoa kwa ajili yetu kwa kumtoa mwanawe awe fidia.
Na sisi kujitoa kihali na kifedha kwa ajili ya injili na kanisa la Kristo, ni nguzo muhimu sana. Tuna wajibu wa kusaidia katika utoaji wa huduma inayotukuza kiroho, kwa zaka na changizo zako, pamoja na kuwasaidia wasiojiweza. Ni kwa sababu, Bwana Yesu na kanisa la kwanza lilikuwa na desturi hiyo. Tazama 1Wakorintho 16:1: "Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo".
Hivyo, wote tukizitendea kazi nguzo hizo saba muhimu, tuwe na uhakika kuwa jengo letu la Imani litakuwa imara sana. Litaweza kustahili tufani na majaribu yote; jengo lililoundwa vyema, kwa utukufu wa Mungu, hata siku ile ya kuja kwake Yesu Kristo.
Nguzo hizo saba, ndiyo ukristo wenyewe. Bila kuzitendea kazi, ni sawa na kurudi nyuma katika ukristo na kudhoofika.